Brazil: Mlinda mlango aliyemuua mpenziwe asajiliwa Boa Esporte

Bruno Fernandes alipokamatwa na polisi mwaka 2010
Maelezo ya picha, Bruno Fernandes alipokamatwa na polisi mwaka 2010

Timu ya mpira wa miguu ya Brazil Ba oEsporte imepata wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wake wenye hasira pamoja na watetezi wa haki za binaadam baada ya kumsajili mlinda mlango ambaye amewahi kufungwa kwa kumuua mchumba wake miaka saba iliyopita.

Mwili wa mwanamke huyo ulipewa mbwa wakala.

Eliza Samudio aliuawa katika hoteli moja mjini in Rio de Janeiro
Maelezo ya picha, Eliza Samudio aliuawa katika hoteli moja mjini in Rio de Janeiro

Klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la pili ilithibitisha kusajiliwa kwa Bruno Fernandes katika mkutano na waandishi wa habari licha ya kupata upinzani mkubwa kutoka kwenye mitandao ya kijamii na wahisani wa timu hiyo.

Mchezaji huyo alifungwa miaka 22 gerezani kwa kumua mchumba wake aliyeitwa Eliza Samudio lakini ameachiliwa.

Mawakili wake wanasema kuwa haikuwezekana kuendelea kukaa gerezani wakati mahakama imeshindwa kusikiliza rufaa yake.

Awali Fernandes Bruno alifungwa miaka 22 gerezani lakini akatoka kabla ya muda wake kuisha
Maelezo ya picha, Awali Fernandes Bruno alifungwa miaka 22 gerezani lakini akatoka kabla ya muda wake kuisha

Bruno mwenye miaka 22 aliwahi kucheza klabu ya Flamengo ya nchini Brazil.