Safari ya Rigathi Gachagua kama Naibu wa Rais wa Kenya yafika tamati
Gachagua alitakiwa kujitetea mbele ya Bunge la Seneti mchana huu lakini wakati wake wa kujitokeza bungeni ulipofika, hakuwepo.
Muhtasari
Naibu wa Rais Rigathi Gachagua hospitalini huku Seneti ikiendelea kujadili hoja ya kumuondoa madarakani
Kesi ya kumuondoa Gachagua madarakani kuamuliwa Jumamosi
Sinwar ndiye mlengwa mkuu wa Israel huko Gaza
'Tathmini zaidi' zinaonesha Sinwar amefariki dunia, duru zaiambia BBC
Naibu Rais Gachagua ana 'maumivu makali ya kifua'- asema wakili Muite
Israel 'inaangalia uwezekano' kwamba ilimuua kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar huko Gaza
Liam Payne: Tunachojua kuhusu kifo cha nyota huyo wa muziki
Naibu Jaji: Majaji watafuata utaratibu wa katiba kesi ya Gachagua ikirejea mahakamani
Naibu Rais Rigathi Gachagua ni mgonjwa na yuko hospitalini - Wakili Paul Muite
Bangladesh yatoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa zamani Hasina
Katiba ya Korea Kaskazini sasa yaitaja Korea Kusini kuwa 'nchi hasimu'
Marekani inaifuatilia Israel kuhakikisha haiendeshi 'sera ya kuwaangamiza watu kwa njaa' huko Gaza
HRW: Tanzania izingatie haki za binadamu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa
Wanne mbaroni Tanzania kwa kumuua mume wa mdaiwa mkopo
Jeshi la Rwanda lakanusha madai ya kuwabaka wanawake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
Marekani yashambulia hifadhi za silaha za Wahouthi zilizofichwa chini ya ardhi
Rigathi Gachagua:Je, ni kesi gani haswa inayomuandama naibu rais katika seneti?
Marekani kutenga dola milioni 425 za msaada wa kijeshi kwa Kyiv, huku Australia ikipeleka vifaru 49 vya Abrams
Rigathi Gachagua: Bunge la Seneti Kenya kupiga kura kuhusu hoja ya kumuondoa madarakani Naibu Rais
Mbunge aliyewasilisha hoja ya kumuondoa naibu wa rais bungeni Kenya ajipata mashakani
Meya na watu wengine 15 waliuawa katika shambulio la Israeli kwenye mkutano wa baraza la Lebanon
Moja kwa moja
Na Asha Juma, Ambia Hirsi & Dinah gahamanyi
Tunachojua kuhusu kuuawa kwa Yahya Sinwar
Chanzo cha picha, Reuters
Haya ndiyo tunayofahamu kuhusu kifo cha kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar kufikia sasa:
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema lilimuua Sinwar kusini mwa Ukanda wa Gaza wakati wanajeshi wa IDF walipokuwa wakifanya kazi huko kufuatia taarifa za kijasusi "zilizoonyesha maeneo yanayoshukiwa ya wanachama wakuu wa Hamas"
Wanajeshi kutoka Brigedi yake ya 828 waliwaua "magaidi" watatu huko , mmoja wao alithibitishwa baadaye kama Sinwar, IDF inasema.
Alitambuliwa kupitia uchunguzi wa meno na vidole , polisi wa Israeli wanasema
Muda kamili haujabainika - IDF inasema Sinwar aliuawa jana, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz akisema aliuawa leo.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema aliuawa huko Rafah , mji ulioko kusini mwa eneo la mpaka na Misri wakati akikimbia vikosi vya IDF.
Uthibitisho wa kifo hicho ulifuatia masaa kadhaa ya uvumi, baada ya IDF kusema mapema ilikuwa inachunguza uwezekano wa kumuua.
Picha za kutisha zimekuwa zikisambaa mtandaoni leo zikionyesha mwili unaofanana sana na Sinwar - BBC bado haijaweza kuzithibitisha.
Hamas bado haijatoa maoni
IDF yasema Sinwar aliuawa siku ya Jumatano kusini mwa Gaza
Chanzo cha picha, Reuters
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limetoa taarifa likisema Kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar aliuawa na wanajeshi wake katika operesheni iliyofanyika kusini mwa Gaza jana baada ya "kuwindwa kwa mwaka mzima".
Haya yanajiri baada ya waziri wa mambo ya nje wa Israel Israel Katz kuwaambia viongozi wenzake kote duniani kuwa Sinwar aliuawa leo. Sababu ya kutofautiana kuhusu siku ya kuuwa kwake haijulikani wazi.
Katika taarifa, IDF inasema Sinwar alipanga na kutekeleza shambulio la Oktoba 7 na "alihusika na mauaji na utekaji nyara wa Waisraeli wengi".
"Yahya Sinwar aliondolewa baada ya kujificha kwa mwaka uliopita nyuma ya raia wa Gaza, juu na chini ya ardhi katika mahandaki ya Hamas katika Ukanda wa Gaza," inasema.
Jeshi la Israel linasema limekuwa likiendesha shughuli zake kusini mwa Gaza kufuatia taarifa za kijasusi "zilizoonyesha maeneo yanayoshukiwa ya wanachama wakuu wa Hamas".
