Siku ya Malaria duniani: Mabadiliko ya tabia nchi na chanjo yanavyoathiri mapambano dhidi ya ugonjwa unaoua duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna zaidi ya visa milioni 240 vya malaria kila mwaka, huku ugonjwa huo ukiwauwa zaidi ya watu 400,000 katika nchi 60 kila mwaka.
Tarehe 25 Aprili ni siku ya Malaria duniani wakati ambapo Shirika la Afya duniani (WHO) hutoa uelewa kwa jumla kuhusu juhudi za pamoja na kuiepusha dunia na malaria.
Lakini huku mapambano hayo yakisaidia kuanzishwa kutolewa kwa chanjo ya kwanza duniani iliyoidhinishwa na WHO, mabadiliko ya tabia nchi, na ongezeko la viwango vya joto vinamaanisha kuwa ugonjwa huo unaoua unaweza kusambaa katika maeneo mengine mapya ambako haukuwahi kushuhudiwa kabla.
Kusambaa kwa ugonjwa unaoua
"Viwango vya juu zaidi ya joto huongeza uwezo wa mbu kubeba vimelea wa malaria ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa ," anasema Dkt Isabel Fletcher, meneja wa teknolojia ya dataza kisayansi katika taasisi ya Wellcome Trust charity.
"Mabadiliko ya tabia nchi yatafanya maeneo mengi zaidi ya dunia kuwa mahala panapofaa kwa ajili ya usambazaji wa mbu. Kwasababu dunia itakuwa na joto zaidi , malaria inatarajiwa kupanuka zaidi katika maeneo ya nyanda za juu, ambayo kwa sasa yanaweza kuwa baridi sana kiasi kwamba mbu hawawezi kusambaza ugonjwa ," alitahadharisha.
Kulingana na jopo la Umoja wa Mataifa la serikali kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (IPCC),hata kama sera zote za kupunguza hewa ya kaboni ambazo serikali ziliweka kufikia mwaka 20202, zilitekelezwa kikamilifu, dunia bado imeendelea kuchemka kwa kiwango cha nyuzijoto 3.2 katika karne hii. Lengo la dunia ni kutaka ongezeko la viwango vya joto vibakie katika nyuzijoto 1.5 au chini yake kwa kupunguza hewa ya kaboni.

Chanzo cha picha, Getty Images
Zaidi ya kuongezeka kwa viwango vya joto dunaini, watafiti wanaonya kwamba kupungua kwa viwango vya mvua na unyevu nyevu na hata hali ya ukame pia kunaweza kusababisha ukuaji wa wa haraka wa mbu wanaobeba ugonjwa katika maeneo ambayo haukuwahi kuripotiwa kabla.
"Tafiti zimeonyesha katika mataifa ya Caribbean na katika Brazili kwamba wakati kunakipindi cha ukame, watu watatunza maji zaidi. Hilo husababisha makazi mazuri ya mbu . Hiyo ndio maana katika hali za ukame, unaweza kupata ongezeko la maambukizi ya homa ya dengue ," Dkt Fletcher anasema.
Kuna hofu kwamba kama hii hutokea kwa homa ya dengue, itatokea pia kwa malaria.
Mabadiliko ya tabia nchi yanweza kupunguza kusambaa kwa malali katika baadhi ya maeneoambako tayai hali ilikuwa mbaya zaidi, ndio maana Dkt Fletcher anadhani kwamba uelewa mkubwa zaidi wa athari za mabadiliko ya hali ya joto litakuwa ni jambo muhimu katika kuendelea kupambana dhidi ya ugonjwa wa malaria.
"Kwa kubuni makadiria ya hatari katika siku zijazo, tunaweza kutambua watu ambao wako katika hatari na hivyo kuwalenga katika juhudi za kuzuwia ipasavyo kusambaa kwa ugonjwa ," anasema.

Ni zipi dalili za malaria?
Malaria ni ugonjwa hatari unaosambazwa nna mbu, ambao unaweza kusababisha kifo iwapo haubainika na kutibiwa haraka. Dalili zake ni pamoja na:
- Viwango vya juu vya joto mwilini, kutoka jasho na kuhisi baridi mwilini
- Maumivu ya kichwa na kuhisi kuchanganyikiwa
- Kuhisi mchoko na kulala (hususan kwa watoto)
- Kuhisi na kuumwa, tumbo na kuharisha
- Kupoteza hamu ya kula
- Maumivu ya mwili
- Ngozi kuwa ya manjano au macho kuwa meupe
- Maumivu ya koo, kukohoa na kupata ugumu wa kupumua
Chanzo: NHS

