Je! Wanajeshi wa Korea Kaskazini wanajiunga na vita vya Urusi huko Ukraine?

.

Chanzo cha picha, ED JONES/AFP

Maelezo ya picha, Urusi inakanusha kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wanajiandaa kwa mapigano nchini Ukraine (picha ya faili)
Muda wa kusoma: Dakika 3

Jeshi la Urusi linaunda kikosi cha takriban wanajeshi 3,000 wa Korea Kaskazini, chanzo cha kijasusi cha kijeshi cha Ukraine kimeiambia BBC, katika ripoti ya hivi punde inayodokeza kwamba Pyongyang inaunda muungano wa karibu wa kijeshi na Urusi.

Hadi sasa BBC bado haijaona dalili yoyote ya kitengo hicho kikubwa kuundwa katika Mashariki ya mbali ya Urusi, na msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amepuuzilia mbali ripoti za kuhusika kwa Korea Kaskazini.

"Hii sio ujasusi wa Uingereza pekee, pia ni ujasusi wa Marekani. Wanaripoti kila wakati, hawatoi ushahidi wowote," alisema.

Hakuna shaka Moscow na Pyongyang zimeongeza kiwango chao cha ushirikiano katika miezi ya hivi karibuni. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alimtumia Vladimir Putin ujumbe wa siku ya kuzaliwa wiki iliyopita tu akimwita "rafiki wake wa karibu".

Volodymyr Zelensky wa Ukraine amezungumza kuhusu Korea Kaskazini kujiunga na vita, na waziri wa ulinzi wa Korea Kusini alisema mwezi huu kwamba fursa ya kutumwa kwa Korea Kaskazini nchini Ukraine ni "uwezekano mkubwa".

Swali kuu ni kuhusu idadi inayohusishwa

Chanzo cha kijeshi katika Mashariki ya mbali nchini Urusi kiliithibitishia BBC Urusi kwamba "idadi ya kubwa ya Wakorea Kaskazini wamewasili" na waliwekwa katika kambi moja ya kijeshi karibu na Ussuriysk, kaskazini mwa Vladivostok. Lakini chanzo kilikataa kutoa idadi sahihi, isipokuwa "hawakufikia 3,000".

Wataalamu wa kijeshi wametuambia wana shaka kuwa vitengo vya jeshi la Urusi vinaweza kujumuisha wanajeshi wa Korea Kaskazini kwa idadi kubwa.

"Haikuwa rahisi hata kidogo kujumuisha mamia ya wafungwa wa Urusi mwanzoni - na watu hao wote walizungumza Kirusi," mchambuzi mmoja - ambaye yuko Urusi ambaye hakutaka kutajwa jina - aliiambia BBC.

Hata kama wangefikia 3,000, haingekuwa idadi kubwa katika uwanja wa vita, lakini Marekani ina wasiwasi kama Ukraine.

"Itaashiria ongezeko kubwa la uhusiano wao," msemaji wa idara ya serikali ya Marekani Matthew Miller, ambaye aliona kama "kiwango kipya cha kukata tamaa cha Urusi" huku ikipata k hasara kubwa kwenye uwanja wa vita.

.

Chanzo cha picha, VLADIMIR SMIRNOV/POOL/AFP

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ilikuwa nyuma mwezi wa Juni ambapo Vladimir Putin aliingia katika mkataba wa "amani na ulinzi" na Kim Jong Un.

Na kuna ushahidi unaoongezeka kwamba Korea Kaskazini inaipatia Urusi silaha, kama ilivyoonyeshwa hivi karibuni na kupatikana kwa kombora la Korea Kaskazini katika mkoa wa Poltava wa Ukraine.

Kwa hakika, ripoti za mabomu na makombora zilizotolewa na Pyongyang ni za Desemba 2023 katika mazungumzo ya Telegram yanayohusisha jumuiya za kijeshi za Urusi.

Wanajeshi wa Urusi walioko nchini Ukraine, mara nyingi wamelalamika kuhusu kiwango cha silaha na kwamba makumi ya wanajeshi wamejeruhiwa.

Kyiv inashuku kuwa kikosi cha wanajeshi wa Korea Kaskazini kinajiandaa katika eneo la Ulan-Ude karibu na mpaka wa Mongolia kabla ya kupelekwa katika jimbo la Kursk la Urusi, ambako vikosi vya Ukraine vilianzisha uvamizi mwezi Agosti.

"Wanaweza kulinda baadhi ya sehemu za mpaka wa Urusi na Ukraine,hatua ambayo itawaacha huru wanajeshi wa Urusi kwa mapigano mahali pengine," alisema Valeriy Ryabykh, mhariri wa gazeti la Ukraine la Defense Express.

"Sidhani kwamba vitengo hivi vitaonekana mara moja kwenye mstari wa mbele."

Ryabakh hayuko pekee katika wazo hili.

Korea Kaskazini inaweza kuwa na takriban wanajeshi milioni 1.28 lakini jeshi lake halina uzoefu wa hivi karibuni wa operesheni za mapigano, tofauti na jeshi la Urusi.

Pyongyang imefuata mtindo wa zamani wa Kisovieti katika vikosi vyake vya kijeshi lakini haijulikani ni jinsi gani kikosi chake kikuu cha askari wa miguu wenye magari kinaweza kuingia katika vita vya Ukraine.

Kisha kuna kizuizi cha lugha cha wazi na kutokujulikana na mifumo ya Kirusi ambayo inaweza kutatiza majukumu yoyote ya mapigano.

Hiyo haizuii jeshi la Korea Kaskazini kushiriki katika vita kamili vya Urusi nchini Ukraine, lakini wanatambuliwa zaidi na wataalam kwa uwezo wao wa uhandisi na ujenzi, sio kwa mapigano.

Wanachofanya wote wawili ni motisha za pamoja.

Pyongyang inahitaji pesa na teknolojia, Moscow inahitaji wanajeshi na silaha.

"Pyongyang ingelipwa vizuri na labda kupata ufikiaji wa teknolojia ya kijeshi ya Urusi, ambayo vinginevyo Moscow ingesita kuhamishia Korea Kaskazini," anasema Andrei Lankov, mkurugenzi wa Kundi lililopo katika Hatari la Korea.

"Pia ingewapa wanajeshi wao uzoefu halisi wa mapigano, lakini pia kuna hatari ya kuwaonyesha maisha mazuri raia wa Wakorea Kaskazini katika nchi za Magharibi, ambayo ni sehemu yenye mafanikio zaidi."

Kwa Putin, kuna hitaji la dharura la kufidia hasara kubwa wakati wa zaidi ya miaka miwili na nusu ya vita.

Valeriy Akimenko kutoka Kituo cha Utafiti wa Mafunzo ya Migogoro cha Uingereza anaamini kupeleka Wakorea Kaskazini kungemsaidia kiongozi huyo wa Urusi kukabiliana na duru ya awali ya uhamasishaji wa lazima uliogonga mwamba .

"Kwa hivyo anafikiria, wakati idadi ya wanajeshi wa Urusi inapunguzwa na Ukraine, ni wazo zuri -kwa nini tusiwaruhusu Wakorea Kaskazini waingie katika vita?"