Deng aapishwa nafasi ya Machar Sudan Kusini

Makamu mpya wa rais nchini Sudan Kusini, Taban Deng Gai, ameapishwa kwenye hafla iliyoandaliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Amechukua nafasi ya Riek Machar aliyetoroka Juba baada ya mapigano kutokea baina ya wanajeshi watiifu kwake na wanajeshi waaminifu kwa Rais Salva Kiir.
Watu karibu 300 waliuawa wakati wa vita hivyo.
- <link type="page"><caption> Riek Machar ''apinduliwa'' Sudan Kusini</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/07/160725_south_sudan_taban_deng" platform="highweb"/></link>
Hatua ya kundi moja ndani ya kambi ya Bw Machar kumuidhinisha Bw Deng kuchukua nafasi ya Bw Machar imepingwa na wanasiasa waaminifu kwake.

Chanzo cha picha, Reuters
Bw Deng ni nani?
Brigidia Taban Deng ambaye ni waziri wa madini amechaguliwa baada ya kikao cha wapinzani wa wa Machar katika kundi la Sudan People's Liberation Movement in-Opposition (SPLM-IO) ambao vinara wao wanapingwa na wafuasi wa Machar.
Bw Deng alikuwa mpatanishi mkuu wa Machar na hatua yake ya kuchukua wadhifa huo inaonyesha kuwa wametofautiana sana, hivyo basi kuweka mgawanyiko katika upinzani jambo ambalo linazidi kutatiza juhudi za kupata amani nchini Sudan Kusini.
Mbali na kuwa ni veterani wa vita vya ukombozi wa Sudan kusini hadi kujipatia uhuru wake hapo 2011, Maelezo ya Brigidia Jenerali Taban Deng Gai kuhusu elimu yake hayajulikani vyema.
Kabla suitafahamu hii ya sasa alikuwa mshirika wa karibu wa Bw Machar, na wote wanatoka jamii ya Wanuer ambalo ndilo kabila la pili kwa ukubwa nchini Sudan Kusini.
La kwanza kwa ukubwa ni lile la rais Salvaa Kiir la Wadinka.
Wanuer wengi wanaishi kazkazini mwa nchi hiyo.