Wanajeshi wa IDF kutoka Brigedi ya 828 inayofanya kazi katika eneo hilo "waliwatambua na kuwaondoa magaidi watatu", inasema, na kuongeza mchakato wa kuwatambua mmoja wa waliouawa alikuwa Sinwar.
Vita bado havijaisha, Netanyahu anasema
Tumekuwa tu kusikia kutoka kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, ambaye anaelezea Sinwar aliyehusika na "mauaji mbaya zaidi katika historia ya watu wetu tangu Holocaust".
Anasema kwamba, wakati Israeli "ilisuluhisha matokeo naye", "kazi iliyo mbele yetu bado haijakamilika" - kwani Israeli itaendelea na mapambano yake hadi mateka warudishwe nyumbani.
Akiwahutubia watu huko Gaza, Netanyahu anasema "Sinwar aliharibu maisha yenu" na kwamba sasa amekufa "Hamas haitadhibiti tena" eneo hilo, akielezea hii kama fursa kwao kujikomboa "kutoka kwa udhalimu wake".
"Kurejea kwa mateka wetu ni fursa ya kufikia malengo yetu yote na kutuleta karibu na mwisho wa vita," anasema.
Habari za hivi punde, Naibu wa Rais Rigathi Gachagua hospitalini huku Seneti ikiendelea kujadili hoja ya kumuondoa madarakani
Chanzo cha picha, Reuters
Bunge la Seneti limepiga kura kuendelea na hoja ya kuondolewa madarakani kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua bila kuwepo kwake.
"Kwa vile mchakato huu unaendana na muda kulingana na katiba, na ikizingatiwa kuwa muda unakamilika Jumamosi, fursa pekee iliyopo ni kutangaza Jumamosi kama siku ya mwisho ya kusikilizwa kwa hoja hii," Kingi alielekeza Bunge kabla ya maseneta hao kupiga kura.
Na baada ya hapo, maseneta walipiga kura ya kiutaratibu ama kukubali au
kutokubali kuendelea na hoja ya kuahirisha kikao hadi tarehe nyingine ambayo ilikuwa imependekezwa na Spika wa Bunge Amason Kingi.
Lakini baada ya kuulizwa swali la ama kukubali au kukataa, Bunge lilikataa kusongeza mbele tarehe ya kusikilizwa kwa hoja ya kumuondoa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Mawakili wa Naibu Rais waondoka Bungeni
Wakati huo huo, punde tu baada ya Bunge kuamua kuendelea na kikao cha
kujadili hoja hiyo, mawakili wanaomwakilisha Naibu Rais Rigathi Gachagua
walitoka nje ya Bunge.
"Kutokana na
uamuzi wa Seneti, sisi kama timu ya wanasheria wanaomwakilisha naibu rais
hatuwezi kuendelea kuwepo Bungeni bila maagizo. Kwa hivyo tunaondoka," alisema
Wakili Mkuu Paul Muite, anayemwakilisha Gachagua.
Wakili Mwandamizi Paul Muite alisema Rigathi Gachagua amepata maumivu makali ya kifua na kukimbizwa katika Hospitali ya Karen kwa matibabu, hivyo basi, hataweza kufika mbele ya Bunge kuhojiwa.
Kesi ya kumuondoa Gachagua madarakani kuamuliwa Jumamosi
Spika wa Bunge la Senenti nchini Kenya Amason Kingi amemuagiza Karani wa bunge hilo kuweka katika gazeti rasmi la serikali hoja ya bunge hilo kufanya kikao maalum siku ya Jumamosi.
Kufuatia uamuzi huo Kiongozi wa wengi Bungeni amewasilisha hoja ya kupendekeza kikao maalum kifanyike siku ya Jumamosi kuanzai saa tatu asubuhi ili kusikiza na kuamua hoja.
Mchakato wa kumuondoa madarakani Naibu wa Rais wa Kenya kisheria ulitarajiwa kukamilika ndani ya siku 10 baada ya Bunge la Kitaifa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Mawakili wanaowakilisha Bunge la Kitaifa kwa sasa wanaendelea kujadili kesi dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua katika Seneti licha ya Gachagua na mawakili wake kutokuwepo katika Bunge hilo.
Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ameripotiwa kuugua baada ya kupata maumivu makali ya kifua na kukimbizwa katika Hospitali ya Karen kwa matibabu siku ya Alhamisi, kulingana na wakili wake Wakili Mwandamizi Paul Muite.
Muite hivyo aliomba shauri hilo kuahirishwa hadi Jumanne wiki ijayo ili kuruhusu Gachagua kuhudumiwa ipasavyo, na baada ya hapo afikishwe mbele ya mashahidi na kuwasilisha utetezi wake katika kesi ya mashtaka.
Sinwar ndiye mlengwa mkuu wa Israel huko Gaza
Chanzo cha picha, EPA
Yahya Sinwar ndiye mlengwa namba moja wa Israel huko Gaza
na alishutumiwa kwa kuhusika kuandaa na kuongoza mashambulizi ya Oktoba 7 mwaka
jana, wakati maelfu ya watu wenye silaha walivunja uzio wa Gaza na kuua watu
1200 huku wengine zaidi ya 250 wakitekwa nyara.
