Mkurugenzi wa Idara ya Secret Service Marekani ajiuzulu

Cheatle alikuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka kwa viongozi wa vyama viwili vikubwa nchini humo ajiuzulu baada ya mtu mwenye bunduki, mwenye umri wa miaka 20 kumjeruhi Trump

Muhtasari

  • Papa wagunduliwa kuwa na viwango vya juu vya kokeini
  • Rais William Ruto afanya tena mabadiliko katika Baraza lake jipya la Mawaziri
  • De Bruyne 'haondoki' Man City – Guardiola
  • Mlinzi wa kiongozi wa zamani wa S Leone afungwa jela kwa jaribio la mapinduzi
  • Waandamanaji waliokuwa wakielekea majengo ya bunge wakamatwa Uganda
  • China kuunganisha makundi ya Palestina kuafikia maridhiano
  • Maporomoko ya ardhi Ethiopia yaua 157 - maafisa
  • Ukraine yashambulia feri na kuua mtu mmoja mmoja katika bandari ya Urusi
  • Wakenya wapokea chanjo ya kwanza ya kifua kikuu katika kipindi cha miaka 100
  • Maandamano Kenya: Polisi waonya dhidi ya maandamano
  • Jeshi la Urusi lasema kuwa ndege zisizo na rubani 25 za Ukraine zimedunguliwa
  • Maandamano Uganda: Usalama waimarishwa huku vijana wakijiandaa kuandamana hadi bungeni kuwasilisha madai yao
  • Bunge kuwakagua mawaziri wateule walioteuliwa na Rais Ruto
  • Israel inajiandaa kuanzisha "operesheni kubwa" Khan Yunis, huku mateka wengine wawili wakiuawa katika Ukanda wa Gaza
  • Israel inajiandaa kuanzisha "operesheni kubwa" Khan Yunis, huku mateka wengine wawili wakiuawa katika Ukanda wa Gaza
  • Harris ana uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wajumbe kuwa mteule wa Democrat
  • Netanyahu akabiliwa na wakati mgumu baada ya Biden kujiondoa

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi & Seif Abdalla

  1. Mkurugenzi wa Idara ya Secret Service Marekani ajiuzulu

    th

    Chanzo cha picha, Tom Williams/CQ-Roll Call, Inc kupitia Getty Images

    Mkurugenzi wa idara ya ulinzi wa viongozi (Secret Service), Kimberly Cheatle, amejiuzulu, siku moja baada ya kukiri kuwa idara hiyo ilishindwa katika dhamira yake ya kuzuia jaribio la mauaji dhidi ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

    Cheatle alikuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka kwa viongozi wa vyama viwili vikubwa nchini humo ajiuzulu baada ya mtu mwenye bunduki, mwenye umri wa miaka 20 kumjeruhi Trump mgombea wa sasa wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican katika mkutano wa kampeni wa Julai 13 mjini Butler, Pennsylvania.

    Cheatle alifika mbele ya kamati ya bunge siku ya Jumatatu na kusema kuwa shambulizi dhidi ya Trump, ambaye alijeruhiwa kidogo kwenye sikio lake la kulia, lilikuwa kushindwa kwa idara hiyo ya Secret Service.

    Warepublican na Wademokrat walimtaka Cheatle ajiuzulu. Aliwakasirisha wabunge kutoka pande zote mbili kwa kukataa kutoa maelezo mahsusi kuhusu shambulio hilo, akitoa sababu ya kuwepo kwa uchunguzi unaoendelea.

    Mshambuliaji huyo alimfyatulia risasi Trump kwa bunduki aina ya AR dakika chache baada ya kuanza kuwahutubia waliohudhuria hafla hiyo ya kampeni.

    Akiwa juu ya paa la jengo lililo karibu, aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa Secret Service chini ya sekunde 30 baada ya kufyatua risasi ya kwanza, kati ya nane zilizotumika.

    Wabunge walimhoji Bi Cheatle kuhusu maandalizi ya usalama kabla ya mkutano wa kampeni wakati wa kikao cha saa sita cha Kamati ya Uangalizi ya Bunge.

    Bi Cheatle alichukua jukumu la kudorora kwa usalama, lakini alionekana kukataa kabisauwezekano wake kujiuzulu.

