"Ngono ni marufuku": Uvamizi uliofanywa na polisi wa Urusi kwenye karamu kusaka "shughuli za wapenzi wa jinsi moja"

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Na Amalia Zatari &Anastasia Golubeva

Jukumu, BBC Habari za Kirusi

Mamlaka ya Urusi yana fuatilia kwa karibu tafrija za ngono zinazoandaliwa na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja baada ya Mahakama ya Juu kuamua mnamo Novemba kuidhinisha vuguvugu la mapenzi ya jinsi moja na watu wa jamii ya LGBTQ kwa ujumla kama kundi la "itikadi kali."

Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na angalau visa sita vya uvamizi wa polisi dhidi ya tafrija za ngono za umma naza kibinafsi katika mikoa tofauti ya Urusi.

Baadhi ya matukio hayakuwa na uhusiano na jumuiya ya LGBTQ.

Mnamo mwezi wa Februari, polisi wa Urusi walivamia kilabu cha usiku katika jiji la Yekaterinburg, kilomita 1,500 mashariki mwa Moscow, ambapo karamu ya ngono inayoitwa "Blue Velvet" ilikuwa ikifanyika, ambapo washiriki wake walivaa vazi kuficha utambulisho wao.

Takriban maafisa 50 wa polisi walishiriki katika uvamizi huo na baadhi yao walionekana kuwa wanachama wa kikosi maalum cha usalama cha FSB, waandalizi wa karamu ya ngono kutoka jumuiya ya LGBTQ waliambia idhaa ya BBC Urusi.

Polisi waliwalazimisha washiriki wote kujifunua mavazi waliyokuwa wameyavaa kwa ajili ya kuficha sura zao na kuwataka watoe taarifa za kibinafsi za utambulisho wao, alisema Stanislav Slovikovsky, mmoja wa waandaaji.

"Waliniuliza kama kulikuwa na wanaume na wanawake wa jinsi moja kwenye karamu au [kama kulikuwa na] propaganda zozote za LGBT. Pia waliuliza ikiwa watu walitumia dawa za kulevya, ingawa walionekana kutopendezwa sana na hilo,” alisema.

Kwa zaidi ya muongo mmoja, mamlaka ya Urusi yamejaribu kuharamisha mapenzi ya jinsi moja na kuwanyang'anya wanachama wa jumuiya ya LGBTQ haki zao kwa msururu wa sheria zinazobainisha vuguvugu la LGBTQ kama itikadi kali.

f

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kuunga mkono vuguvugu la LGBTQ sasa ni uhalifu nchini Urusi, adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 10 jela.

Mnamo 2013, kamati ya Bunge ilipitisha mswada wa kupiga marufuku kile kinachojulikana kama "propaganda za LGBT," kwa ufanisi kuzuia mjadala wowote wa umma kuhusu haki za LGBT na masuala yanayohusiana.

Hata sheria kali zaidi dhidi ya LGBTQ ilitekelezwa mwaka jana.

Mnamo Julai, Bunge lilipiga marufuku kubadilisha jinsia , jambo ambalo lilikuwa halali tangu 1997, na kupiga marufuku taratibu za upasuaji zinazohusu jinsia, tiba ya homoni, na kubadilisha jinsia kwenye hati rasmi.

Novemba mwaka uliopia, Mahakama Kuu ya Urusi ililitangaza rasmi vuguvugu la LGBTQ kama "itikadi kali."

Kwa njia vugu vugu hilo liliongezwa kwenye orodha ya vikundi vyenye msimamo mkali, pamoja na Islamic State na Mashahidi wa Yehova.

Kuisaidia jumuiya ya LGBTQ sasa ni uhalifu nchini Urusi, adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 10 jela.

maonyesho ya hisia

Hakuna chochote kilichofanywa katika karamu ya "Blue Velvet" ambacho kinaweza kuwa uhalifu, Stanislav Slovikovsky aliiambia BBC.

Alidai kuwa katika tafrija yake kulikuwa na maonyesho ya mapenzi na baadhi yake yalikuwa na vipengele vya BDSM, vitendo mbalimbali vya ngono na maigizo, ambapo washiriki walialikwa kushiriki.

Wakati huo huo, Slovikovsky anasema, hakukuwa na matarajio au shinikizo kwa wageni kufanya ngono .

f
Maelezo ya picha, Waliohudhuria kwenye karamu ya "Blue Velvet" walivaa vazi kuficha utambulisho wao.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Polisi wa jiji la Yekaterinburg baadaye walitoa taarifa wakisema kwamba vikosi vya usalama vilikuwa vikifanya uvamizi wa "kuzuia" usiku huo.

"Hakuna anayeweza kukataa kwamba jumuiya ya LGBTQ inaweza kufanya mikutano yake katika mfumo wa tafrija za BDSM," alisema Dmitry Choukreev, mwanachama wa chumba cha umma cha Yekaterinburg.

Licha ya kuongezeka kwa ukandamizaji wa mamlaka dhidi ya jumuiya ya wapenzi wa jinsi moja -LGBTQ katika miaka ya hivi karibuni, "watu hawa hawajatoweka," alisema.