Picha zilizowekwa mtandaoni zinaonyesha mtu anayefanana
na Sinwar akiwa amelala kwenye vifusi vya jengo baada ya shambulizi kali
lililotekelezwa na wanajeshi wa Israel huku akiwa na majeraha mabaya.
Inadhaniwa kuwa vipimo - vya kimwili na ya kibayometriki
- vitafanywa na Waisraeli ili kuhakikisha kama kweli ni Yahya Sinwar.
Ikiwa ameuawa, itakuwa mafanikio makubwa ya kijeshi kwa
Israeli. Sinwar, 61, aliachiliwa kutoka jela ya Israel mwaka 2011 kama sehemu
ya kubadilishana wafungwa na kuwa mtu mwenye msimamo mkali na mwenye ushawishi
mkubwa kwa Hamas ambaye alipendelea makabiliano ya silaha na Israel badala ya
mipango ya kidiplomasia.
Ilichukuliwa kuwa Sinwar amekuwa akitumia muda mwingi kwenye
mahandaki huko Gaza, akiwa anatumia mateka wa Israel kama ngao, hasa baada ya
kuwa kiongozi mkuu wa Hamas kufuatia mauaji ya Ismael Hanieyh.
Lakini kulingana na ripoti kutoka kwa IDF, hakuna mateka
waliopatikana karibu na eneo hilo.
Kifo chake hakiwezi kumaliza mara moja vita vya Israel
huko Gaza lakini kuendelea kwa operesheni za kijeshi za Israel dhidi ya Hamas
katika eneo la Palestina, ambapo mamia ya raia pia wameuawa, mwisho wa vita
hivi kunaweza kukaribia zaidi.
Habari za hivi punde, 'Tathmini zaidi' zinaonesha Sinwar amefariki dunia, duru zaiambia BBC
Kulingana na vyanzo vya BBC vinavyofahamu suala hilo, kwa
sasa 'tathmini zaidi' zinaonesha kwamba Yahya Sinwar amefariki dunia, lakini
uthibitisho wa mwisho bado unahitajika.
Baraza la mawaziri la usalama lasema kuna 'uwezekano mkubwa Sinwar amefariki', - Reuters
Wajumbe wa baraza la mawaziri la usalama la Israel
wamefahamishwa kuwa kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar ana uwezekano mkubwa kuwa
amefariki, maafisa wawili wanaofahamu suala hilo wameiambia Reuters.
Maafisa wasiojulikana pia wameripotiwa kuiambia Channel
12 ya Israel kwamba Sinwar "ameuawa".
'Adui zetu hawawezi kujificha' asema waziri wa ulinzi wa
Israel
Katika ujumbe uliowekwa kwenye mtandao wa kijamii katika
saa iliyopita, Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant amenukuu Torah akisema maadui wa
Israel hawawezi kujificha.
Gallant ameshirikisha kifungu kutoka Leviticus 26 kinachosema:
"Mtawafuatia adui zenu, nao wataanguka mbele yenu kwa upanga."
"Adui zetu hawawezi kujificha. Tutawafuata na kuwamaliza,"
Gallant anaongeza.
Habari za hivi punde, Naibu Rais Gachagua ana 'maumivu makali ya kifua'- asema wakili Muite
Wakili wa Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua, Paul Muite ameliambia Bunge la Seneti kuwa mteja wake anakabiliwa na ''maumivu makali ya kifua'' na kwamba hataweza kufika mbele ya bunge hilo.
Muite ameyasema hayo wakati Seneti linaporejelea vikao vyake kusikiza mashtaka dhidi ya Gachagua.
Gachagua alikuwa amepewa muda wa saa mbili kufika mbele ya seneti baada ya kukosa kuwasili mwendo wa saa tisa mchana leo.
Muite pia amemuomba Spika wa Seneti Amason Kingi kuwapa muda hadi Jumanne ili kumpa nafasi Gachagua kufika mbele ya maseneta kujitetea.
Haya ndiyo tunayofahamu kuhusu mashtaka dhidi ya Naibu Rais:
Kulingana na mbunge wa Kibwezi Magharibi, aliyewasilisha hoja ya kumuondoa madarakani Mutuse Mwengi, anakabiliwa na tuhuma kumi na moja.
Gachagua analaumiwa kwa kukinzana na sera za serikali na kukosa kutekeleza majukumu yake kama Naibu Rais, hivyo basi kukiuka kanuni ya uwajibikaji wa pamoja wa Baraza la Mawaziri.
Hoja hiyo ya Mutuse Mwengi pia inadai kuwa Gachagua aliingilia shughuli za ugatuzi wa kaunti, kuhujumu ugatuzi na kutishia idara ya mahakama, hatua inayokiuka kanuni ya uhuru wa idara ya mahakama.
Vilevile hoja hiyo inataja utovu wa nidhamu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi, kutomtii Rais, kuwaonea maafisa wa umma, na kushawishi vitendo vya rushwa.
Mbunge huyo wa Kibwezi Magharibi anasema kwamba Bw Gachagua alishindwa kuheshimu na kutetea Katiba, huku matamshi yake ya uchochezi yakidaiwa kukiuka Sheria ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa kwa kuendeleza chuki za kikabila.