    Mashahidi waliripoti kumwona mshukiwa Thomas Matthew Crooks - akiwa na bunduki juu ya paa kwenye mkutano huo dakika chache kabla ya risasi kufyatuliwa.

    Maafisa wa usalama na watekelezaji sheria kutoka kwa vyombo mbalimbali walikuwepo kwenye mkutano huo.

    Wakati wa ushuhuda wake, Bi Cheatle hakuwapa wabunge habari yoyote mpya kuhusu jinsi Crooks alivyoweza kufikia paa ambapo alikuwa amelala na kwa nini Trump aliruhusiwa kupanda jukwaani.

    Unaweza pia kusoma

  2. Papa wagunduliwa kuwa na viwango vya juu vya kokeini

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wanabiolojia wa baharini waliwafanyia majaribio papa 13 wa Brazil waliochukuliwa kutoka ufuo ulio karibu na Rio de Janeiro na wakagundua walikuwa na viwango vya juu vya kokeini kwenye misuli na maini yao.

    Viwango hivyo vilikuwa mara 100 zaidi ya vilivyoripotiwa hapo awali kwa viumbe wengine wa majini.

    Utafiti huo, uliofanywa na Wakfu wa Oswaldo Cruz, ni wa kwanza kugundua uwepo wa kokeini kwenye papa.

    Wataalamu wanaamini kuwa kokeini inaingia majini kupitia maabara inayoendesha shughuli zake kwa njia haramu ambapo dawa hiyo inatengenezwa au kupitia kinyesi cha watumiaji wa dawa za kulevya.

    Pakiti za kokeini zilizopotea au kutupwa na wasafirishaji haramu baharini pia zinaweza kuwa chanzo, ingawa hii ina uwezekano mdogo, watafiti wanasema.

    Sara Novais, mtaalam wa sumu ya mazingira ya baharini katika Kituo cha Sayansi ya Bahari na Mazingira cha Chuo Kikuu cha Polytechnic cha Leiria, aliliambia jarida la Sayansi kwamba ugunduzi huo ni "muhimu sana na wenye uwezo wa kusababisha wasiwasi".

    Papa wote walikuwa wanawake na wajawazito, lakini athari ya kokeini kwa vijusi haijulikani, wataalam wanasema.

    Utafiti zaidi unahitajika ili kuhakikisha kama kokeini inabadilisha tabia ya papa.

    Hata hivyo, utafiti wa hapo awali umeonyesha kuwa dawa zinaweza kuwa na athari sawa kwa wanyama kama zinavyofanya kwa binadamu.

  3. Rais William Ruto awabadilishia wizara mawaziri wawili aliowateua maajuzi

    .

    Chanzo cha picha, IKULU YA RAIS

    Rais William Ruto nchini Kenya amefanya tena mabadiliko katika baraza la mawaziri.

    Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Aden Duale amepelekwa katika wizara ya mazingira huku Waziri aliyekuwa ametuliwa kushika nafasi hiyo, Soipan Tuya akipewa Wizara ya Ulinzi.

    Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, mheshimiwa Aden Duale alisema, ‘’Ninamshukuru Rais @WilliamsRuto kwa kunitoa kutoka Wizara ya Ulinzi hadi Wizara ya Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu’’.

    Alionyesha kujitolea kwake katika majumu yake mapya, na kusisitiza kuwa atahakikisha angalizo linawekwa katika usimamizi endelevu wa mazingira, kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kukuza juhudi za upandaji miti na uhifadhi.

    Rais William Ruto alitangaza mawaziri kumi na moja katika baraza lake la mawaziri.

    Katika hotuba yake kwa taifa, rais Ruto alisema kwamba idadi ya mawaziri waliosalia itatangazwa baada ya mashauriano.

    Hayo yalijiri baada ya shinikizo kuongezeka kwa Rais kuchagua watu wenye uwezo ambao watamsaidia kutekeleza ajenda yake.

    Soma zaidi:

  4. De Bruyne 'haondoki' Man City – Guardiola

    Kevin de Bruyne na Pep Guardiola

    Chanzo cha picha, Getty

    Maelezo ya picha, Kevin de Bruyne na Pep Guardiola wameshindia Manchester City mataji 17

    Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kiungo mwenye ushawishi mkubwa Kevin de Bruyne atasalia katika klabu hiyo.

