Tetesi za soka Ulaya: Man City wanamtaka Trent Alexander-Arnold

AN

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester City wanaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya beki wa kulia wa England, Trent Alexander-Arnold, huku sintofahamu ikiendelea kuongezeka kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 katika klabu ya Real Madrid. (Teamtalk)

Liverpool wamewasiliana na wawakilishi wa aliyekuwa kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso, ili kuulizia upatikanaji wake, ambapo kocha huyo raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 44 anaripotiwa kutoa majibu chanya kwa klabu yake ya zamani. (AS – Spain)

Bournemouth wako karibu kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Mbrazil wa klabu ya Vasco da Gama, Rayan, mwenye umri wa miaka 19, kwa mkataba wa kudumu. (Athletic)

Xabi Alonso

Chanzo cha picha, getty

Maelezo ya picha, Xabi Alonso

Lazio wamewasilisha ofa yenye thamani ya hadi pauni milioni 15 kwa ajili ya kiungo wa Everton mwenye umri wa miaka 22, Tim Iroegbunam, raia wa England. (Football Insider)

Chelsea na Manchester United wanaendelea kumfuatilia mshambuliaji kijana wa Rennes mwenye umri wa miaka 18, Mohamed Kader Meite, raia wa Ufaransa. (CaughtOffside)

Wakati huo huo, klabu ya Rennes inayoshiriki Ligue 1 imekataa ombi la Chelsea la mwezi Januari kwa ajili ya beki wa kati wa timu ya taifa ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 21, Jeremy Jacquet, lakini Chelsea bado wana nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 wakati wa majira ya kiangazi. (Fabrizio Romano)

Kipa wa Borussia Monchengladbach na timu ya taifa ya Uswisi, Jonas Omlin, mwenye umri wa miaka 32, ambaye alikuwa akisakwa na Sunderland, amejiunga na Bayer Leverkusen kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Sky Germany)