Aidha Gachagua anadaiwa alijihusisha na ufisadi, ufujaji wa pesa na matumizi mabaya ya ofisi, kukiuka sheria za kupambana na ufisadi , kutoa taarifa za uongo na uovu na kukiuka kanuni za adhabu na sheria ya uongozi na uadilifu.
Israel 'inaangalia uwezekano' kwamba ilimuua kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar huko Gaza
Chanzo cha picha, Reuters
Jeshi la Israel linasema kuwa linaangalia uwezekano
kwamba kiongozi wa Hamas, Yahya Sinwar, ameuawa huko Gaza.
Katika taarifa, Jeshi la Ulinzi la Israel linasema kuwa
utambulisho wa "magaidi watatu waliouawa" ulikuwa bado
haujathibitishwa.
"Katika jengo ambalo magaidi waliondolewa, hakukuwa
na dalili za kuwepo kwa mateka katika eneo hilo," IDF inaongeza.
Uchunguzi wa DNA unaendelea ili kubaini kama mwili ni wa Sinwar - ripoti
Taarifa za maelezo zaidi sasa kuhusu juhudi za Israel
kuthibitisha kama imemuua Yahya Sinwar.
Afisa wa usalama wa Israel pia anasema uchunguzi wa DNA
unaendelea ili kuthibitisha kama mtu aliyeuawa alikuwa kiongozi wa Hamas, AFP
inaripoti.
Israeli itapata DNA ya Sinwar na data zingine za kibayometriki
kwenye faili kutoka wakati wake gerezani huko.
Redio ya jeshi la Israel inaripoti kuwa kisa hicho
kilitokea katika eneo lililolengwa linalofanya kazi katika mji wa Rafah kusini
mwa Gaza wakati ambapo wanajeshi wa Israel waliwaua wanamgambo watatu,
kulingana na Reuters.
Matangazo ya kijeshi pia yanasema ushahidi unaonyesha
Sinwar alikuwa mmoja wa wale waliouawa, na kwamba vipimo vya DNA vinafanywa.
Liam Payne: Tunachojua kuhusu kifo cha nyota huyo wa muziki
Chanzo cha picha, Getty Images
Nyota wa zamani wa One Direction Liam Payne, 31,
amefariki dunia baada ya kuanguka kutoka kwenye roshani ya hoteli ya
Casa Sur mjini Buenos Aires,
Argentina. Haya ndiyo tunayojua:
Polisi walienda kwenye hoteli hiyo kufuatia simu ya dharura kuhusu "mtu mwenye fujo" aliyekuwa akisababisha ‘usumbufu’
Katika simu ya dharura ambayo BBC imeisikiliza mpiga simu anasema mgeni amelewa na kutumia dawa za kulevya na wana hofu kuhusu usalama wake.
Baada ya polisi kufika eneo la tukio sauti kubwa ilisikika kutoka kwenye ua wa ndani ambapo mwili wa Payne uligunduliwa.
Mwili wa Payne umehamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini humo
·Risala za rambirambi zimemiminika kwenye mitandao ya kijamii . Mtangazaji wa X Factor Dermot O'Leary alisema Payne alikuwa "mwenye busara
na mwenye ‘moyo mchanga’
'Tumevunjika moyo', familia ya Liam Payne yasema
Familia ya Liam Payne imetoa taarifa kufuatia kifo chake:
"Tumeumia mioyoni mwetu. Liam ataishi milele mioyoni mwetu na tutamkumbuka kwa moyo wake wa fadhili, mcheshi na ushujaa.
"Tunasaidiana kadri tuwezavyo kama familia na tunaomba faragha na nafasi katika wakati huu mgumu."
Chanzo cha picha, EPA
One Direction ilishika nafasi ya tatu katika mashindano ya X Factor ya 2010, nyuma ya mshindi Matt Cardle na mshindi wa pili Rebecca Ferguson - ambaye ameelezea huzuzi yake kutokana na kifo cha Liam Payne.
Akichapisha kwenye mitandao ya kijamii, Ferguson anakumbuka "kutumiwa vibaya kwa mastaa wachanga" anapokumbuka wakati alipokutana na Payne katika kituo cha gari la moshi la Euston London na kupanda teksi kuelekea maonyesho ya X Factor.
"Siwezi kujizuia kumfikiria yule mvulana ambaye alikuwa na matumaini na akitazamia mustakabali wake mzuri mbeleni. Kama hangeingia kwenye treni hiyo na kuruka kwenye teksi hiyo naamini angekuwa hai leo.
Naibu Jaji: Majaji watafuata utaratibu wa katiba kesi ya Gachagua ikirejea mahakamani
Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu amesema iwapo mchakato wa
kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua utarejea tena mahakamani, majaji watafuata
utaratibu ulioainishwa kwenye katiba.
Mwilu alisema mchakato huo si wa kipekee kwani unafuata
mchakato wa Kikatiba na utazingatiwa kama kesi nyingine yoyote.
"Kila kitu kina mwanzo wake kwa hivyo kuhusu
mchakato wa kumshtaki naibu rais wetu sio wa kipekee," alisema.
