Je, lishe ya mboga mboga ni nzuri kwa watoto?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kamala Thiagarajan anachunguza kile ambacho familia za walaji mboga zinaweza kujifunza kutoka kwa utamaduni wa kale wa India wa upishi unaotegemea mimea, pamoja na maarifa mapya ya kisayansi.
Mwaka 2010, Ashish Kumar Jain, wakati huo alikuwa na umri wa miaka 28 akifanya kazi nchini Uingereza kama mtaalamu wa TEHAMA, alijionea video ya mtandaoni ambayo ilimvutia sana.
Ilielezea ukatili unaofanywa na sekta ya maziwa, hasa kwa ndama.
Akiwa mzazi mjamzito, na wakati ambapo alikuwa akitamani kurudi India kwa ajili ya kumzaa mtoto wake wa kwanza, anasema ilimshawishi yeye na mke wake kubadili lishe hadi ya mboga mboga.
Wakiishi Indore, jiji lililo katikati mwa jimbo la India la Madhya Pradesh, wenzi hao waliamua kumlea mtoto wao kama asiyekula nyama pia.
Leo, binti yake Arul ni mtoto mwenye afya njema, mwenye umri wa miaka 11 na anayependa mboga mboga.
Kumlea kama mtoto asiye kula nyama hakukuwa na mfadhaiko kama kushughulikia maswala kutoka kwa familia kubwa kuhusu chaguzi hizi, anasema Jain.
Sababu moja ilifanya mabadiliko hayo kuwa rahisi, anasema: Historia ndefu ya India ya kupika bila nyama.
Ingawa mila hiyo inaelekea kuwa ya mboga badala ya mboga mboga, ina masomo muhimu juu ya kuongeza nguvu ya lishe ya milo inayotokana na mimea - ambayo inaweza kufaidisha idadi inayoongezeka ya watu wazima na watoto wasio kula nyama sio tu nchini India, lakini ulimwenguni kote.
Takriban watu milioni 400 nchini India (idadi ya 39% ya wakazi wa nchi hiyo), wanajitambua kama walaji mboga kwa sababu za kidini na nyinginezo, ikilinganishwa na takriban 5% pekee nchini Marekani.
Mlo wa wasio kula nyama sio sawa na chakula cha wasiokula chochote kitokanacho na nyama kwa kawaida hujumuisha maziwa, kwa mfano, wakati chakula huepuka bidhaa zote za wanyama.
Hata hivyo, urithi wa mboga wa India umesababisha vyakula mbalimbali hasa vyakula vinavyozingatia mimea vinavyotoholewa kwa urahisi kulingana na mahitaji ya wasiokula nyama na chochotekitokanacho na nyama.
Sambamba na maarifa mapya ya kisayansi kuhusu vyakula vinavyotokana na mimea kutoka kwa watafiti duniani kote, uzoefu huo unaweza pia kuwasaidia wazazi kujibu swali muhimu: je, lishe ya mboga mboga pekee ni salama kwa watoto?
Idadi ya wasiokula nyama na chochote kitokanacho na hicho inaendelea kuongezeka

Chanzo cha picha, Ashish Kumar Jain
Ulaji mboga pekee umekuwa ukivutia wengi kote ulimwenguni, ukiungwa mkono na kampeni mbalimbali kama vile 'Veganuary' (ambayo inahimiza watu kula mboga mboga kwa mwezi mmoja) pamoja na kuongezeka kwa ufahamu wa faida za hali ya hewa za lishe isiyo na nyama na maziwa.
Utafiti unaokua unapendekeza lishe inayotokana na mimea ina faida nyingi za kiafya kwa watu wazima.
Nchini India, vuguvugu linalokua likiendeleza ulaji wa mboga mboga tu linaegemea mila ya zamani, huku vikundi vya mitandao ya kijamii vya wasio kula nyama na biadhaa za wanyama na washawishi wakiangazia nguvu ya lishe ya nafaka za ndani, kunde na nafaka.
