Wavulana wavalia sketi shuleni Uingereza

Sketi

Chanzo cha picha, WESLEY ALLEN

Maelezo ya picha, Wanafunzi hao walivalia sketi siku mbili

Wanafunzi hao wa darasa la mwaka wa tisa katika shule yaLonghill eneo la Rottingdean, Sussex Mashariki, walikuwa miongoni mwa wanafunzi 20 wavulana waliovalia kaptura za kuvaliwa wakati wa mazoezi badala ya suruali ndefu.

Baadhi walifukuzwa shuleni Jumanne na wengine kutengwa hadi siku iliyofuata. Waliokubali kuvua kaptura hizo na kuvalia suruali ndefu hawakuadhibiwa.

Lakini badala ya kuvalia sare kamili ya wakati wa masomo, kama walivyokuwa wameagizwa, wanafunzi wanne walirejea shuleni Alhamisi wakiwa wamevalia sketi.

Parker

Chanzo cha picha, ANGELA PARKER

Maelezo ya picha, Michael Parker, mmoja wa wanafunzi, akiwa na kaptura na akiwa na sketi

Watatu waliambia wavue sketi hizo lakini wote kwa pamoja wakakataa na ndipo wakaruhusiwa kuendelea kukaa shuleni.

Mwalimu mkuu Kate Williams aliwaambia wanaweza kuvalia mavazi yoyote, mradi yawe ni sehemu ya sare iliyokubalika shuleni.