Matamshi ya Mwilu yanawadia baada ya maombi 29
kuwasilishwa katika Mahakama ya Juu kusitisha mchakato unaoendelea wa kumtimua
naibu huyo kuendelea hadi katika Bunge Seneti.
Matumaini ya mwisho ya Gachagua kusitisha mchakato huo
yalikatizwa Jumatano baada ya ombi lake kukataliwa na majaji.
Mchakato wa kumuondoa Naibu Rais madarakani unaendelea katika
Bunge la Seneti ambapo maseneta hao wanatarajiwa kutoa uamuzi kufikia Alhamisi,
Oktoba 17.
Habari za hivi punde, Naibu Rais Rigathi Gachagua ni mgonjwa na yuko hospitalini - Wakili Paul Muite
Chanzo cha picha, Reuters
Wakili wa upande wa Naibu Rais Paul Muite amearifu Bunge
la Seneti kwamba Naibu Rais Rigathi Gachagua ni mgonjwa na kuwa yuko hospitalini.
Gachagua alitakiwa kujitetea mbele ya Bunge la Seneti
mchana huu lakini wakati wake wa kujitokeza bungeni ulipofika, hakuwepo.
Haya yamejiri baada ya kesi hiyo kusitishwa pale Naibu Rais alipokosa kujitokeza kama ilivyokuwa imepangwa.
Na baada ya kutoa taarifa ya kuwa naibu rais ni mgonjwa, Spika wa Bunge la Seneti Amason Kingi alimuuliza anapendekeza nini kifanyike:
''Mheshimiwa spika nimepata ujumbe huu muda mfupi uliopita. Naomba
kuchukua muda ili kutathmini hali ilivyo kisha nifahamishe Bunge hili hatua
itakayofuata.''
''Huu ni mchakato ambao hauwezi kusitishwa,'' Spika Kingi aliongeza kusema.
Kwa sasa kikao kimeahirishwa hadi saa kumi na moja jioni.
Theluthi mbili ya maseneta 67 wanahitajika kupiga kura kumuondoa madarakani. Gachagua anakabiliwa na mashtaka 11, ikiwa ni pamoja na rushwa, kuchochea migawanyiko ya kikabila na kudhoofisha serikali.
Kesi hiyo ilipoanza siku ya Jumatano, naibu rais alikanusha mashtaka hayo mbele ya bunge hilo.
Bangladesh yatoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa zamani Hasina
Chanzo cha picha, Getty Images
Mahakama ya Bangladesh imeamuru kukamatwa kwa waziri mkuu
wa zamani Sheikh Hasina, ambaye alikimbilia India mwezi Agosti baada ya
kuondolewa madarakani na maandamano makubwa.
Hasina anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa
Bangladesh kwa madai ya kuhusika kwake katika "uhalifu dhidi ya binadamu"
ambao ulifanyika wakati wa maandamano na mamia kuuawa.
Hasina, ambaye alikuwa akiiongoza Bangladesh kwa zaidi ya
miaka 20, alionekana kama mbabe ambaye serikali yake iliwabana wapinzani bila
huruma.
Hati za kukamatwa pia zimetolewa kwa wengine 45, wakiwemo
mawaziri wa zamani wa serikali ambao pia waliikimbia nchi.
Katiba ya Korea Kaskazini sasa yaitaja Korea Kusini kuwa 'nchi hasimu'
Chanzo cha picha, Reuters
Katiba ya Korea Kaskazini sasa inafafanua Kusini kama
"nchi hasimu", kulingana na vyombo vya habari vya serikali, katika
kutajwa kwa mara ya kwanza kwa marekebisho ya hivi majuzi ya katiba ya
Pyongyang.
Gazeti la serikali Rodong Sinmun liliripoti mabadiliko
hayo kama "hatua halali isiyoepukika", wakati ambapo mivutano kati ya
Korea iko katika kiwango cha juu zaidi kwa miaka mingi.
Korea Kaskazini siku ya Jumanne ililipua barabara na reli
zinazoiunganisha na Korea Kusini - hatua ambayo vyombo vya habari vya serikali
vilielezea kama "sehemu ya utekelezaji wa hatua kwa hatua kutenganisha
[Korea] hizo kikamilifu".
Baadhi ya waangalizi wanaona marekebisho hayo ya katiba
kama hatua ya mfano kwa kiasi kikubwa, kutokana na kiongozi wa Korea Kaskazini
Kim Jong Un kukataa kuungana mapema Desemba 2023.
Wakati huo, vyombo vya habari vya serikali viliripoti Kim
akisema kuwa uhusiano kati ya Korea Kaskazini umekuwa "uhusiano kati ya
nchi mbili zenye uhasama".
Kisha, mnamo mwezi Januari, alitangaza kuungana na Korea
Kusini kama jambo lisilowezekana, na akadokeza mabadiliko ya kikatiba kutaja
Kusini kama "adui mkuu".
Kumekuwa na msururu wa mabadilishano kati ya nchi za
Korea tangu wakati huo, haswa katika miezi michache iliyopita na kusababisha
mvutano ukiongezeka kwa kasi.
