UN kutuma kikosi maalum cha polisi Burundi

Wanajeshi wa Umoja wa mataifa.
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Umoja wa mataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kutuma kikosi maalumu cha kimataifa nchini Burundi kujaribu kutuliza ghasia na ukiukaji wa haki za kibinadamu ambao umekumba taifa hilo la Afrika ya Kati kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Baraza hilo liliidhinisha pendekezo lililowasilishwa na Ufaransa, lililopendekeza zaidi ya maafisa wa usalama 228 wawe nchini humo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Rais Pierre Nkurunziza

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Rais Pierre Nkurunziza

Awali Serikali ya Burundi ilikuwa imesema kuwa haitawakubali zaidi ya polisi 50.

Zaidi ya watu 500 wameuawa wengi wao katika mauaji bila kufikishwa mahakamani.

Mauaji hayo yamelaumiwa maafisa wa polisi.

Ghasia nchini Burundi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ghasia nchini Burundi

Ghasia zilianza nchini humo wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza mipango yake ya kutaka kugombea urais katika awamu ya tatu, ambapo alifanya hivyo na kushinda.