Biden anasema 'alifanya vibaya' kwenye mjadalala lakini hataiacha nia yake ya kuwania urais

Uvumi unazidi kutanda iwapo rais ataendelea na azma yake ya kuchaguliwa tena baada ya mjadala mbaya wa wiki jana.

Muhtasari

  • Israel yachunguza majibu ya Hamas kuhusu mpango wa kusitisha mapigano
  • Mwili wapatikana wakati wa zoezi la kumtafuta mtoto aliyeshambuliwa na mamba
  • Mama akiri kukatisha maisha ya mwanawe mwenye saratani
  • Jeff Bezos kuuza hisa nyingine $5bn za Amazon
  • Mpango wa kikatili wa Urusi wa kupata ushindi vitani
  • Nyota wa Chess, 9, kuwa mchezaji mdogo zaidi wa Uingereza
  • Binti wa rais wa Cameroon adokeza kuhusu uhusiano wa watu wa jinsia moja
  • Shambulio la Israel lamuua kamanda mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon
  • Mamilioni kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Uingereza
  • Siondoki, Biden asema, huku shinikizo la kumtaka asiwanie urais likiongezeka

Moja kwa moja

Asha Juma

  1. Droo ya kufuzu Afcon 2025 yaleta mechi za kuvutia

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mabingwa watetezi Ivory Coast watakuwa na uhakika wa kufika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 nchini Morocco lakini Nigeria wamewekwa katika kundi gumu katika droo ya kufuzu.

    Droo iliyofanyika jijini Johannesburg iliwafanya Super Eagles kumenyana na Benin, Rwanda na Libya.

    Benin, ambayo sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Nigeria, Gernot Rohr, iliwashinda majirani zao 2-1 mwezi uliopita wakati timu hizo zilipokutana katika kufuzu kwa Kombe la Dunia la Fifa 2026.

    Nigeria inatafuta meneja mpya baada ya Finidi George kujiuzulu kama kocha baada ya kushindwa na kujiunga na klabu ya Rivers United - ingawa shirikisho la soka nchini humo bado halijathibitisha rasmi kuondoka kwake.

    Ivory Coast, ambayo ilishinda taji lao la tatu la bara mwezi Februari ilipoifunga Nigeria katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) iliyocheleweshwa 2023, itamenyana na mabingwa wa 2012 Zambia, Sierra Leone na Chad.

    Ifuatayo ni droo ya Afcon 2025

    Kundi A:Tunisia, Madagascar, Comoros, The Gambia.

    Kundi B:Morocco, Gabon, Central African Republic, Lesotho.

    Kundi C:Egypt, Cape Verde, Mauritania, Botswana.

    Kundi D:Nigeria, Benin, Libya, Rwanda.

    Kundi E:Algeria, Equatorial Guinea, Togo, Liberia.

    Kundi F:Ghana, Angola, Sudan, Niger.

    Kundi G:Ivory Coast, Zambia, Sierra Leone, Chad.

    Kundi H:DR Congo, Guinea, Tanzania, Ethiopia.

    Kundi I:Mali, Mozambique, Guinea-Bissau, Eswatini.

    Kundi J:Cameroon, Namibia, Kenya, Zimbabwe.

    Kundi K:South Africa, Uganda, Congo, South Sudan.

    Kundi L:Senegal, Burkina Faso, Malawi, Burundi.

  2. Mpishi wa Ghana ashutumiwa kwa kughushi tuzo ya Guinness World Records

    .

    Chanzo cha picha, Chef Smith Cook-A-Thon/X

    Maelezo ya picha, Ebenezer Smith alijaribu rekodi ya dunia ya kupika bila kukoma mapema mwaka huu

    Mpishi mmoja raia wa Ghana aliyedai kuvunja rekodi ya dunia ya kupika kwa muda mrefu bila kukoma na mtu mmoja amekamatwa kutokana na mzozo kati yake na mfadhili wake.

    Ebenezer Smith alifanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne na kutangaza kuwa ndiye mmiliki mpya wa rekodi ya dunia baada ya kupika mfululizo kwa saa 802 na dakika 25.