Marekani inaifuatilia Israel kuhakikisha haiendeshi 'sera ya kuwaangamiza watu kwa njaa' huko Gaza
Chanzo cha picha, Reuters
Maafisa wakuu wa Marekani wamekariri matakwa yao ya kuitaka Israel kuongeza kiwango cha misaada inayoingia Ukanda wa Gaza, kufuatia barua iliyoonya kuwa ufadhili wa silaha za Marekani unaweza kuathirika ikiwa mpango huo hautaboreshwa.
Katika muda wa siku tatu zilizopita, misaada imeweza kufika kaskazini mwa Gaza baada ya muda wa wiki mbili ambapo Umoja wa Mataifa unasema hakuna hata moja iliyotolewa huko.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alikuwa mtia saini mwenza wa barua hiyo yenye maneno makali akiitaka Israel kuchukua hatua mahususi kushughulikia hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza.
Pentagon - kama Idara ya kitaifa - imekubali maboresho katika utoaji wa misaada wiki hii - lakini inaendelea kutilia mkazo ujumbe huo.
Msaada ulijadiliwa tena katika simu ya usiku kati ya Austin na waziri wa ulinzi wa Israel.
Hapo awali, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Washington inafuatilia kwa makini mpango wa Israel ili kuhakikisha kwamba hatua zake haziendani na kile alichokiita "sera ya kuwaangamiza watu kwa njaa."
Israel inakanusha kwamba imekuwa ikizuia chakula kupelekwa kaskazini mwa Gaza ambako ilianza mashambulizi mapya ya ardhini wiki mbili zilizopita kukabiliana na kile inachosema ni kuchibuka tena kwa wapiganaji wa Hamas.
Jabalia, kaskazini, imekuwa ikizingirwa na wanajeshi wa Israeli huku wakazi wakisema wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
HRW: Tanzania izingatie haki za binadamu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa,
Shirika la kimatatifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch
limeitaka serikali ya Tanzania kulinda haki za binadamu kuelekea uchaguzi wa
serikali za mitaa.
Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi wa serikali za mtaa tarehe 27
Novemba huku wapiga kura wakitarajiwa kuchagua Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi
mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi
la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka za Wilaya.
Nafasi zingine zinazotarajiwa
kugombaniwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo,
Mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi Mchanganyiko la Wanaume
na Wanawake) na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za
Miji.
Hata hivyo, Human Rights
Watch wanasema ndani ya miezi michache iliyopita kumekuwepo na matukio mengi ya
uvunjifu wa haki za binaadamu nchini Tanzania hali inayotia hofu kuelekea
uchaguzi huo.
“Tangu mwezi Juni, mamlaka
zimewakamata kiholela mamia ya wafuasi wa upinzani, zimedhibiti upatikanaji wa
mitandao ya kijamii, zimefungia vyombo huru vya habari, na zimehusishwa na
kutekwa na mauaji ya wapinzani wa serikali wasiopungua wanane” imesema sehemu
ya ripoti ya Human Rights Watch.
Hatahivyo akizungumza, waziri wa
sheria na katiba nchini humo Palamagamba Kabudi amesema madai hayo yamejazwa chumvi na kwamba hayaendani na hali halisi
nchini Tanzania.
Bwana Kabudi ameitetea serikali ya Tanzania akisema kwamba imekuwa kifua
mbele kulinda haki za kibinadamu na
kwamba uchaguzi wa mitaa utakaofanyika mwezi ujao utakuwa huru na wa haki.
Katika ripoti hiyo, Human
Rights Watch imetaja tukio la kutekwa kwa Edgar Mwakabela, anayejulikana kwa
jina la Sativa. Imezungumzia pia tukio la Kombo Mbwana, mwanachama wa chama cha
upinzani cha Chadema aliyepotea kwa takribani siku 30 na baadae polisi mkoani
Tanga kujitokeza na kuthibitisha kumshikilia.
Human Rights Watch wametaja pia kupotea kwa Dioniz Kipanya, mwanachama wa Chadema wilayani Sumbawanga, mkoa wa Rukwa pamoja na tukio la kupotezwa kwa Deusdedith Soka anayedaiwa kutekwa mnamo tarehe 18 Agosti pamoja na msaidizi wake Jacob Godwin Mlay na dereva bodaboda Frank Mbise.
Kupotea kwa Shadrack Chaula, ambaye hajaonekana tangu tarehe 2 Agosti, mwezi mmoja baada ya kushitakiwa kwa kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan, kumetajwa pia katika ripoti hiyo. Tukio la kuuwawa kwa Ali Mohamed Kibao tarehe 7 Septemba limetajwa pia katika ripoti hiyo.
Matukio mengine yalliyoorodheshwa katika ripoti hiyo ni yale ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kufungia kampuni ya habari ya Mwananchi kuchapisha maudhui katika mitandao baada ya kuchapisha kibonzo kilichomuonyesha muhusika aliyefanana na Rais Samia akitazama habari mbalimbali zilizohusu matukio ya utekaji.
Akijibu kuhusu kukamatwa kiholela kwa wafuasi wa upinzani na mauaji
ya wakosoaji wa serikali, Kabudi amesema, taarifa hizo hazina msingi na kwamba
zinalenga kuchafua jina zuri la Tanzania kimataifa.
