Urusi na Ukraine: Ni nchi gani za Ulaya zisizounga mkono upande wowote (na ni nini Ukraine inaweza kujifunza kutokana na uzoefu )

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema serikali yake imejiandaa kuangalia uwezekano wa kuwa na hadhi ya kutofungamana na upande wowote kama sehemu ya mkataba wa amani na Urusi.
Mtaalamu wa historia ya jeshi, ulinzi na mtaalamu usalama Peter Caddick-Adams anajadili kutofungama na upande wowote kutakuwa na maana gani kwa Ukraine na anatathimi uzoefu wa nchi nnyingine katika historia ambazo zilichukua mwelekeo huo.
Dunia inavitazama vita vya Ukraine kwa hofu vita vya Ukraine na Urusi. Kila siku vinagarimu maisha mapya ya watu, mara nyingi watu wasio na hatia, ambao hawawezi kujilinda wenyewe huku nyumba zao zikigeuzwa kuwa vumbi
Ujumbe kutoka Urusi uko wazi: 'Fanya kama tunavyosema , la sivyo tutawafanya muumie vibaya zaidi '.
Uchokozi wa Shirikisho la Urusi pia umeelekezwa kwa dunia kwa ujumla,ikidai iache kuingilia kati.
Zelensky, mwigizaji ambaye aligeuka kuwa rais anacheza mchezo wa maisha, ni mwanaume mwenye akili.
Ni mchezo ambao umefunikwa na kuikonga mioyo ya wengi duniani, lakini pia wa kuboresha mikakati kwa ajili ya amani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Karata moja aliyoiweka mezani ni kumaliza majaribio ya Ukraine ya kujiunga na muungano wa NATO.
Badala yake, ameangazia kuhusu kamali ya Kiev kuwa mjumbe wa Muungano wa Ulaya,ambao utaipa usalama, lakini zaidi faida za kiuchumi.
Ukraine na EU
Tarehe 28, 2022, Zelensky aliomba rasmi kujiunga na uanachama wa Muungano wa Uaya na machi 11, baada ya saa tano za mjadala mkali, Baraza la EU lilipiga kura kwa wingi wa kura kuidhinisha nchi hiyo " kuwa na ushirikiano na Ulaya ".
Kuwa mjumbe ajaye wa EU lakini sio wa NATO, hali ya Ukraine itakuwa saw ana ile ya nchi kama Cyprus, Austria, Finland, Ireland, Malta na Sweden.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kisiwa cha Cyprus kimegawanyika baina ya Jamuhuri ya Cyprus, kikisaidiwa na Ugiriki na Jamuhuri ya Uturuki ya kaskazini mwa Cyprus, ikisaidiwa na Turkey.
Kutokana na ukweli kwamba imesalia kuwa maeneo mawili tofauti, kila moja likiwa chini ya mshirika tofauti wa NATO (Ugiriki na Uturuki), inakuwa vigumu kujiunga siku zijazo na muungano wa NATO.
Wakati huo huo Austria, Finland, Ireland, Malta and Sweden, zinajiona kama nchi zisizofungamana na upande wowote kwa njia tofauti.
Kutofungamana na upande wowote inamaanisha kuwa nchi haina ushirika wa kijeshi na wengine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutokuwa na mafungamano yoyote kwa Austria kulikubaliwa na dola nne zilizochukua mamlaka baada ya Vita vya pili vya dunia ( Muungano wa Usovieti, Marekani, uingereza na Ufaransa ) wakati walipoondoka mwaka 1955, Pamoja na Austria yenyewe.
Inalizuwia taifa kuingia ndani ya miungano ya kijeshi au kuruhusu ngome za kijeshi kwenye ardhi yake

Chanzo cha picha, Getty Images
Sweden ni nchi nyingine ya Ulaya yenye utamaduni wa muda mrefu wa kutokuwa na uhusiano wa kijeshi na upande wowote.
Ilitokana na sera ya jeshi lake ya kutofungamana na upande wowote katika nusu ya karne ya 19 , baada ya kuwa na nguvu za kijeshi kwa muda mrefu katika Baltic na ikatangazwa rasmi mwaka 1834.
Sawa na Uswizi, imebuni dhana ya "kutokuwa na mafungamano yoyote ya kijeshi" kulinda hadhi yake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya Finland kuunga mkono Wanazi wa Ujerumani dhidi ya Muungano wa Usovieti , makubaliano ya silaha yalisainiwa mwaka 1944 , na ukawa mkataba kamili wa urafiki, ushirikiano na usaidizi wa pamoja baina ya Muungano wa Usovieti na Finland wa mwaka 1948.
Mkataba ule ulizuia kila upande kujiunga na muungano wa kijeshi dhidi ya upande mwingine: Finland haiwezi kuruhusu eneo lake kutumiwa kwa shambulio dhdii ya Urusi.
Inaweza kuigarimu kiasi gani Ukraine kutofungamana na upande?
Kutokuw ana mafungamano yoyote kwa Ukraine kwa siku zijazo kunaweza labda kuwa na misingi ya makubaliano ya kimataifa, kama yake yaliyobuniwa na Uswizi au Austria, na kuongeza kipengele cha kujilinda iwapo itavamiwa, kama vile yanavyofanya mataifa ya Sweden na Finland.
Nje ya NATO, Sweden imetangaza hivi karibuni ongezeko la matumizi ya yake ya sekta ya ulinzi kutoka 1.3% ya pato lake la ndani hadi 2% "haraka iwezekanavyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hatahivyo, Sweden na finland kwa pamoja sasa zinatathmini upya mienendo yao juu ya kujiunga na NATO, huku maoni ya umma katika nchi zote mbili yakionyesha kuwa wengi wanaunga mkono sana nchi zao zijiunge na Muungano huo.
Uchokozi wa urusi nchini Ukraine umechochea ushindani wa silaha katika Ulaya ambao haujawahi kushuhudiwa tangu mwaka 1914 .
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine












