Unene kupita kiasi hudhoofisha uwezo wa kukumbuka

Chanzo cha picha, Getty
Watu wanene kupita kiasi wana kumbu kumbu mbaya zaidi kuliko wenzao wembamba zaidi, utafiti mdogo umeonyesha. Uchunguzi uliofanywa kwa watu 50 ulionyesha kwamba kuwa mmene kupita kiasi kulikua na uhusiano na '' kumbu kumbu ya msururu wa matukio " ama uwezo wa kukumbuka mambo yaliyopita.

Chanzo cha picha, SPL
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Experimantal Psychology, unadai kwamba kumbu kumbu ndogo zaidi inayosababishwa na milo ya hivi karibuni inaweza kusababisha ulaji wa kupita kiasi.
Hata hivyo, masuala mengine yanayochangia mtu kuwa na kumbu kumbu ndogo kama vile uelewa wa mambo kwa ujumla hayakuangaziwa na utafiti huu.

Chanzo cha picha, Don Mammoser Alamy
Vipimo walivyofanyiwa panya awali vilionyesha kwamba waliokua na unene zaidi walishindwa kufanya vizuri katika vipimo vya kumbu kumbu, lakini ushahidi kwa binadamu umekua na matokeo tofauti tofauti.
Utafiti wa hivi karibuni uliangazia zaidi kumbu kumbu za matukio katika mfulurizo -kama mkanda wa video katika ubongo wako - ambao hukumbuka harufu ya kikombe cha kahawa ama hisia za kushika mkono wa mtu mwingine.