    Aliwasilisha cheti kinachodaiwa kutoka Guinness World Records (GWR) kilichomthibitisha kama mmiliki wa rekodi hiyo.

    Lakini siku ya Jumatano, msemaji wa GWR aliiambia BBC Pidgin madai hayo "si ya kweli" na kuongeza kuwa "sio cheti chetu".

    Katika majibu mengine kwa chombo cha habari cha Ghana, GWR pia ilieleza kuwa hawakujua kuhusu jaribio lake na kwamba hawakupokea maombi kutoka kwake.

  3. Israel yachunguza majibu ya Hamas kuhusu mpango wa kusitisha mapigano

    Hakujawa na maendeleo kuelekea usitishaji vita tangu tangazo la Biden wiki tano zilizopita

    Chanzo cha picha, Reuters

    Israel inasema inafuatilia kwa karibu jibu la Hamas kuhusu mpango wa kusitisha mapigano Gaza ulioainishwa na Rais Biden mwishoni mwa Mei.

    Hatua hii inakuja baada ya uongozi wa kisiasa wa Hamas kusema kuwa umewasiliana na wapatanishi Misri na Qatar "kuhusu mawazo" ambayo imekuwa ikijadili kwa lengo la kufikia makubaliano.

    Hadi sasa Hamas imedai kukomesha vita na kuondolewa kikamilifu kwa wanajeshi wa Israel kutoka Gaza.

    Israel inasema itakubali kusitishwa kwa muda kwa mapigano hayo hadi itakapowaondoa Hamas.

    Rais Biden alisema mpango huo alioutaja ulitokana na pendekezo la la Israel. Awamu ya kwanza itajumuisha "usitishaji kamili", kuondolewa kwa vikosi vya IDF kutoka maeneo yenye watu wengi na kubadilishana mateka kwa wafungwa wa Kipalestina.

    Awamu ya pili itahusisha "kukomesha kabisa uhasama" na awamu ya tatu mpango mkubwa wa ujenzi mpya wa Gaza na kukamilika kwa urejeshaji wa mabaki ya mateka waliokufa.

    Taarifa ya pamoja kutoka ofisi ya waziri mkuu wa Israel na shirika la ujasusi la Mossad Jumatano usiku ilisema wapatanishi hao "wamewasilisha kwa timu ya mazungumzo ya [Israel] matamshi ya Hamas kuhusu mpango wa mateka". "Israel inatathmini matamshi hayo na itawasilisha jibu lake kwa wapatanishi," iliongeza.

    Afisa mkuu wa Palestina aliiambia BBC siku ya Alhamisi kwamba Hamas imeachana na sharti la kusitisha mapigano kabisa ili kubadilishana masharti mapya kuhusiana na kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kutoka eneo la mpaka wa kusini mwa Gaza linalojulikana kama Philadelphi corridor na kutoka kwenye kivuko cha Rafah kati ya Gaza na Misri.

    Marekani imeishutumu Hamas kwa kuzuia maendeleo kuelekea mpango wa kusitisha mapigano.

    Unaweza kusoma;

  4. Mwili wapatikana wakati wa zoezi la kumtafuta mtoto aliyeshambuliwa na mamba Australia

    Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 alionekana mara ya mwisho jioni ya Jumanne, akiogelea karibu na mji wa mbali wa Wilaya ya Kaskazini wa Nganmarriyanga.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Polisi wa Australia wamepata mabaki ya binadamu walipokuwa wakimtafuta mtoto wa umri wa miaka 12 wanayeamini alikuwa mwathirika wa shambulio la mamba.

    Mtoto huyo alionekana mara ya mwisho siku ya Jumanne, akiogelea na familia yake karibu na mji wa mbali wa Waaboriginal wa Nganmarriyanga,

    "Hizi ni habari za kuhuzunisha kwa familia, jamii na kila mtu anayehusika katika utafutaji," alisema Sgt Mwandamizi Erica Gibson, akiongeza kuwa polisi watatoa msaada kwa kila mtu aliyeathiriwa.

    Hapo awali Sgt Gibson aliiambia ABC News kwamba mamba mweusi ameonekana katika eneo la karibu.

    Kiasi cha watu 40 wa jamii hiyo waliwasaidia maafisa wa polisi katika msako wa mtoto huyo, ambao ulianza muda mfupi baada ya mtoto huyo wa miaka 12 kuripotiwa kutoweka.

    Walizunguka eneo hilo kwa miguu, kwa mashua na kwa kutumia helikopta, walipita kwenye ardhi ngumu yenye mimea minene na njia nyembamba ya maji yenye kupindapinda.

    Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa iwapo mamba anayeshukiwa kumshambulia mtoto huyo alipatikana.

  5. Mama akiri kukatisha maisha ya mwanawe mwenye saratani

    .

    Chanzo cha picha, PA Media

    Mama mmoja amekiri kwamba alimpa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka saba, ambaye alikuwa akiugua saratani, kipimo kikubwa cha "morphine" ili kukomesha mateso anayopitia na "kumaliza maisha yake kimya kimya."

    Antonia Cooper, kutoka Abingdon, Oxfordshire, alisema mwanawe Hamish alikuwa na saratani ya hatua ya nne na alikuwa katika "maumivu makali" kabla ya kufariki mwaka 1981.

    Mama huyo sasa anaugua saratani, kulingana na kile alichosema wakati wa mahojiano na BBC Radio huko Oxford, kama sehemu ya jaribio linalolenga kubadilisha sheria na kuruhusu "kusaidiwa kufariki dunia" kwa watu wanaoteseka.

    Kusaidia mtu kufariki dunia, au kumsaidia mtu mwingine kimakusudi kumaliza maisha yake, ambayo pia huitwa "euthanasia" au "kumaliza maisha ya mtu kimakusudi", ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

    Hali ya mtoto huyo iligunduliwa akiwa na umri wa miaka mitano, na awali madaktari walimwekea makataa ya miezi mitatu, lakini mama yake alisema kwamba baada ya miezi 16 ya matibabu ya saratani "ya kutisha" katika Hospitali ya Great Ormond Street, Hamish aliendelea kuishi lakini alianza kuteseka kwa maumivu makali.

    Akaongeza: "Usiku mmoja aliposema ana maumivu makali, nilimwambia: Je! unataka nikuondolee maumivu haya? Akasema: Ndiyo, tafadhali, mama."

    Anasema: "Nilimpa, kupitia Hickman catheter, dozi kubwa ya morphine, ambayo ilimaliza maisha yake kwa amani.

    Soma zaidi:

  6. Jeff Bezos kuuza hisa za thamani ya $5bn za Amazon

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos anasema atauza hisa nyingine milioni 25 katika kampuni kubwa ya teknolojia, yenye thamani ya karibu $5bn (£3.9bn).

    Hii inawadia baada ya thamani ya soko la hisa ya kampuni hiyo kufikia rekodi ya juu siku ya Jumatano.

    Mnamo mwezi Februari, alitangaza kwamba atauza hisa za Amazon zenye thamani ya karibu $8.5bn.

    Hiyo ilikuwa mara ya kwanza tangu 2021 kwa Bw Bezos kuuza hisa za Amazon.

    Hisa za kampuni hiyo zimeongezeka kwa zaidi ya 30% mwaka huu kwa matarajio kwamba kuongezeka kwa mahitaji ya teknolojia ya akili bandia (AI) kutaongeza mapato katika biashara yake ya ‘cloud computing’.

    Mwezi uliopita, hesabu ya soko la hisa la Amazon ilipanda $2tn kwa mara ya kwanza.

    Hata hivyo, bado iko nyuma ya makampuni mengine makubwa ya teknolojia ya Nvidia, Apple na Microsoft, ambayo yote yamevuka $3tn.

    Amazon iliripoti mapato makubwa ya robo mwaka mwishoni mwa Aprili, ambayo yalionyesha dau la kampuni kwenye AI ilikuwa likizaa matunda.

    Bw Bezos alijiuzulu kama mtendaji mkuu wa kampuni hiyo mnamo 2021 na kwa sasa ndiye mwenyekiti wake mkuu na anasalia kuwa mwanahisa mkuu.

    Alianzisha Amazon mwaka wa 1994 katika karakana huko Bellevue, Washington, wakati mtandao ulikuwa bado mchanga.

    Kampuni hiyo ilianza kama muuzaji vitabu mtandaoni, na kupigia debe mkusanyiko mkubwa zaidi wa vitabu kwa njia ya kielektroniki duniani.

    Tangu wakati huo Amazon imekuwa mojawapo ya makampuni yanayoongoza duniani ya rejareja na ‘cloud computing’.

    Pia alianzisha kampuni ya roketi ya Blue Origin, ambayo mnamo mwezi Mei ilituma wateja sita mwisho kabisa mwa anga la mbali.

    Bw Bezos ndiye mtu wa pili tajiri zaidi duniani, kwa mujibu wa orodha ya Mabilionea ya Forbes, akiwa na utajiri wa takriban $214bn.

    Soma zaidi:

  7. Ukraine inayaita ‘mashambulizi ya kikatili’: Mpango wa kikatili wa Urusi wa kupata ushindi vitani

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Katika mstari wa mbele, wanajeshi wa Ukraine hutumia picha kuelezea mbinu za Urusi wanazokabiliana nazo kila siku.

    Wanayaita "mashambulizi ya kikatili": mawimbi ya wanajeshi wa Urusi yanayokuja kwenye nafasi zao za ulinzi, wakati mwingine karibu mara kadhaa kwa siku.

    Lt Kanali Anton Bayev wa Brigedi ya Khartia ya Walinzi wa Kitaifa wa Ukraine anasema wimbi baada ya wimbi linaweza kutokea ndani ya saa chache tu kwenye maeneo ya mstari wa mbele kaskazini mwa Kharkiv.

    "Warusi hutumia wanajeshi hawa katika hali nyingi ili kuona mahali ambapo silaha zetu zilipo, na kuandama vitengo vyetu kila wakati," alisema.

    "Watu wetu wanasimama kwenye nafasi zao na kupigana, na wakati mawimbi manne au matano ya adui yanapokujia kwa siku, ambayo lazima uyaharibu bila mwisho, inakuwa kazi ngumu sana - sio tu kimwili, bali pia kisaikolojia."

    Mbinu hii imesababisha hasara kubwa kwa Urusi tangu Moscow ilipoanzisha mashambulizi yake ya hivi punde miezi miwili iliyopita.

    Takriban wanajeshi 1,200 wa Urusi walikuwa wakiuawa au kujeruhiwa kila siku mwezi Mei na Juni, kiwango cha juu zaidi tangu kuanza kwa vita, kulingana na maafisa wa Magharibi.

    Wale wanaoshambulia kawaida huonekana haraka na ndege zisizo na rubani na Warusi huacha maiti zao na majeruhi kwenye uwanja wa vita, Lt Kanali Bayev anasema. "Kazi yao kuu ni mashambulizi ya nyama na sisi kuwa na uchovu wa ajabu."

    Mbinu hiyo ni ishara kwamba Urusi inatafuta kutumia vyema fursa wanayopata.

    Huko Pokrovsk katika eneo la Donetsk, Kapteni Ivan Sekach kutoka Brigedi ya 110 ya Ukraine analinganisha kile anachokiona na mkanda wa kusafirisha mizigo unaoleta Warusi kuuawa, ingawa bado unawaruhusu kusonga mbele polepole.

    Urusi inafaidika na idadi kubwa ya watu kuliko Ukraine. Baadhi ya walio katika mashambulio hayo ni wafungwa wa zamani, lakini Urusi pia inaweza kusajili kupitia malipo ya mara moja, wakati mwingine maelfu ya dola.

    Na kumekuwa na malalamiko kutoka upande wa Urusi kuhusu wanajeshi waliojeruhiwa kulazimika kurudi kwenye mapigano.

    Video moja inaonyesha makumi ya wanaume, wengine wakitembea kwa magongo, wakiomba makamanda wao kwa sababu wanasema wamejeruhiwa na wanahitaji matibabu ya hospitali, lakini badala yake wanarudishwa kwenye mapigano.

    Haya yote, maafisa wa Magharibi wanasema, ina maana kwamba Moscow inaweza kuendelea kuwaleta wanajeshi, hata kama wana mafunzo duni, moja kwa moja kwenye mstari wa mbele kwa kiwango kile kile wanachouawa au kujeruhiwa.

    Pia unaweza kusoma zaidi:

  8. Nyota wa Chess, 9, kuwa mchezaji mdogo zaidi wa Uingereza

    .

    Chanzo cha picha, Simon Walker

    Mchezaji wa chess mwenye umri wa miaka tisa anatazamiwa kuweka historia ya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuiwakilisha Uingereza kimataifa katika mchezo wowote.

    Bodhana Sivanandan, kutoka Harrow, kaskazini-magharibi mwa London, atajiunga na Timu ya Wanawake ya Uingereza kwenye Olympiad ya Chess huko Hungary baadaye mwaka huu.

    Yeye ni mdogo kwa takriban miaka 15 kuliko mchezaji mwenzake mwenye umri mdogo zaidi, Lan Yao mwenye umri wa miaka 23.

    "Niligundua jana baada ya kurejea kutoka shuleni, wakati baba yangu aliniambia," Bodhana aliambia BBC. "Nilikuwa na furaha. Natumai nitafanya vyema, na kupata tuzo nyingine."

    Malcolm Pein, meneja wa timu ya chess ya Uingereza, anasema msichana huyo wa shule ndiye mwana Chess wa Uingereza wa ajabu kuwahi kutokea.

    "Inafurahisha - yuko mbioni kuwa mmoja wa wachezaji bora wa Uingereza kuwahi kuonekana," alisema.

    Hata hivyo babake mtoto huyo mwenye umri wa miaka tisa, Siva, anasema haelewi ni wapi bintiye alipata talanta yake.

    "Mimi ni mhitimu wa uhandisi, kama vile mke wangu, lakini sijui mchezo wa chess," aliiambia BBC. "Nilijaribu michezo kadhaa ya ligi, lakini nilikuwa nikifanya vibaya sana."

    Bodhana alisema, "Wakati fulani rafiki wa baba yangu alipokuwa akirejea India, alitupatia baadhi ya mifuko michache [yenye vitu]," Bodhana alisema. "Kulikuwa na ubao wa chess, na nilipendezwa na vipande hivyo nikaanza kucheza."

    Anasema chess humfanya ajisikie "vizuri" na humsaidia "vitu vingine vingi kama hesabu na jinsi ya kuhesabu".

    Pia unaweza kusoma:

  9. Binti wa rais wa Cameroon adokeza kuhusu uhusiano wa watu wa jinsia moja

    .

    Chanzo cha picha, Brenda Biya/Instagram

    Binti wa rais wa Cameroon amesambaza picha akiwa anambusu mwanamke mwingine, jambo ambalo limezua hisia tofauti katika nchi ambayo mahusiano ya watu wa jinsia moja ni kinyume cha sheria.

    Picha hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa Instagram inaonyesha Brenda Biya mwenye umri wa miaka 26 akimkumbatia mwanamitindo wa Brazil Layyons Valença.

    "Ninakupenda kupita maelezo na ninataka ulimwengu ujue," Biya aliandika, akiongeza emoji ya mapenzi.

    Baba yake mwenye umri wa miaka 91, Paul Biya, alikua rais wa Cameroon mwaka 1982 na ni mmoja wa viongozi waliotawala kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.

    Wale wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja au mahusiano ya aina hiyo katika taifa hilo la Afrika ya Kati wanakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.

    Bi Biya - mwanamuziki anayeishi ng'ambo anayejulikana kwa jina la King Nasty - hakutaja wazi jinsia yake alipochapisha picha ya busu hilo.

    Hata hivyo, muda baada ya picha hiyo kuchapishwa, Bi Biya alishirikisha makala kutoka Le Monde, ambapo gazeti la Ufaransa liliripoti kwamba "amejitokeza".

    Pia alishirikisha ujumbe mwingine kutoka kwa watu wakionyesha kumuunga mkono.

    Mwanaharakati wa Cameroon aliyebadili jinsia, Shakiro alikuwa miongoni mwa waliomsifu Biya, akisema ujumbe wake wa Instagram unaweza kuwa "mabadiliko kwa jumuiya ya LGBTQ+ nchini Cameroon".

    Shakiro alisema Bi Biya "sasa anajiweka kama sauti ya mabadiliko ya kijamii katika nchi ambayo miiko imekita mizizi".

    Kwa sasa Shakiro anaishi Ubelgiji. Alitafuta hifadhi huko baada ya kuhukumiwa kwa "jaribio la mapenzi ya jinsia moja" nchini Cameroon.

    Ingawa Biya amesifiwa na watu wengine, watumiaji kadhaa wa mitandao ya kijamii nchini Cameroon walijibu ujumbe wake kwa maoni ya chuki dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

    Baadhi wameuliza ikiwa Bi Biya alishirikisha picha hiyo ili kuzua gumzo, ikizingatiwa sifa yake ya kuweka ujumbe kwenye mitandao ya kijamii ambao huzua mijadala miongoni mwa raia wa Cameroon.

    Soma zaidi:

  10. Shambulio la Israel lamuua kamanda mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon

    .

    Chanzo cha picha, Hezbollah

    Hezbollah imesema mmoja wa makamanda wake wakuu aliuawa katika shambulio la anga la Israel kusini mwa Lebanon, huku kundi hilo la waasi linaloungwa mkono na Iran likilipiza kisasi kwa msururu wa makombora dhidi ya Israel.

    Mohammed Nimah Nasser ndiye mjumbe mkuu wa hivi punde zaidi wa Hezbollah kulengwa na Israel katika kipindi cha takriban miezi tisa ya ghasia za kuvuka mpaka ambazo zimezua hofu ya vita vya pande zote.

    Hezbollah ilisema kuwa imerusha roketi na makombora 100 katika vituo vya kijeshi vya Israel "kama sehemu ya kukabiliana na mauaji". Jeshi la Israel lilisema kuwa makombora kadhaa yaliyoanguka katika maeneo ya wazi yalizua moto, lakini hakuna majeruhi yoyote yaliyoripotiwa.

    Jeshi lilisema Nasser aliamuru Kitengo cha Aziz cha Hezbollah, ambacho kinahusika na kurusha roketi kutoka kusini-magharibi mwa Lebanon, na kumshutumu kwa kuongoza "idadi kubwa ya mashambulizi ya kigaidi".

    Pia ilimtaja"mwenzake" Taleb Sami Abdullah, kamanda wa kitengo kingine ambaye mauaji yake yalifanyika mwezi uliopita yaliifanya Hezbollah kurusha Zaidi ya roketi 200 na makombora kaskazini mwa Israel kwa siku moja.

    Tangu wakati huo, kumekuwa na msururu wa juhudi za kidiplomasia za kupunguza mvutano, huku Umoja wa Mataifa na Marekani zikionya kuhusu matokeo yanayoweza kuwa mabaya ya vita ambavyo vinaweza pia kuvuta Iran na makundi mengine washirika.

    Kumekuwa na kurushiana risasi karibu kila siku katika mpaka wa Israel na Lebanon tangu siku moja baada ya kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza tarehe 7 Oktoba.

    Hezbollah imesema inafanya kazi katika kuunga mkono kundi la Palestina ambalo pia linaungwa mkono na Iran. Vikundi vyote viwili vimetangazwa kuwa mashirika ya kigaidi na Israel, Uingereza na nchi zingine.

    Soma zaidi:

  11. Mamilioni kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Uingereza

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mamilioni ya wapiga kura wanatazamiwa kupiga kura zao katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa Julai nchini Uingereza tangu 1945.

    Vituo vya kupigia kura, vilivyowekwa katika majengo kama vile shule za mitaa na kumbi za jumuiya, vitafunguliwa kati ya 07:00 na 22:00 BST siku ya Alhamisi.

    Takriban wapiga kura milioni 46 wanastahiki kuwachagua wabunge 650 katika Bunge la Chini.

    Matokeo ya kila eneo, au eneo bunge, yatatangazwa usiku kucha na hadi Ijumaa asubuhi.

    Vyama vya kisiasa vinatazamia kushinda zaidi ya nusu ya viti, 326, ili kuunda serikali ya walio wengi.

