Maisha ya Stephen Keshi kwa picha

Chanzo cha picha, Getty
Keshi, nahodha wa zamani wa kikosi cha Nigeria, alikuwa mmoja wa watu wawili pekee kushinda michuano ya kombe la bara Afrika akiwa mchezaji na kocha.

Alikuwa mkufunzi wa kikosi cha Nigeria kwa vipindi vitatu ,na kuisaidia Nigeria kufuzu katika michuano ya bara Afrika 2013 nchini Afrika Kusini pamoja na kombe la dunia mwaka 2014 huko Brazil.

Pia alifunza Togo na Mali,na aliwahi kuichezea timu ya Anderlecht ya Ubelgiji.

Akiwa mchezaji ,keshi alikuwa katika kikosi cha Super Eagles kilichoshinda kombe la bara Afrika mnamo mwaka 1994 na kushindwa kushirki katika mechi za robo fainali za kombe la dunia mwaka huohuo.

Keshi anadaiwa kuugua mshtuko wa moyo, kulingana na vyombo vya habari vya Nigeria.