"Bado wanahitaji kujiliwaza na kutekeleza mawazo yao kwa vitendo. Wanaweza kusherehekea aina hizi za hafla wakiwa wamevaa kama BDSM, ambayo kwa sasa haijakatazwa ,” alisema.

Sherehe za ngono nchini Urusi zimekuwa zikifanyika katika miji mikubwa kwa muongo mmoja uliopita, haswa katika mazingira ya mijini ya watu wengi.

Inakadiriwa kuwa sehemu ndogo ya idadi ya watu hushiriki na huvutia watu wa tabaka la kati na kazi katika tasnia ya ubunifu au ufundi.

Sherehe hizo hutumika kuonyesha uhuru na uvumilivu ndani ya jamii ya Urusi, lakini kwa kupitishwa kwa sheria zinazozidi kuwa za kihafidhina, sherehe hizi zinazidi kuwa za siri.

Kashfa ya tafrija ya 'Nusu Uchi'

Ukandamizaji wa mamlaka ya Urusi dhidi ya karamu za ngono uliimarishwa mnamo Disemba baada ya mshawishi na mtangazaji wa TV Anastasiya Ivleeva kuadhinimisha sherehe ya kuzaliwa, ambapo kanuni ya mavazi ilihitaji wageni kuonekana wamevaa "Nusu Uchi."

Sherehe hiyo ilitangazwa kwenye mitandao ya kijamii na wageni walijumuisha watu mashuhuri wengi wa Urusi walioorodheshwa , akiwemo Kseniya Sobchak, binti ya mshirika na mshauri wa muda mrefu wa Vladimir Putin, Anatoly Sobchak, pamoja na mwimbaji mkongwe wa pop, Philipp Kirkorov.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Baadhi ya vituo vya televisheni vilifichua taarifa za kibinafsi za waliohudhuria sherehe za ngono.

Ingawa wengi miongoni mwa waliohudhuria walivaa nguo za juu za matundu na nguo za ndani, baadhi yao waliamua kuvaa mavazi ya kujionyesha mwili zaidi. Rapa Vacio alionekana akiwa na soksi tu kwenye sehemu zake za siri.

Picha za tukio hilo zilizua taharuki kwa wengi.

Vacio alifungwa jela kwa siku 15 kwa shtaka la kuharibu mali na kutozwa faini ya rubles 200,000 (kama dola 2,154) kwa mavazi yake.

Ivleeva mwenyewe alitozwa faini ya rubo 100,000 ($ 1,077) kwa kuandaa sherehe hiyo.

Shida zilianza kwa mwenye sherehe na wageni wake wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin alipoona picha hizo.

Baadhi ya watu mashuhuri walioshiriki katika hafla hiyo walisema awali walipanga uzuia kuonekana kwao kwenye vyombo vya habari ili kuepuk kuchukuliwa hatua za uhalifu.

Putin alizidisha maradufu maagizo kuhusu "maadili ya jadi" baada ya uchaguzi wa rais nchini Urusi ambao ulimruhusu kushinda muhula wake wa tano.

'Vitisho'

'Vitisho'

Uvamizi wa hivi majuzi dhidi ya karamu za ngono ulifuata mtindo huo: polisi walijitokeza, wakaamuru kila mtu alale chini, na kuendelea kuchukua maelezo ya utambulishi kwa waliohudhuria.

Uvamizi mwingi ulitangazwa na vyombo vya habari vya vinavyounga mkono utawala wa Kremlin , na baadhi ya vituo vya televisheni vilifichua taarifa za kibinafsi za waliohudhuria.

Ukandamizaji haukuwa tu kwa matukio ya umma . Katika angalau kesi mbili polisi walijitokeza kwenye karamu ya kibinafsi.

Baadhi ya wageni wa kiume walitishiwa kutumwa kupigana katika vita nchini Ukraine, mshiriki mmoja aliiambia BBC.

f
Maelezo ya picha, Waandalizi maarufu wa sherehe za wapenzi wa jinsi moja -queer techno ya Moscow Popoff Kitchen- wamesitisha matukio yake nchini Urusi.

Kutokana na ongezeko la uvamizi na aibu hadharani dhidi ya wapenzi wa jinsi moja waandalizi wa sherehe wameghairi kufanya matukio nchini urusi.

Mnamo Februari, karamu ya kifahari ya Moscow Popoff Kitchen, inayojulikana sana miongoni mwa jumuiya ya LGBTQ ya eneo hilo, na Kinky Party yenye mada ya ngono ilitangaza kuwa wataacha kufanya matukio nchini Urusi.

"Tumepokea onyo kwamba kuanzia sasa hakuna matukio yoyote yanayohusiana na mada ya ngono yataruhusiwa," waandaaji wa Kinky Party walisema katika taarifa.

"Haiwezekani kufanya kazi kwa kujua kwamba usalama [wa wageni wako] hauwezi kuhakikishwa," Nikita Egorov-Kirillov wa Popoff Kitchen aliiambia BBC.

"Uvamizi wote huo, vitisho, kuondoa taarifa binafsi za watu... Hili likitokea mara moja, huwezi kuwaaminisha watu kuwa chama chako kiko salama tena," alisema.