    De Bruyne amekuwa akihusishwa na tetesi za kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Saudia majira ya kiangazi.

    Amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na The Blues na alisema mwezi uliopita atatathmini ofa kutoka kwa Ligi Kuu ya Saudia kwa sababu ya "fedha za ajabu" zilizopo.

    Hata hivyo, Guardiola hana hofu ya kumpoteza De Bruyne.

    "Kevin haondoki," aliwaambia wanahabari kabla ya mechi ya ufunguzi ya timu yake ya kabla ya msimu mpya dhidi ya Celtic huko Chapel Hill, North Carolina, Jumatano

    De Bruyne aliisaidia City kunyakua taji la Ligi Kuu msimu uliopita, likiwa ni la nne mfululizo katika klabu hiyo na la sita kwa jumla katika klabu hiyo.

    Soma pia:

  5. Mlinzi wa kiongozi wa zamani wa S Leone afungwa jela kwa jaribio la mapinduzi

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Aliyekuwa mlinzi wa aliyekuwa Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amepatikana na hatia ya uhaini na kuhukumiwa pamoja na watu wengine 10 kwa kosa la jaribio la mapinduzi mwaka jana.

    Amadu Koita Makalo ambaye pia ni mwanajeshi wa zamani alihukumiwa kifungo cha miaka 182 jela kwa makosa ya uhaini, mauaji na mashambulizi ya risasi kwa nia ya kuua.

    Mashtaka hayo yalifuatia mashambulizi ya watu wenye silaha kwenye kambi ya kijeshi na magereza mwezi Novemba mwaka jana.

    Hilo lilitokea miezi kadhaa baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata ambao ulishuhudia Rais Julius Maada Bio akichaguliwa tena kwa muhula wa pili.

    Zaidi ya wafungwa 2,000 waliachiliwa na takriban watu 20 kuuawa kabla ya serikali kurejesha udhibiti, na kutaja shambulio hilo kuwa jaribio la kupindua serikali.

    Makalo ambaye alifuatiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii ambapo aliikosoa serikali, alishutumiwa kuwa miongoni mwa waandaaji wa njama hiyo ya mapinduzi.

    Wakati wa hukumu yake siku ya Jumatatu, jaji alisema kwamba mlinzi huyo wa zamani wa rais hakuonyesha majuto wakati wote wa kesi hiyo, gazeti la ndani la Awoko liliripoti.

    "Madhumuni ya hukumu hii ni onyo kwa watu kwamba mapinduzi au jaribio la kupindua serikali yoyote halali halikubaliwi tena," Komba Kamanda alinukuliwa akisema.

    Iliripoti kwamba washtakiwa wenzake Makalo walihukumiwa kati ya miaka 39 na 182 jela.

    Soma zaidi:

  6. Waandamanaji waliokuwa wakielekea majengo ya bunge wakamatwa Uganda

    .

    Chanzo cha picha, Bobi Wine/X

    Makumi wa raia wa Uganda wanasemekana kukamatwa na polisi wakati wa makabiliano kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji wenye nia ya kuandamana hadi majengo ya Bunge kama ishara ya kupinga ufisadi, kulingana na gazeti la Daily Monitor.

    Vijana ambao wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa ajira na kupanda kwa gharama ya maisha, walibeba mabango wakitaka spika wa bunge ajuzulu.

    Kulingana na Daily Monitor, wakili anayetetea haki za kibinadamu Eriah Nuwenuwe, ni miongoni mwa waliokamatwa katika maeneo ya bunge.

    Tangu siku ya Jumatatu, kumeshuhudiwa ulinzi mkali katika maeneo ya majengo ya bunge na maafisa walijitokeza mitaani kukabili waandamanaji.

    Hapo jana, kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine alisema vikosi vya usalama katika mji mkuu Kampala vilikuwa vimezingira makao makuu ya chama chake katika mkesha wa maandamano hayo.

    Polisi walisema walikuwa wamechukua "hatua za tahadhari" kuzuia "uhamasishaji wa maandamano".

    Aidha, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alionya Jumamosi kwamba waandamanaji wa maandamano yaliyopangwa kwenda bungeni "wanacheza na moto".

