Mtoto mnene zaidi duniani

Mtoto wa miaka 10 kutoka Indonesia, ambaye ametajwa kuwa mtoto aliyenenepa zaidi duniani ameanza kupewa chakula cha kupunguza uzani kwa kuwa wazazi wake wanahofia afya yake.

Chanzo cha picha, BBC Indonesia
Arya Permana ana uzani wa kilo 188 na ameorodheshwa kuwa na unene usio wa kawaida.

BBC ilizungumza na mamaake Rokayah huko Karawang Indonesia ambaye ana wasiwasi sana kuhusu afya ya mwanawe.