Wahindi wasiokula nyama na bidhaa zozote zinazotokana na wanyama hubadilisha mapishi ya kitamaduni katika vikundi kama vile ''Kupika na Mtama'', ''Hebu tushiriki safari yetu ya mtama'', ambako kunakuza ueneaji wa zao la nafaka nchini India.
Washawishi wa mboga mboga wanasisitiza faida za viungo vya zamani kama vile dengu, mbaazi na maharagwe ya mung.
Mnamo mwaka wa 2016, Chuo cha Kimataifa cha Ujerumani, shule ya makazi katika mji wa Kusini mwa India wa Chennai, ilitengeneza vichwa vya habari ilipokuwa shule ya wanaokula mboga mboga pekee.
Na ingawa walaji mboga wengi wa Kihindi hutegemea sana bidhaa za maziwa kama vile (siagi iliyosafishwa), mtindi, na (jibini), Jain anadokeza kwamba hapo awali haikuwa hivyo, kwani vyakula vingi vya kitamaduni havina maziwa.
Hata hivyo, kwa watoto, hatari na faida za lishe ya wanaokula mboga mboga pekee ni ngumu zaidi kuliko kwa watu wazima.
Kupanga lishe salama ya mboga mboga

Chanzo cha picha, Getty Images
Labda jambo muhimu zaidi la kuzingatia ni kwamba mtoto anayekua anahitaji virutubishi maalum kwa kila hatua ya ukuaji.
Ikiwa hizo zimekosa, matokeo yanaweza kuwa hatari, hasa kwa watoto wadogo.
Chakula chao pia kinahitaji kuwa na virutubishi na wingi wa nishati, kwa sababu chakula chao huwa ni kidogo.
''Watoto wachanga na watoto wanakua na kukua kwa kasi (hasa wakati wa utotoni) na wana mahitaji ya juu sana ya virutubishi fulani huku wakiwa na matumbo madogo.
''Hii ina maana kwamba vyakula wanavyopewa vinapaswa kuwa na virutubisho vya juu zaidi na nishati ya kutosha kwa ujazo mdogo,'' anasema Mary Fewtrell, profesa wa lishe ya watoto katika Taasisi ya Afya ya Mtoto ya Chuo Kikuu cha London, huko Great Ormond Street.
Kwa watoto wachanga, maziwa ya mama yanaonekana kuwa njia bora zaidi ya kutoa lishe na nishati wanayohitaji kukua, wakati kwa watoto wachanga na watoto wadogo, mlo wa vegan yale wale wasiokula nyama wala kitokanacho na wanyama wanahitaji kupangwa kwa uangalifu ili kuhakikisha kuwa lishe yao inakidhi mahitaji yao.
Ulaji mboga potofu kwa kweli umesababisha baadhi ya visa adimu, vinavyoweza kuepukika katika kundi hilo la umri. Mnamo 2016, mtoto wa mwaka mmoja huko Milan, Italia alichukuliwa kutoka kwa wazazi wake baada ya vipimo vya damu kubaini kuwa alikuwa na kiwango cha chini cha kalsiamu baada ya kufuata lishe ya mboga.
Vyombo vya habari vya Italia viliripoti kwamba mtoto huyo wa mwaka mmoja alikuwa na uzito wa mtoto wa miezi mitatu, na viwango vyake vya kalsiamu vilitosha tu kuishi kwa shida.
Mnamo mwaka wa 2017, mahakama nchini Ubelgiji iliwatia hatiani wazazi wa mtoto mchanga wa miezi saba ambaye alikufa kutokana na upungufu wa maji mwilini na utapiamlo baada ya kulishwa mlo wa maziwa ya mboga yaliyotengenezwa kwa shayiri, buckwheat, wali na quinoa.
Kwa watoto wakubwa, utafiti unapendekeza kwamba mlo wa vegan unaweza kuwa na manufaa - lakini pia, baadhi ya hasara.