  7. China kuunganisha makundi ya Palestina kufikia maridhiano

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Pande hasimu za Palestina Hamas na Fatah zimetia saini tamko la kukubali kuunda "serikali ya muda ya maridhiano ya kitaifa" huko Ukingo wa Magharibi na Gaza inayokaliwa kwa mabavu baada ya vita na Israel, katika mkutano uliosimamiwa na China, waziri wa mambo ya nje wa China na maafisa wa Hamas wamesema.

    Wawakilishi kutoka makundi yote na makundi mengine 12 ya Wapalestina waliahidi kufanya kazi kwa ushirikiano baada ya siku tatu za mazungumzo mjini Beijing.

    Ni makubaliano ya hivi punde kati ya mikataba kadhaa ya maridhiano ambayo Hamas na Fatah wamekubaliana katika uhusiano wao wa muda mrefu uliovunjika, ambao hakuna hata mmoja wao umehitimisha mgawanyiko wao.

    Israel pia imeondoa jukumu la Hamas au Fatah katika kutawala Gaza baada ya kutulia kwa vita eneo hilo.

    Mgawanyiko mkubwa ulianza mwaka 2007 wakati Hamas ikiwa mtawala pekee huko Gaza baada ya kuwaondoa kwa nguvu Fatah kutoka eneo hilo.

    Hayo yalijiri baada ya Rais wa Palestina na kiongozi wa Fatah Mahmoud Abbas kuvunja serikali ya umoja iliyoongozwa na Hamas iliyoundwa wakati Hamas iliposhinda uchaguzi wa kitaifa mwaka mmoja kabla.

    Tangu wakati huo, Mamlaka ya Palestina inayotawaliwa na Fatah imeachiwa kutawala sehemu tu za Ukingo wa Magharibi.

    Hamas imepoteza udhibiti katika eneo la Gaza tangu vita na Israel kuanza tarehe 7 Oktoba na mashambulizi ya kipekee ya Hamas dhidi ya Israel, yalioua takriban watu 1,200 na wengine 251 wakarudishwa Gaza kama mateka.

    Zaidi ya Wapalestina 39,000 wameuawa huko Gaza kutokana na mashambulizi ya Israel, kwa mujibu wa wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.

    Soma zaidi:

  8. Maporomoko ya ardhi Ethiopia yaua 157 - maafisa

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Idadi ya watu waliouawa katika maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia imeongezeka na kufikia takriban 157, maafisa wa eneo hilo wamesema.

    Matukio mawili yanakisiwa kutokea Jumapili jioni na Jumatatu asubuhi, baada ya mvua kubwa kunyesha katika eneo la mbali la milima la ukanda wa Gofa.

    Mamlaka ya eneo hilo ilisema kuwa utafutaji wa manusura ulikuwa "unaendelea" lakini "idadi ya vifo bado inaweza kuongezeka".

    Picha zilionyesha mamia ya watu wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la tukio na wengine wakichimba chini ya vifusi kutafuta watu walionasa.

    Kwa nyuma, sehemu ya kilima inaweza kuonekana ikiwa imeporomoka kiasi na sehemu kubwa ya ardhi yenye udongo mwekundu.

    Meskir Mitku, msimamizi mkuu wa eneo la Gofa, alisema wanawake, watoto na maafisa wa polisi walikuwa miongoni mwa waliopoteza maisha.

    "Kulikuwa na mvua kubwa jana [Jumapili] usiku na baadhi ya watu walifariki kutokana na maporomoko ya ardhi," msemaji wa serikali wa wilaya ya Gofa Kassahun Abayneh alisema.

    Gofa ni sehemu ya jimbo linalojulikana kama Kusini mwa Ethiopia, lililoko karibu kilomita 320 (maili 199) kusini-magharibi mwa mji mkuu, Addis Ababa.

    Taarifa ya idara ya mawasiliano ya eneo la Gofa ilisema kuwa idadi ya waliofariki imepita 146, na inaweza kuongezeka zaidi, AFP inaripoti.

    Kusini mwa Ethiopia ni miongoni mwa maeneo ya nchi hiyo ambayo yamekumbwa na mvua kubwa na mafuriko katika miezi ya hivi karibuni, kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (Ocha).

