Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hatua ya Singapore ya kuhalalisha ugandishaji wa mayai inasema nini kuhusu jamii yake
Baada ya miaka ya majadiliano, Singapore ilitangaza mwezi uliopita kwamba ingeondoa marufuku kwa wanawake wasio na waume ambao wanataka kugandisha mayai yao kwa sababu zisizo za kiafya.
Lakini wakati wengi wamefurahishwa na kukaribisha hatua hizo, wengine wanasema bado kuna mengi yanayohitajika katika utaratibu huo na yanaonyesha Singapore bado ina safari ndefu kabla ya sera hiyo kuzingatiwa kuwa inajumuisha kila mmoja.
Gwendolyn Tan alikuwa na umri wa miaka 31 alipoamua kugandisha mayai yake.
Mwanamke mseja anayefanya kazi, siku zote alitaka kuwa na watoto wake wa kuwazaa - lakini hakuwa na mwenzi wake bado.
Suluhisho bora zaidi kwake lilikuwa kugandisha mayai yake - kuhakikisha kukutana na mtu si jambo la kukimbilia kwa ajili tu ya kupata watoto.
Alisafiri kwenye ndege peke yake na kuvuka maelfu ya maili hadi mji mkuu wa Thailand wa Bangkok, ambapo utaratibu ulifanyika.
Haikuwa nafuu - Gwendolyn anasema alitumia kiasi cha S$15,000 (£8571; $10932) kwa utaratibu huo.
Lakini kwake na wanawake wengi nchini Singapore ambao walitaka kugandishwa kwa mayai yao - kwenda ngambo lilikuwa chaguo pekee walilokuwa nalo.
Kugandisha yai ni marufuku nchini Singapore isipokuwa kwa wachache.
Mnamo mwaka 2020, Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Familia ya nchi hiyo, ilisema walipaswa kuzingatia ''maswala ya kimaadili na kijamii juu ya kuhalalisha kugandisha yai'', miongoni mwa mambo mengine.
Walakini, mwezi uliopita, katika hatua ya msingi, serikali ilitangaza kwamba kuanzia 2023, wanawake wasio na waume kati ya 21-35 wataruhusiwa kugandisha mayai yao.
Lakini kwa tahadhari - wanaweza kutumia mayai ikiwa tu wameolewa kisheria.
Hii haijumuishi mara moja wanawake wasio na waume ambao wanaweza kutaka kulea watoto nje ya ndoa na pia wapenzi wa jinsia moja ambao hawawezi kuolewa chini ya sheria za Singapore.
Kuhifadhi mayai ya uzazi
Ulimwenguni kote, ugandishaji wa mayai umekuwa maarufu.
Inahusisha kukusanya mayai ya mwanamke kutoka kwenye ovari yake, kuyahifadhi katika hali ya kuganda kwa kina na kuyayeyusha katika hatua ya baadaye.
Kwa wakati huu, huwa yanawekwa pamoja na manii kwa matumaini kwamba kiinitete hujitengeneza na mimba inakua.
Mnamo mwaka wa 2009, ni wanawake 475 pekee waliogandisha mayai yao nchini Marekani, kulingana na data za Jumuiya ya Teknolojia ya Usaidizi ya Uzazi.
Kufikia mwaka 2018, wanawake 13,275 walikuwa wamefanya hivyo - ongezeko la zaidi ya 2500%.
Singapore imeshuhudia ongezeko kama huo.
Kliniki moja katika mji mkuu wa Malaysia wa Kuala Lumpur ililiambia shirika la habari la AFP kwamba mwaka wa 2021, waliona ''idadi inayoongezeka'' ya wanawake wa Singapore wanaokuja kufanyiwa mchakato huo.
Na kadiri watu wengi zaidi nchini Singapore walivyoanza kugeukia kugandisha mayai - walianza pia kuzungumzia marufuku hiyo.
Emma, ambaye mnamo mwaka 2021 alianza kampeni ya 'My Eggs My Time' - inayotaka ugandishaji wa yai uhalalishwe nchini Singapore, alikuwa miongoni mwao.
''Alijibu, hatua hiyo [ilikuwa] chanya. Nilipokea ujumbe chungu nzima kutoka kwa wanawake wakishirikisha simulizi zao kuhusu kwa nini walitaka kugandisha mayai yao,'' alisema Emma, ambaye anatambulika kwa jina lake la kwanza.
Mada hiyo pia ilikuwa ni ile ambayo ililetwa mara kwa mara bungeni na Mbunge Cheng Li Hui.
''Mwaka wa 2016, nilipoibua mada hii mara ya kwanza, watu walikuwa wakionyesha kama wanauliza, Hii ni nini? Wewe ni wa kisasa sana kwetu,'' alisema.
''Lakini kadiri muda ulivyokwenda, kumekuwa na mazungumzo mengi zaidi. Mwaka jana [baada ya kuleta mada hii], niliweza kuona tofauti kubwa [katika miitikio]. Nilipata barua pepe nyingi zaidi za kunishukuru.''
Wengi pia wamekaribisha ukweli kwamba kugandisha yai kunaweza kusaidia kuongeza kiwango cha uzazi cha Singapore, ambacho ni miongoni mwa viwango vya chini zaidi duniani.
Mnamo mwaka 2020, kuzaliana kulifikia kiwango cha chini katika kihistoria cha watoto 1.1 kwa kila mwanamke, ikilinganishwa na wastani wa kimataifa wa 2.4.
''Hii ni hatua imewadia wakati muafaka,'' alisema Shailey Hingorani, mkuu wa Utafiti na Utetezi, lakini anaongeza kuwa kuna tahadhari kadhaa ambazo 'zinakatisha tamaa'.
Kiini cha jadi cha ufafanuzi wa familia
Singapore ni moja wapo ya miji ya kisasa zaidi ulimwenguni - lakini pia ina uhafidhina - haswa katika dhana yake ya familia, ambayo inarejelea kama ''msingi vya ujenzi wa jamii''.
Kwa kiasi kikubwa jamii hiyo inajaribu kusukuma mbele ''ufafanuzi wa kuwa na familia ndogo''. ... ambao kiutamaduni hufafanuliwa kama baba, mama na watoto wao'', asema Bi Hingorani.
Sera za serikali bila shaka zinalenga kuhimiza ukuaji wa familia kama hizo.
Wazazi wasioolewa na wasio na wenzi wao, kwa mfano, wanastahiki tu ruzuku ndogo ya nyumba.
''Sera za makazi za Singapore hazimchukulii mama mmoja ambaye hajaolewa na watoto wake kama 'msingi wa familia', na hivyo kuwazuia kuhitimu kupata ruzuku fulani,'' alisema Bi Hingorani.
Watu wasio na waume - ikiwa ni pamoja na wanandoa wa jinsia moja ambao hawawezi kuoana kihalali - lazima pia wangoje hadi umri wa miaka 35 ili kununua nyumba za makazi za umma, na hata hivyo wawe na idadi ndogo ya chaguzi za kuchagua.
Alipoulizwa kama kulikuwa na mipango ya kubadilisha sera hizi, msemaji kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Familia ya Singapore, alisema sera ya umma ya nchi ''inahimiza uzazi ndani ya ndoa''.
Bi Hingorani aliongeza kuwa hii ''ilikuwa ya kukatisha tamaa, lakini haishangazi'', na ametoa wito kwa Singapore ''kufanya ugandishaji wa mayai uliochaguliwa kupatikana kwa wote bila kujali hali ya ndoa, uwezo wa kifedha na hali ya elimu''.
Suala jingine ambalo limeletwa na sera hiyo mpya ni kwamba Singapore itawaruhusu tu wanawake walio na umri wa chini ya miaka 35 kugandisha mayai yao.
Hii ni kwa mujibu wa miongozo iliyowekwa na shirika la udhibiti wa uzazi la Uingereza HFEA, ambalo linasema uzazi hupungua kulingana na umri, hivyo wakati mzuri wa kugandisha yai ni kabla ya mwanamke kufikia umri wa miaka 35.
Hata hivyo data imeonyesha kuwa umri unaojulikana zaidi ambao wanawake nchini Uingereza hutibiwa ni miaka 38, na wengi hugandisha mayai wakiwa na umri wa miaka ya 40.
Bi Cheng anasema wanawake nchini Singapore huenda wakakabiliwa na hali kama hiyo.
''Sisi ni taifa lililoendelea, tumeelimisha wanawake ambao wana taaluma na uchaguzi, nadhani umri wa miaka 35 ni mdogo sana. Ikiwa mtoto wa miaka 37 ana hifadhi nzuri ya mayai ina maana tuwazuie kugandisha mayai yao?,'' alisema.
Lakini shirika la Jamii linasema ukomo wa umri ''unatokana na ushahidi wa kimataifa wa kisayansi na makubaliano ya kitaalamu kwamba ubora wa yai huelekea kupungua sana baada ya miaka 35'', ingawa walisema inawezekana kwa wanawake kukata rufaa dhidi ya kikomo hiki cha umri kwa msingi wa watu hutofautiana.
Waliongeza kuwa ''wanaweza kukagua kikomo hiki cha umri... ikiwa kutakuwa na maendeleo ya kimatibabu ambayo yataruhusu uwezekano mkubwa wa kushika mimba kwa mayai ambayo yanatoka kwa wanawake wa umri mkubwa."
Lakini wanawake kama Gwendolyn wanahisi kwamba wakati hatua ya serikali ina vikwazo, anaamini kwa ujumla ''itawawezesha'' wanawake zaidi wa Singapore kufanya mayai yao yagandish
''Tunapaswa kuruhusu wanawake kuwa na wakala - ni mayai yangu. Hivyo kama nina umri wa miaka 40 na ninataka kuwa mzazi asiye na mwenzi, basi hilo ni chaguo langu. Lakini nadhani hatimaye, mwisho wa siku, ukweli kwamba sisi kuruhusu hili ni dhahiri ni mabadiliko makubwa ya hatua. Je, tunaweza kufanya zaidi? Kweli kabisa. Lakini nadhani kwa sasa, tunapaswa kusherehekea mabadiliko haya.''we.