BBC inaendelea na jitihada za kupata maoni ya serikali kutoka kwa msemaji wa serikali
Wanne mbaroni Tanzania kwa kumuua mume wa mdaiwa mkopo,
Chanzo cha picha, BBC/Lasteck
Jeshi la polisi nchini
Tanzania linawashikilia wafanyakazi wanne wa kampuni ya kutoa ya mikopo ya
kifedha ya OYA kwa tuhuma za mauaji ya Juma Mfaume kwa kumshambulia sehemu
mbalimbali za mwili mume wa mdaiwa wa mkopo.
Taarifa ya Kaimu Kamanda
wa Polisi mkoa wa Pwani, Muhudhwari Msuya inasema tukio hilo limetokea Jumatatu
katika wilaya ya kipolisi Mlandizi ambapo wafanyakazi hao walifika nyumbani
hapo kwa lengo la kudai fedha za marejesho ya mkopo kwa mke wa Mfaume.
Kwa mujibu wa polisi,
baada ya kufika nyumbani kwa Mfaume aliwaelekeza kuwa mkewe hakuwepo lakini
watuhumiwa hao walilazimisha kuingia ndani kwa nguvu huku wakimshambulia kwa
kumchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea kuanguka chini
na kupoteza fahamu.
Kamanda Msuya alisema
kutokana na hali hiyo watuhumiwa walimbeba Mfaume kwenye gari lao kwaajili ya
kumpeleka hospitali lakini alifariki akiwa anapewa matibabu.
Alisema, "Mwili wa
marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari kisha kukabidhiwa ndugu kwa taratibu
za mazishi.”
Hata hivyo, Jeshi la
Polisi linatoa wito kwa makampuni na taasisi za kifedha kufuata taratibu za
kisheria katika kudai fedha kutoka kwa wateja wao ili kuepusha usumbufu na
madhara yanayoweza kutoka ikiwemo uharibifu wa Mali, kujeruhi na vifo.
Kwa upande wake,
Mkurugenzi wa Kampuni ya OYA ya nchini Tanzania, Alpha Peter ameiambia BBC kuwa
waliodaiwa kusababisha kifo ni watumishi wa taasisi yao na kwamba kitendo hicho
hakikuwa maelekezo ya kampuni hiyo.
Peter alisema,
“Kilichofanyika, si maelekezo wala utaratibu wa taasisi yetu pale tunapoenda
kudai marejesho kwa wateja wetu. Kwasasa tuko karibu na familia kuifariji
lakini pia tunaendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi wakati huu
wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.”
Kampuni ya OYA ya nchini
Tanzania ilisajiliwa mwaka 2020 na kwasasa inatoa huduma kwenye mikoa nane.
Jeshi la Rwanda lakanusha madai ya kuwabaka wanawake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
Chanzo cha picha, MINUSCA
Maelezo ya picha, Picha ya jeshi la Rwanda katika ujumbe wa MINUSCA akiwa pamoja na muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Valentine Rugwabiza (mbele ya askari)
Jeshi la Rwanda limekanusha madai ya ubakaji dhidi
ya wanajeshi wake wanaohudumu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), likisema kuwa
wanajeshi wa Rwanda katika ujumbe huo ni "wastaarabu" na
"wanalinda na kuheshimu watu wanaokutana nao".
Gazeti la New Humanitarian liliripoti Jumatano
jinsi wanawake na wasichana katika Jamhuri ya Afrika ya Kati "wanavyoendelea
kutishiwa" na unyanyasaji wa kijinsia na vikosi vya kulinda amani vya
Umoja wa Mataifa, na wengi wanakaa kimya "kwa hofu ya kulipiziwa
kisasi".
Takriban wanawake wanne wanawatuhumu wanajeshi sita
wa Rwanda, wawili kati yao wakiwa nchini humo chini ya makubaliano ya ushirikiano
wa pande mbili, na wengine katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaojulikana kama
MINUSCA.
Jeshi la Rwanda
linasema kwamba vituo vya jeshi la Rwanda katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
haviruhusu kuingia kwa raia ambao hawakuja kwa njia inayojulikana, "ili
kusiwe na unyanyasaji wa raia katika kituo hicho".
Miongoni mwa
wanaotuhumiwa kwa vitendo hivyo ni pamoja na vikosi vya Rwanda, Burundi na
Zambia ambavyo ni sehemu ya ujumbe unaojulikana kwa jina la MINUSCA pamoja na
wapiganaji wa zamani wa Kundi la Wagner ambao ni sehemu ya makubaliano ya
ushirikiano wa nchi hizo. New Humanitarian anasema.
Vikosi vya kijeshi vya
nchi zote zilizotajwa hazijatoa maoni yoyote juu ya mashtaka dhidi ya askari
wao.
Rwanda
ina jeshi la ngazi mbili katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, lile lililo katika
ujumbe wa MINUSCA na lile lililo katika makubaliano ya usaidizi yaliyotiwa
saini kati ya Kigali na Bangui mwishoni mwa 2019, ambayo yaliwezesha jeshi la Rwanda
kutetea utawala wa Rais Faustin- Archange Touadéra ambayo ilirejeshwa na waasi
wakiongozwa na rais wa zamani François Bozizé.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa
tangu mwaka 2015 kumekuwa na zaidi ya visa 730 vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanajeshi wa
Umoja wa Mataifa huko Afrika ya Kati.
