Fumio Kishida: Tazama kanda ya video kuhusu jaribio la shambulizi dhidi ya waziri mkuu wa Japan

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida alitolewa nje ya uwanja wa umma baada ya kile kilichoonekana kuwa bomu la moshi.

Mtu mmoja alikamatwa katika eneo la Wakayama, ambapo Bw Kishida alipaswa kutoa hotuba, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya eneo hilo.

Mmoja ya watu walioshuhudia tukio hilo alisema waliona mtu akirusha kitu, kisha kulikuwa na moshi, huku mwingine akisema walisikia kishindo kikubwa. Hakuna majeraha yaliyoripotiwa.

Polisi walisema wamemkamata mtu kwa kitendo hicho, lakini hadi sasa wamegoma kutoa maelezo zaidi.

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ameapa kuimarisha usalama huku mawaziri wa kigeni wakizuru nchini humo

Japan itakuwa mwenyeji wa mawaziri kutoka mataifa saba tajiri zaidi duniani siku ya Jumapili.

Bw Kishida alisema ni lazima nchi "iongeze juhudi zake" kuhusu usalama.

Picha ya kushangaza ilionyesha wakati bomy hilo liliporushwa

Mtu huyo alikamatwa kwa tuhuma za kuzuia biashara na baadaye kutambuliwa na mamlaka kama Ryuji Kimura mwenye umri wa miaka 24. Dhamira ya shambulio hilo bado haijulikani.