    Lakini matukio ya maporomoko ya ardhi na mafuriko yamekuwa yakitokea siku za nyuma. Mnamo mwezi Mei 2016, takriban watu 50 waliuawa katika mafuriko na maporomoko ya ardhi kufuatia mvua kubwa kusini mwa nchi.

    Idadi ya watu waliouawa katika maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia imeongezeka na kufikia takriban 146, maafisa wa eneo hilo wamesema.

    Matukio mawili yanakisiwa kutokea Jumapili jioni na Jumatatu asubuhi, baada ya mvua kubwa kunyesha katika eneo la mbali la milima la ukanda wa Gofa.

    Mamlaka ya eneo hilo ilisema kuwa utafutaji wa manusura ulikuwa "unaendelea" lakini "idadi ya vifo bado inaweza kuongezeka".

    Picha zilionyesha mamia ya watu wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la tukio na wengine wakichimba chini ya vifusi kutafuta watu walionasa.

    Kwa nyuma, sehemu ya kilima inaweza kuonekana ikiwa imeporomoka kiasi na sehemu kubwa ya ardhi yenye udongo mwekundu.

    Meskir Mitku, msimamizi mkuu wa eneo la Gofa, alisema wanawake, watoto na maafisa wa polisi walikuwa miongoni mwa waliopoteza maisha.

    "Kulikuwa na mvua kubwa jana [Jumapili] usiku na baadhi ya watu walifariki kutokana na maporomoko ya ardhi," msemaji wa serikali wa wilaya ya Gofa Kassahun Abayneh alisema.

    Gofa ni sehemu ya jimbo linalojulikana kama Kusini mwa Ethiopia, lililoko karibu kilomita 320 (maili 199) kusini-magharibi mwa mji mkuu, Addis Ababa.

    Taarifa ya idara ya mawasiliano ya eneo la Gofa ilisema kuwa idadi ya waliofariki imepita 146, na inaweza kuongezeka zaidi, AFP inaripoti.

    Kusini mwa Ethiopia ni miongoni mwa maeneo ya nchi hiyo ambayo yamekumbwa na mvua kubwa na mafuriko katika miezi ya hivi karibuni, kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (Ocha).

    Lakini matukio ya maporomoko ya ardhi na mafuriko yamekuwa yakitokea siku za nyuma. Mnamo mwezi Mei 2016, takriban watu 50 waliuawa katika mafuriko na maporomoko ya ardhi kufuatia mvua kubwa kusini mwa nchi.

    Soma zaidi:

  9. Ukraine yashambulia feri na kuua mtu mmoja mmoja katika bandari ya Urusi

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mtu mmoja ameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani za Ukraine kwenye kivuko katika bandari ya kusini mwa Urusi, gavana wa eneo hilo amesema.

    Gavana wa Krasnodar Veniamin Kondratyev alisema feri hiyo ilishika moto katika bandari ya Kavkaz.

    Bandari hiyo iko kilomita chache kutoka daraja la Kerch, ambalo huwezesha usafiri wa barabara na reli kati ya Urusi na rasi ya Crimea, ambayo Urusi iliichukua kinyume cha sheria mwaka 2014.

    "Kwa bahati mbaya kuna waliojeruhiwa na kufariki dunia kati ya wafanyakazi feri na wa bandari," Bw Kondratyev alisema.

    Aliongeza kuwa huduma za dharura zilikuwa kwenye eneo la tukio.

    Ukraine ilishambulia eneo hilo hilo mwishoni mwa Mei, katika kituo cha mafuta karibu na bandari ya Kavkaz.

    Eneo karibu na daraja lililojengwa na Urusi juu ya Mlango-Bahari wa Kerch limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na vikosi vya Ukraine tangu uvamizi wa Urusi mnamo 2022.

    Meli za jeshi la wanamaji la Urusi zilizoko Crimea zimezama au kuharibiwa vibaya. Mapema mwezi huu mkuu wa jeshi la wanamaji la Ukraine alisema Meli ya Urusi katika Bahari Nyeusi imelazimika kuhamisha karibu meli zake zote za kivita kutoka eneo la Crimea linalokaliwa kwa mabavu hadi bandari nyingine.

    Katika tukio tofauti usiku kucha, vikosi vya ulinzi vya anga vya Ukraine vilidungua ndege saba zisizo na rubani aina ya Shahed na kombora la cruise lililorushwa na Urusi.

    Ndege moja isiyo na rubani ya Urusi ilishambulia kituo muhimu cha miundombinu katika Mkoa wa Sumy.

    Vikosi vya Urusi vilidungua ndege 25 zisizo na rubani za Ukraine magharibi mwa nchi na eneo la Crimea, wizara ya ulinzi ya Moscow ilisema.

    Soma zaidi:

  10. Wakenya wapokea chanjo ya kwanza ya kifua kikuu katika kipindi cha miaka 100

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kundi la kwanza la Wakenya limepokea chanjo inayoelekea kuwa ya kwanza ya kifua kikuu (TB) katika kipindi cha takriban miaka 100.

    Chanjo hiyo ilitolewa tarehe 12 Julai katika miji ya Kisumu, Kilifi, Machakos na Nairobi.

    Hata hivyo, chanjo bado inafanyiwa majaribio na huenda isipatikane kwa wingi kwa umma kabla ya mwaka 2030.

    Hivi sasa, chanjo pekee ya TB inayopatikana ni BCG kwa watoto waliotengenezwa mnamo 1921.

    BCG huwalinda watoto wachanga na watoto wadogo dhidi ya aina kali za kifua kikuu, lakini inatoa ulinzi duni kwa vijana na watu wazima dhidi ya aina ya ugonjwa wa mapafu, husababisha maambukizi ya bakteria wanaoeneza gonjwa wa kifua kikuu.

  11. Habari za hivi punde, Maandamano Kenya: Polisi waonya dhidi ya waandamanaji kuingia katika uwanja wa ndege JKIA

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Kaimu Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja Kirocho ameonya waandamanaji siku ya Jumanne kutojaribu kuingia katika maeneo yanayolindwa na serikali huku maandamano ya kuipinga serikali yakiendelea.

    Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Kanja amesema kuwa ripoti za ujasusi zinaonyesha kuwa maandamano ya sasa yamesheheni vitendo vya fujo vinavyotekelezwa na wahalifu.

    "Kulingana na duru za kuaminika, maandamano ya sasa yamegeuzwa kimbilio la wahalifu, walio na ari ya kupora na kuharibu mali ya Wakenya wachapakazi,"

    Afisa huyo alikuwa akizungumza dhidi ya wito wa vijana wa Kenya kutaka kuingia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International Airport kupinga utawala wa Ruto.

    "Polisi inasisitiza kwamba maeneo yaliyohifadhiwa hayafai kuingiliwa ikama livyoainishwa katika Sheria ya Maeneo yaliotengwa."

    Kulingana na afis huyo wa polisi, maeneo yote yaliyotengwa, ikiwa ni pamoja na mitambo ya LPG na Bitumen na mabohari ya petroli katika eneo la Embakasi , Uwanja wa ndege wa JKIA, hayapaswi kuingiwa na watu wasioruhusiwa.

    Aliendelea kusema kuwa Sheria ya Usafiri wa Anga ya Kenya inasema ni kinyume na sheria kuingilia ardhi yoyote ambayo ni sehemu ya uwanja wa ndege wa serikali.

    "Haitakubalika kuingia kwa Uwanja wa ndege ikiwa huna ruhusa, hiyo haitakubalika," alisema mkuu huyo wa polisi .

  12. Jeshi la Urusi lasema kuwa ndege zisizo na rubani 25 za Ukraine zimedunguliwa

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Wizara ya Ulinzi ya Urusi inadai kwamba ndege 21 zisizo na rubani za Ukraine "zilinaswa na kuharibiwa" kwenye eneo la Crimea Jumatatu usiku. Kulingana na ripoti hiyo, shambulio lililohusisha ndege mbili zisizo na rubani lilizuiliwa katika eneo la Bryansk, na idadi sawa hiyo katika mkoa wa Belgorod.

    Mkuu mji wa Sevastopol il uliotwaliwa na Urusi, Mikhail Razvozhaev, amesema usiku kwamba "zaidi ya ndege zisizo na rubani 15" zilidunguliwa juu ya Bahari Nyeusi, na "hakuna kitu kilichoharibiwa katika jiji hilo."

    Gavana wa Belgorod, Vyacheslav Gladkov aliripoti hapo awali kwamba karibu na Belgorod, katika kijiji cha Shchetinovka, ndege isiyo na rubani ilishambulia gari la abiria lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara. "Wanaume watatu walijeruhiwa.

    Upande wa Ukraine haujatoa maelezo yoyote kuhusiana na taarifa hizi.

    Unaweza pia kusoma:

  13. Maandamano Uganda: Usalama waimarishwa huku vijana wakijiandaa kuandamana hadi bungeni kuwasilisha madai yao

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wanajeshi na polisi wenye silaha wameonekana katika maeneo ya mji mkuu Kampala kabla ya maandamano ya vijana yaliyopangwa kufanyika Jumanne

    Hali ya usalama imeimarishwa mjini Kampala Uganda huku wanajeshi wenye silaha wakionekana kuizingira mitaa baada ya vijana kupanga kuandamana hadi kwenye bunge kuwasilisha madai yao, ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Spika.

    Awali rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni aliwaonya waandamanaji kwamba "watakuwa wakicheza na moto" ikiwa wataendelea na mipango ya kuandaa maandamano ya kupinga ufisadi hadi bungeni siku ya Jumanne.

    Haya ni baadhi ya madai ya waandamanaji waliyopanga kuyawasilisha bungeni leo:

    • Kujiuzulu kwa Annet Among kama Spika wa Uganda
    • Kujiuzulu kwa makamisha wanne
    • Kupunguzwa kwa idadi ya wabunge
    • Mbunge yoyote aliyehusika na kashfa yoyote ya ufisadi lazima ajiuzulu wakati uchunguzi ukiendelea
    • Kufanyika kwa ukaguzi wa mali na mtindo wa maisha wa wabunge na kuutangazwa
    • Kukatwa kwa mishahara na marupurupu ya wabunge wote hadi shilingi milioni 3 za Uganda
    • Kuwaruhusu Waganda kuendelea kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kukusanyinyika kwa amani bila kizuizi
  14. Bunge kuwakagua mawaziri wateule 11 walioteuliwa na Rais Ruto

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mawaziri 11 wateule wanatarajiwa kuulizwa maswali na wabunge kubaini iwapo wanafaa kuongoza wizara zilizopendekezwa kwao na rais Ruto

    Wabunge nchini Kenya Jumanne wataendelea na vikao baada ya mapumziko ya wiki tatu, kufuatia maandamano mabaya yaliyopelekea Bunge la Agosti kuvamiwa na waandamanaji tarehe 25 Juni.

    Ajenda kuu ya ya bunge hilo itakuwa ni kuwakagua mawaziri 11, ambao ni sehemu ya baraza la mawaziri wateule waliotangazwa na Rais William Ruto siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

    Spika wa Bunge la taifa Moses Wetang'ula alifichua kwamba mawaziri wote wateule watafanyiwa mtihani kubaini iwapo wanafaa kushikilia nyadhifa za uwaziri zilizopendekezwa.

    Viongozi hao wanarejea baada ya shughuli za bunge kufungwa kwa ukarabati kwa takriban mwezi mmoja .

    Unaweza pia kusoma:

  15. Israel inajiandaa kuanzisha "operesheni kubwa" Khan Yunis, huku mateka wengine wawili wakiuawa katika Ukanda wa Gaza

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Vifaru vya Israel vimeegeshwa karibu na mpaka kati ya Israel na Gaza

    Israel imetangaza kuuawa kwa mateka wake wawili waliokuwa wameshikiliwa huko Gaza, huku jeshi likisema katika taarifa tofauti kwamba Hamas inahifadhi miili hiyo na kwamba inafanya uchunguzi kuhusu mazingira ya vifo vyao.

    Familia za mateka waliozuiliwa zilisema katika taarifa kwamba Yagiv Buchstab mwenye umri wa miaka 35 na Alex Dansig mwenye umri wa miaka 76 walitekwa nyara wakati wa shambulio la Oktoba 7, ambalo lilifanywa na Hamas ndani ya Israeli, na kwamba mauaji yao yanawakilisha "ukumbusho wa hitaji la dharura" la kuwarudisha mateka wote nyumbani , kulingana na Shirika la habari la Ufaransa Agence France-Presse.

