Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Madai ya kupotosha kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais Kenya

Huku Wakenya wakisubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne, baadhi ya watumiaji wa mtandao wamekuwa wakisambaza madai ya kupotosha kuhusu matokeo na mchakato wa upigaji kura.

Tunaangazia baadhi ya madai ambayo imeshirikishwa sana mitandaoni.

Kura zilizopigwa sio zaidi ya wapiga kura katika ngome ya Odinga

Mwanablogu anayemuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto alichapisha fomu ya matokeo kwenye Twitter inayoonyesha idadi ya wapiga kura katika kituo cha kupigia kura katika ngome ya mpinzani wake mkuu Raila Odinga ya Kisumu magharibi mwa Kenya ilikuwa 107.7%.

"Wapiga kura waliojiandikisha katika Soko la Kondele 1 wameonyeshwa kama 362 na waliopiga kura ni 390," aliandika kwenye ujumbe wa Twitter.

https://twitter.com/OleItumbi/status/1557080010753773568

Kusoma data kwenye fomu kunatoa hisia kwamba watu wengi zaidi ya waliojiandikisha kupiga kura walipiga kura zao.

Hata hivyo, ukiangalia takwimu rasmi za wapiga kura waliojiandikisha kwenye tovuti ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka inaonyesha idadi halisi ya wapiga kura katika kituo hicho ni 632.

Hitilafu ya kiuandishi - kubadili sita na tatu - ilifanya ionekane kana kwamba watu wengi walikuwa wamepiga kura kuliko jumla ya idadi ya wapiga kura - ambayo haikuwa hivyo.

Gachagua hakutambuliwa kwa kutumia sajili la kawaida

Msemaji wa Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga alidai kuwa mgombea mwezna wa Bw Ruto alifanikiwa kupiga baada ya jina lake kuangaliwa katika sajili iliyochapishwa.

Bw. Makau Mutua alidai kuwa kifaa cha kielekroniki kilichotumiwa kuwatambua wapiga kura katika kituo cha kupiga kura kilikumbwa na hitilafu,kushindwa kumtambua Bw. Rigathi Gachagua ambaye muungano wake wa kisiasa umekuwa ukipinga matumizi ya daftari la kawaida.

https://twitter.com/makaumutua/status/1556924449114492928

Ingawa kifaa hicho cha kielektroniki kilikuwa na matatizo ya kumtambua Bw Gachagua, hatimaye kilifanya kazi baada ya kusugua kidole chake kwenye nywele zake na kumruhusu kupiga kura.

Akaunti ya Twitter ambayo haihusiani na IEBC

Akaunti ya Twitter inayojiita IEBC Tabulation imekuwa ikichapisha baadhi ya matokeo ya uchaguzi na kutumia nembo ya tume ya uchaguzi kama picha ya wasifu na jalada.

Akaunti hiyo ambayo sasa imesitishwa, ilikuwa imeorodhesha anwani ya tovuti ya IEBC katika maelezo yake ambayo ingepotosha zaidi watu kuwa ni akaunti halali iliyounganishwa na tume hiyo.

Ukiangalia kwa karibu utakuwa na kila sababu ya kutilia shaka uhalali wake.

Iliundwa Aprili mwaka huu na imekuwa ikichapisha maudhui ya ngono kwa wiki kadhaa.

Baadhi ya machapisho ya hivi majuzi pia yalikuwa yanaonyesha upendeleo wa wazi kwa wagombeaji fulani wa kisiasa, jambo ambalo halikutarajiwa kutoka kwa akaunti rasmi.

Imesimamishwa kwa kukiuka sheria za Twitter.

Hakukua na upigaji kura nchini Australia

Ujumbe uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya WhatsApp, Twitter na Facebook zilidai upigaji kura wa nje ya nchi ulifanyika Sydney, Australia na kura tayari zimehesabiwa.

Jumbe hizo zilidai wapiga kura wote walijitokeza na ulikuwa ushindi kwa Bw Odinga.

Tofauti za ujumbe huu ziliachwa Sydney.

Lakini haya yote yaliundwa kwani hakukuwa na upigaji kura unaofanyika nchini Australia.

Tume ya uchaguzi inasema zoezi la kupiga kura kwa Wakenya wanaoishi nje ya nchi linafanyika katika nchi zifuatazo: Burundi, Tanzania, Rwanda, Uganda, Afrika Kusini, Uingereza, Canada, Marekan, Sudan, Kusini,Qatar, UAE, na Ujerumani.

Australia haikuwa miongoni mwa nchi hizo,

Na ubaloi wa Kenya uko katika mji wa Canberra na walasio Sydney.

IEBC ina siku saba kutangaza matokeo.