    Uchaguzi huo, ulioitishwa na Waziri Mkuu Rishi Sunak mwezi Mei, unafanyika chini ya mipaka ya maeneobunge mapya kufuatia tathmini iliyopangwa ili kuzingatia mabadiliko ya idadi ya watu.

    Mipaka hiyo mipya, kulingana na takwimu za usajili wa wapiga kura, imeifanya Uingereza kuwa na wabunge 10 zaidi, na kufikisha jumla ya viti vyake hadi 543.

    Idadi ya viti nchini Wales imepungua kwa viti vinane hadi 32, huku jumla ya viti vya Scotland ikishuka kutoka 59 hadi 57. Ireland ya Kaskazini imesalia sawa na 18.

    Mtu yeyote aliye na umri wa miaka 18 au zaidi anaweza kupiga kura, mradi tu amesajiliwa na ni raia wa Uingereza au raia anayehitimu wa Jumuiya ya Madola au Jamhuri ya Ayalandi. Usajili ulifungwa tarehe 18 Juni.

    Kufuatia mabadiliko ya kisheria mwaka wa 2022, takriban raia milioni mbili wa Uingereza ambao wamekuwa wakiishi nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 15 waliweza kujiandikisha kupiga kura.

    Soma zaidi:

  12. Siondoki, Biden asema, huku shinikizo la kumtaka asiwanie urais likiongezeka

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Rais wa Marekani Joe Biden alifanya kazi ya kuwatuliza Wanademocrats na wafanyakazi wakuu kwenye kampeni yake siku ya Jumatano, kwani ripoti zilidokeza kwamba alikuwa akiangazia mustakabali wake baada ya mjadala wake mbaya na Donald Trump wiki iliyopita.

    Bw Biden alikula chakula cha mchana kwa faragha na Makamu wa Rais Kamala Harris katika Ikulu ya White House huku uvumi ukiongezeka iwapo angechukua nafasi yake kama mgombeaji wa chama katika uchaguzi wa Novemba.

    Wawili hao kisha walijiunga na kampeni ya Democratic ambapo Bw Biden aliweka wazi kuwa atasalia kwenye kinyang'anyiro hicho na Bi Harris akasisitiza kumuunga mkono. "Mimi ndiye mteule wa Chama cha Democratic. Hakuna mtu wa kuniondoa. Siondoki," alisema, chanzo kiliambia BBC News.

    Maneno hayo hayo yalirudiwa katika barua pepe ya kuchangisha pesa iliyotumwa saa chache baadaye na kampeni ya Biden-Harris. "Wacha niseme haya kwa uwazi na kwa urahisi niwezavyo: Ninagombea," Bw Biden alisema katika barua pepe hiyo, na kuongeza kuwa "alikuwa kwenye kinyang'anyiro hicho hadi mwisho".

    Maswali yamekuwa yakiibuka iwapo mzee huyo mwenye umri wa miaka 81 ataendelea na kampeni yake kufuatia mjadala na Trump, ambao ulikuwa na ubabaikaji mkubwa, sauti dhaifu na baadhi ya majibu ambayo yalikuwa magumu kufuatilia. Hilo lilizua wasiwasi katika chama cha Democratic kuhusu uwezo wake kushinda uchaguzi huo.

    Shinikizo la kumtaka Bw Biden kujiuzulu limeongezeka siku chache tu kwa saabu kura nyingi zinaonyesha kuwa mpinzani wake wa chama cha Republican anazidi kupata umaarufu. Kura ya maoni ya New York Times iliyofanywa baada ya mjadala huo, ambayo ilichapishwa Jumatano, ilionyesha kuwa Trump alikuwa akishikilia uongozi kwa mbali zaidi akiwa na alama sita.

    Na kura ya maoni tofauti iliyochapishwa na mshirika wa BBC wa Marekani CBS News ilionyesha kuwa Trump ana pointi tatu mbele ya Biden katika majimbo muhimu. Kura hiyo pia ilionyesha kuwa rais huyo wa zamani alikuwa anaongoza kitaifa.

    Soma zaidi:

  13. Hujambo na karibu katika matangazo yetu mubashara ikiwa ni tarehe 04/07/2024