Mafanikio ya chanjo
Lakini huku mabadiliko ya tabia nchi yakitishia kuyafanya mapambano dhidi ya ugonjwa kuwa magumu, mafanikio mapya yamepatikana katika vita dhidi ya malaria.
WHO imetangaza hivi karibuni kuwa zaidi ya watoto milioni moja katika mataifa ya Ghana, Kenya na Malawi wamekwishapokea dozi moja au mbili za chanjo ya kwanza ya dunia ya malaria, chini ya mpango ulioratibiwa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa.
Majaribio ya kwanza ya chanjo ya malaria, kwa mara ya kwanza yaliyoanzishwa na serikali ya malawi katika mwezi wa Aprili 2019, yameonyesha kwamba chanjo ya RTS,S/AS01 (RTS,S) ni salama na ni rahisi kuitoa, na kwamba inapunguza kwa kiasi kikubwa makali ya malaria.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni upi mkakati wa WHO wa kuzuwia malaria?
- WHO imepanga utaratibu wa kupambana na ugonjwa huo . Malengo ya shirika hilo ni pamoja na:
- Kupunguza visa vya malaria kwa walau 90% ifikapo mwaka 2030
- Kupunguza viwango vya vifo vya malaria kwa walau 90% ifikapo 2030
- Kutokomeza malaria katika walau nchi 35 ifikapo mwaka 2030
- Kuzuwia ugonjwa wa malaria katika nchi zote ambazo hazina malaria
Chanzo: WHO

Shirika hilo linakadiria kuwa chanjo ya malaria inaweza kuyaokoa maisha ya watoto kati ya 40,000 hadi 80,000 wa Afrika kila mwaka.
"Tuliweza kuangalia athari a chanjo baada ya miaka miwili na usalama wake. Kile tulichokiona kilikuwa kwamba chanjo ile ilikuwa salama na iliweza kuvumilika sana," anasema Dkt Mary Hamel, ambaye anaongoza utekelezwaji wa mpango wa chanjo ya malaria ya WHO.
Katika kipindi cha miaka hiyo miwili ya uchunguzi wa chanjo, kulikuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja kushuka kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini na kushuka kwa visa vya kutishia maisha vya malaria kwa kiwango cha theluthi moja ."
Zaidi ya hayo chanjo ya RTS,S, kuna chanjo nyingine za malaria zinazofanyiwa majaribio. R21/Matrix-M, ni miongoni mwa zile ambazo katika awamu ya kwanza ya majaribio.
Kampuni kubwa ya famasia BioNTech pia inalenga kutengeneza chanjo ya malaria kwa kutumia teknolojia inayofanana na ya mRNA ambayo ilitumiwa wazi kwa mara ya kwanza katika chanjo yake ya Covid-19.
Je chanjo inafanyaje kazi? Na je ipo kwa kiwango cha kutosha?

Chanzo cha picha, Getty Images
Malaria ni vimelea ambavyo huvamia na kuharibu seli za damu za binadamu ili kutengeneza upya na huenezwa kwa mbu anayeng'ata na kufyonza damu.
Chanjo iliyopo ya RTS,S huwalenga mbu hatari zaidi ambao wanapatikana sana katika Afrika : Plasmodium falciparum.
Wakati mtu anapoumwa na mbu, vimelea hawa huingia kwenye mfumo wa damu na kuambukiza seli za ini. Chanjo imetengenezwa kuzuwia vimelea hao kuambukiza ini, ambako huweza kukua na kuzaliana, na kuingia tena ndani ya mfumo wa damu na kuathiri chembechembe nyekundu za damu, na hivyo kusababisha kuumwa.
Chanjo hiyo inahitaji dozi nne ili iwe na ufanisi, dozi tatu za kwanza hutolewa baada ya mwezi mmoja mmoja kwa watoto wenye umri wa miezi mitano, sita , na saba na chanjo ya mwisho hutolewa mtoto anapokuwa na umri wa miezi 18, kwa lengo la kuimarisha chanjo za tatu za awali.
Wataalamu wa afya wanashauri kwamba chanjo itumiwa na mikakati kadhaa ili kuzuwia maambukizi na kupunguza kwanza kusambaa kwa ugonjwa.
WHO inatarajia dozi milioni zaidi ya 80 zitahitajika kila mwaka, hususan katika mataifa yote yaliyopo kusini mwa jangwa a sahara.
Kiwango hiki cha dozi za chanjo cha hali ya juu kinakuja na changamoto zake.
"Kiwango cha chanjo kinachotakikana kitakuwa kikubwa kuliko dozi zitakazokuwepo na kwa haraka ambapo watengenezaji wanatakiwa kuongeza kiwango cha uzalishaji ," Dkt Hamel anaelezea.
Kwa sasa kuna mtengenezaji mmoja tu wa chanjo ya malaria, GlaxoSmithKline (GSK).
"Mpango wa GSK ni kuongeza hadi dozi milioni 15 kwa mwaka ," anasema Dkt Hamel.
"Kusema ukweli tunahitaji kushirikiana katika kujitolea na kuwa na utashi wa kisiasa na kuhakikisha kuna chanjo za kutosha kuweza kuwafikia watoto hawa ambao wako katika hatari ya kuugua malaria mbaya."