    Haya yanajiri huku jeshi la Israel likiwataka Wapalestina kuhama vitongoji vya mashariki mwa mji wa Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, na kuelekea katika eneo la Al-Mawasi kwa ajili ya kujiandaa kuanzisha kile ilichoeleza kuwa ni "operesheni kubwa" kujibu "shughuli za silaha" zinazofanywa katika eneo hilo.

    Jeshi limesema katika taarifa yake kwamba makombora yalirushwa kuelekea Israel kutoka huko, na kwamba eneo hili ni miongoni mwa maeneo yanayoitwa ya kibinadamu ambayo Israel iliwataka Wapalestina waliokimbia makazi yao kuhamia.

  16. Harris ana uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wajumbe kuwa mteule wa Democrat

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Makamu wa Rais Kamala Harris amepata uungwaji mkono kutoka kwa wajumbe wengi wa chama cha Democratic kuwa mgombea mteule wa chama hicho, mshirika wa BBC wa Marekani CBS News anaripoti.

    Utafiti uliofanwa na shirika la habari la Associated Press siku ya Jumatatu jioni ulisema Bi Harris amepokea uungwaji mkono wa zaidi ya wajumbe 1,976 wanaohitajika kushinda uteuzi katika duru ya kwanza ya upigaji kura.

    Wajumbe ni watu ambao wamechaguliwa kuwakilisha eneo lao la uchaguzi katika Kongamano la Kitaifa la chama cha Democrats (DNC).

    Uidhinishaji kama huo sio rasmi kisheria, lakini ikiwa jumla ya wajumbe wataendelea kumuunga mkono kati ya sasa na wakati wajumbe watakapopiga kura zao, zilizopangwa kufanyika kuanzia tarehe 1 hadi 7 Agosti, Bi Harris atashinda rasmi uteuzi wa chama.

    Wajumbe kutoka angalau majimbo 27 wametoa taarifa za wajumbe wao kamili wanaomuunga mkono Bi Harris, kulingana na CBS.

    Utafiti huo ni dalili ya msingi wa kumuunga mkono Bi Harris baada ya Rais Joe Biden kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho siku ya Jumapili.

    Maelezo zaidi:

  17. Netanyahu akabiliwa na wakati mgumu baada ya Biden kujiondoa

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) alisafiri kwa ndege kuelekea Israel siku chache tu baada ya shambulio la Oktoba 7 la Hamas

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaizuru Marekani wiki huku akikabiliwa na shinikizo la kukomesha vita vya Gaza, kutoka kwa Waisraeli na utawala wa Marekani. Je, msukosuko wa kisiasa huko Washington unaweza kuathiri vipi safari na mahusiano ya siku zijazo?

    Bw Netanyahu anatazamiwa kukutana na Joe Biden - ikiwa rais amepona Covid-19, na kuhutubia kikao cha pamoja cha Congress, atakuwa ni kiongozi pekee wa kigeni kufanya hivyo kwa mara ya nne.

    Safari hii inampa nafasi ya kurejea Washington baada ya miezi kadhaa ya mivutano kuhusu mtazamo wake mkali wa vita, na fursa ya kujaribu kuwashawishi Waisraeli kwamba hajavuruga uhusiano na mshirika wao muhimu zaidi.

    Lakini ziara hii imegubikwa na uamuzi wa Rais Biden wa kutogombea tena urais, jambo lilosababisha hali ya sintofahamu ya kisiasa kuhusu mshirika mwingine wa Israel katika Ikulu ya White House na pengine kuathiri mambo yaliyotarajiwa kuangaziwa katika ziara ya Bw Netanyahu.

    Nyumbani hakuacha mambo yakiwa mazuri hadi alipopanda ndege kuelekea Marekani. Msururu wa maandamano ulimtaka abaki nyumbani na kushughulikia makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas ili iwaachilie mateka wa Israel.

    "Mpaka atie saini mkataba ulio mezani, sioni jinsi anavyojiinua na kuvuka bahari ya Atlantiki kushughulikia machafuko ya kisiasa ya Marekani," alisema Lee Siegal, mmoja wa wanafamilia wenye ndugu waliotekwa na Hamas ambao wamejitokeza kuandamana.

    Kaka yake Keith mwenye umri wa miaka 65 ni mfungwa huko Gaza.

  18. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 23.07.2024