Habari za hivi punde, Marekani yashambulia hifadhi za silaha za Wahouthi zilizofichwa chini ya ardhi
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ndege za Marekani
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, amethibitisha kuwa vikosi vya jeshi la taifa hilo zikiwemo ndege aina ya B-2 vimeshambulia hifadhi za silaha za chini ya ardhi za wapiganaji wa Kihouthi nchini Yemen.
Bw Austin amesema operesheni hiyo ilihusisha ulipuaji wa "usahihi" wa hifadhi tano "zilizoimarishwa" chini ya ardhi, zenye lengo la kupunguza uwezo wa kundi hilo kushambulia meli katika eneo hilo.
Amesema hifadhi hizo zina aina mbalimbali za silaha ambazo Wahouthi hutumia kulenga meli za raia na za kijeshi katika eneo lote.
"Hii ilikuwa hatua ya kipekee kuhusu uwezo wa Marekani kulenga vifaa ambavyo wapinzani wetu wanajaribu kuficha, bila kujali kina chake cha chini ya ardhi ," aliandika katika taarifa yake.
Rigathi Gachagua:Je, ni kesi gani haswa inayomuandama naibu rais katika seneti?
Bunge la Seneti nchini Kenya linatazamiwa kupiga kura Alhamisi iwapo litamuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua mamlakani katika sakata ya kisiasa ya aina yake ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini Kenya.
Haya ndiyo tunayofahamu kuhusu mashtaka dhidi ya Naibu Rais:
Kulingana na mbunge wa Kibwezi Magharibi, aliyewasilisha hoja ya kumuondoa madarakani Mutuse Mwengi, anakabiliwa na tuhuma kumi na moja.
Gachagua analaumiwa kwa kukinzana na sera za serikali na kukosa kutekeleza majukumu yake kama Naibu Rais, hivyo basi kukiuka kanuni ya uwajibikaji wa pamoja wa Baraza la Mawaziri.
Hoja hiyo ya Mutuse Mwengi pia inadai kuwa Gachagua aliingilia shughuli za ugatuzi wa kaunti, kuhujumu ugatuzi na kutishia idara ya mahakama, hatua inayokiuka kanuni ya uhuru wa idara ya mahakama.
Vilevile hoja hiyo inataja utovu wa nidhamu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi, kutomtii Rais, kuwaonea maafisa wa umma, na kushawishi vitendo vya rushwa.
Mbunge huyo wa Kibwezi Magharibi anasema kwamba Bw Gachagua alishindwa kuheshimu na kutetea Katiba, huku matamshi yake ya uchochezi yakidaiwa kukiuka Sheria ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa kwa kuendeleza chuki za kikabila.
Aidha Gachagua anadaiwa alijihusisha na ufisadi, ufujaji wa pesa na matumizi mabaya ya ofisi, kukiuka sheria za kupambana na ufisadi , kutoa taarifa za uongo na uovu na kukiuka kanuni za adhabu na sheria ya uongozi na uadilifu.
Tayari bunge la taifa limekwishaidhinisha kwa wingi wa kura ya kumuondoa mamlakani na sasa ni zamu ya bunge la seneti kuamua baadaye leo kwa kura iwapo Rigadhi Gachagua ataendelea kuwa Naibu wa Rais William Ruto au la.
Marekani kutenga dola milioni 425 za msaada wa kijeshi kwa Kyiv, huku Australia ikipeleka vifaru 49 vya Abrams
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Mizinga ya Marekani US M1 Abrams ina kasi zaidi kuliko mizinga mingi iliyotengenezwa na Urusi
Rais wa Marekani Joe Biden alizungumza kwa simu na Rais wa Ukraine
Volodymyr Zelensky siku ya Jumatano na kutangaza kifurushi kipya cha msaada wa
kijeshi cha dola milioni 425.
Kulingana na huduma ya vyombo vya habari vya White House,
kifurushi hicho kitajumuisha, mifumo ya ulinzi wa anga, na magari ya kivita.
Wakati huo huo Australia itapeleka mizinga 49 ya Abrams ya mtindo wa zamani wa M1A1 nchini
Ukraine, ripoti ya vyombo vya habari vya Australia ikimnukuu waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Pat Conroy.
Kwa mujibu wa shirka la utangazaji la Australia, wiki chache zilizopita Australia ilipokea kundi la kwanza la mizinga ya mtindo
mpya wa M1A2.
Gharama
ya jumla ya mizinga ambayo Ukraine itapokea inathamani ya dola Australia milioni 245 za Australia (sawa na dola
za Marekani milioni 163.5).
Australia
imeagiza mizinga 120 ya Abrams M1A2, gazeti la The Age limeandika.
Jeshi la Australia litahifadhi idadi fulani
ya vifaru vya zamani kwa sasa hadi magari mapya yatakapowasili.
Uongozi wa Ukraine uliomba
mizinga iliyotengenezwa na nchi za Magharibi katika majira ya baridi ya
2022-23, wakati ilionekana kuwa muhimu kwa ajili ya mashambulizi ya kukabiliana
na mashambulizi ya Urusi.
Biden alizungumza na Zelensky na kutangaza kifurushi kipya cha msaada cha $
425 milioni.