'Nchi yangu ni ndogo lakini sasa ni kitovu cha ulimwengu'

Katika eneo la Souq Waqif lenye shughuli nyingi huko Doha, msisimko na hamasa inaonekana.
Ukizunguka sokoni, unaweza kusikia lugha nyingi tofauti huku mashabiki wakipeperusha bendera za timu wanazoshabikia. Kila mara, kikundi cha watu hulipuka kwa shangwe.
Makundi ya mashabiki wa Mexico, Morocco na Argentina wao ndio haswa wanaonekana kuwa na hamasa zaidi wakifurahia milo yao na Shisha.
Kuna msanii yuko katika hatua za mwisho kuchora picha ya Lionel Messi. Watoto wadogo wanaonekana wamevalia jezi ya taifa ya Qatar.
"Watu kutoka kote ulimwenguni wako hapa sasa," Nasser, ambaye hakutaja jina lake la mwisho, ananiambia, akionyesha umati wa watu sokoni. "Kwetu sisi Waqatari - hii ni siku ya kujivunia."
Kisha macho yote yako kwenye skrini kubwa kwenye migahawa wakati sherehe ya ufunguzi inapoanza. "Siwezi kabisa kuelezea jinsi ninavyohisi. Nchi yangu ndogo sasa ni kitovu cha ulimwengu," Naji Rashed Al Naimi ananiambia.
Kitovu kwa maana ya kutazamwa na kufuatiliwa na dunia nzima wakati huu wa michuano ya kombe la duni.
Yeye ndiye mkuu wa klabu ya The Qatari Dama sokoni hapa, mchezo wa kitamaduni unaofanana na chess. Tunaketi kwenye Majlis - sebule ya kitamaduni - na marafiki zake wote wamekusanyika karibu na Runinga.
"Tumepitia mengi kufika hapa. Shida na changamoto nyingi sana," Bw Al Naimi ananiambia. Yeye na marafiki zake wana shauku ya kutuambia kuhusu ishara ya sherehe - historia ya Qatar na jinsi nchi ya Ghuba iliyokuwa jangwa zamani, kuandaa Kombe la Dunia.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Umati wa watu katika eneo la kikao wakipiga makofi wakati Amir Tamim Bin Hamad Al Thani, na baba yake, Emir wa zamani Hamad bin Khalifa Al Thani, wakiwasili.
Video ya kumbukumbu inaonyesha kiongozi huyo kijana akicheza soka jangwani. Kufikia sasa, mabishano yamefunika soka. Suaa la hivi punde lilikuwa ni marufuku ya dakika za mwisho kwa uuzaji wa bia katika viwanja siku mbili kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Pia kumekuwa na hofu juu ya jinsi mashabiki amao wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBT) wanavyotarajia kutendewa ikizingatiwa nchi hiyo inazingatia sana sheria za kiislamu (Sharia) - ambazo mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Qatar - pamoja na walivyotendewa wafanyakazi wahamiaji.
Lakini usingeweza kujua hili lilikuwa mojawapo ya Kombe la Dunia lenye utata na mjadala mkubwa.
"Hii ilikuwa ndoto, sasa unaweza kuiona mbele yako. Ninajivunia sana," Salem Hassan Al Mohanadi ananiambia. "Wale wote waliotukosoa...hatukusema chochote. Leo tumewaonyesha."
"Haya [ukosoaji] yalinisikitisha," Saad Al Badr aliniambia huku jicho moja likitazama mchezo wa Qatar-Ecuador. "Kwa miaka 12, tulikuwa na wasiwasi, bila kujua kama ingetokea au la. Ila sasa tumefika."

Hii haikuwa safari nyepesi kwa taifa hili dogo na tajiri la Ghuba. Lina mengi ya kuthibitisha bado. Kwa mwezi mmoja ujao Qatar inapaswa kuweka usawa kati ya kuwa kitovu cha dunia ikitazamwa na kila mtu na kudumisha utambulisho wake wa kitamaduni, kidini na kihafidhina.
Ni siku kubwa sio tu kwa nchi mwenyeji bali kwa eneo nzima ambapo michuano hiyo inafanyika kwa mara ya kwanza.
"Kombe hili la Dunia si la Qatar pekee," Bw Al Mohanadi ananiambia. "Pia ni la Waarabu na Waislamu wote."
End of Unaweza pia kusoma