Utafiti wa msingi juu ya watoto wanaolishwa mbogamboga pekee

Chanzo cha picha, Bhavya Chandra Prem
Mnamo mwaka 2021, utafiti uliochapishwa katika Jarida la Amerika la Clinical Nutrition ulilinganisha matokeo ya kiafya ya lishe ya mboga mboga, na ile ya mboga mboga na nyama kwa watoto wa Poland wenye umri wa miaka 5-10.
Utafiti huo ulijumuisha walaji mboga mboga 63, 52 wa mboga mboga na wasiokula chochote kitokanacho na wanyama na 72 wanaokula mboga na bidhaa zitokanazo na wanyama.
Malgorzata Desmond, mwandishi mkuu wa utafiti huo, sasa ni mtafiti mwenzake wa heshima katika Taasisi ya Afya ya Mtoto ya UCL Great Ormond Street.
''Ingawa idadi ya watoto katika utafiti wetu ilikuwa ndogo, huu ni utafiti mkubwa zaidi wa aina yake kuwahi kufanywa haswa kwa watoto wasio chochote zaidi ya mboga wa umri huu; wa kwanza ambao ulishirikisha (zaidi ya) washiriki 50 katika kila kikundi la lishe cha mimea na kuwalinganisha. kwa wanaolingana kwa uangalifu,'' Desmond anasema.
Utafiti huo ulibainisha pointi nzuri na mbaya kwa watoto wanaokula mboga mboga pekee, anasema Fewtrell, ambaye aliandika utafiti huo.
''Habari njema ilikuwa kwamba kwa kulinganisha na wenzao ambao wanakula moga mboga na bidhaa za wanyama, watoto wasiokula nyama walikuwa wembamba na walio katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa moyo, kama vile kolesteroli Iliyo katika damu,'' anasema.
Hii inaweza kuchangia kupungua kwao kwa ugonjwa wa moyo baadaye maishani.
''Hasara ni kwamba walikuwa wafupi na walikuwa na uzito wa chini wa mfupa kuliko ilivyotarajiwa kwa umri wao.''
Baadhi ya matokeo ya utafiti yalikuwa ya kushangaza.
Kwa mfano, watoto wanaokula mboga mboga walikuwa na tabia ya kula vyakula visivyo na faida kubwa mwilini kama vile pizza na vinywaji baridi - ukumbusho kwamba mlo wa mboga peke yake hauwahakikishii menyu yenye afya na uwiano.
Kama inavyoweza kutarajiwa, waliokuwa wanakula mboga mboga na bidhaa zitokanazo na nyama ndio walikuwa na makadirio ya juu zaidi ya ulaji wa protini, na wale waliokuwa wanakula mboga mboga pekee ndio walikuwa wa chini kabisa - lakini walaji mboga walikuwa na makadirio ya juu zaidi ya ulaji wa kalsiamu.
Kwa ujumla, tafiti za lishe zinazozingatia mimea - kwa hivyo, wanaokula mboga mboga lakini sio mboga pekee - kulionekana kuhitimisha kuwa ni salama kwa watoto.
Utafiti wa muda mrefu wa watoto wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi miaka minane nchini Marekani uligundua kuwa hakuna ushahidi wa tofauti za kimatibabu katika ukuaji au hali ya lishe kwa watoto walio na lishe ya mboga, ikilinganishwa na wenzao.
Hata hivyo, watoto wa mboga mboga (sampuli pia ilijumuisha pia wale mboga mboga peke yake) wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito mdogo.
Lishe inayotokana na nyama inaweza pia kuwa na hatari zake yenyewe, kutokana na homoni zinazopatikana katika nyama na maziwa - ingawa ushahidi juu ya hili ni mchanganyiko.
Hata hivyo, pia ilisemekana kuwa maziwa yana faida kadhaa za kiafya.
Lakini ukaguzi unahitimisha kuwa ingawa kiasi cha estrojeni katika maziwa ya ngombe ni cha chini sana kuathiri afya ya watu wazima, utafiti zaidi unapaswa kufanywa kuhusu athari kwa watoto, hasa katika hatua za awali za ukuaji.












