Katiba mpya 2025 yaibua hisia tofauti Tanzania

Kumekuwa na hisia tofauti kufuatia maoni yaliyotolewa leo na kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini Tanzania kupendekeza kwa Rais wa taifa hilo Samia Suluhu Hassan, mchakato wa katiba mpya uanze baada ya uchaguzi wa 2025.
Kupitia mitandao ya kijaamii, baadhi ya wanasiasa, wanaharaki na wanaNchi wa kawaida wamekuwa na mtazamo tofauti.
Daniel Kamwela kupitia mtandao wake wa twitter akichanfgia maoni ya mwanaharakati Maria Sarungi, ameonyesha kutokukubaliana na maoni ya kikosi kazi hicho
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Katibu wa chama cha NRA, Kisabya anasema, Rais kukubali tu kusikiliza maoni ya wadau wa siasa kupitia kikosi kazi hicho chenye wajumbe wa kada mbalimbali ni hatua kubwa kujenga siasa imara, kwa hivyo kamati kupendekezo mwaka 2025 kuanza mchakato wa katiba, ni ridhio lisilo la shaka.
"Kitendo cha wao (kikosi kazi) kupendekeza hivyo, kuna nia njema, na kama kuna nia njema lazima ifuate na maoni mema… kama rais amelikubali, na wamesema tutoe ushauri, hilo ni jema", alisema na kuongeza " muhimu tusifanye jambo la harakaha halafu halafu tukakwama".
Akiwasilisha maoni hayo ya wadau mbele ya Rais Samia Suluhu, mwenyekiti wa kikosi kazi hiyo Profesa Rwekaza Mkandala ametoa sababu kuu nne zilizofanya kikosi kazi hicho kupendekeza mchakato huo kuanzwa baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Sababu ya kwanza aliyoitaja Profesa huyo ni uwepo wa haja ya kuainisha dira mpya ya maendeleo ya 2063 itakayotoa muelekeo wa katiba mpya na suala la kukosena kwa muda wa kutosha kuanza kutumia katiba mpya ndani ya kalenda ya uchaguzi wa 2025.
Masuala mengine ni haja ya kutoa fursa kwa marekebisho ya sheria ya uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa pamoja na haja ya kutoa fursa ya kutosha kufanyia kazi masuala ya muda wa kati ikiwa ni pamoja na kuaninisha dira mpya ya maendeleo.
"Changamoto hapa Mheshimiwa rais ni mbili, moja ni kwamba kuna wale ambao wanasema, hakuna haja ya kuwa na katiba mpya, kwani katiba ya sasa inaweza kufanyiwa marekebisho kukidhi mahitaji ya sasa na baadae lakini ya pili kuna wale wanaodai kwamba, mchakato wa kupata katiba pendekezwa haukuwa shirikishi vya kutosha, kwa sababu baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba walisusia, hivyo katiba hiyo kupitishwa na wajumbe waliobaki", alisema Profesa Mukandala.
Kwa upande wake Rais Samia Suluhu ametaka kikosi kazi hicho kulifanyia kazi na kuleta mapendekezo yatakayotangazwa kwa watanzania wote.
"Mimi nakubaliana kwamba, ni jambo la muda mrefu, lakini watanzania wote waelewe hivyo", alisema Rais na kuongeza " lakini kwanza tukayafanyie kazi maboresho yote tuliyoyasema hapa, halafu huko mbele tuone je kuna haja pia ya kurekebisha katiba yetu? Pengine kutakua na haja, sio kuandika mpya, kurekebisha baadhi ya maeneo na hata kama tunaandika mpya, lakini kazi kubwa ishafanywa kwenye maboresho haya ambayo tumeshayafanya, kule ni kwenda kuingiza tu kwenye hiyo katiba, alisema.
Kumekuwa na makelele mengi katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni kuhusu katiba mpya, hasa kutoka kwa vyama vya siasa va upinzani na baadhi ya wanaharakati,
Mwaka 2011 Tanzania ilianza mchakato wa kutunga katiba mpya kwa kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba namba 83 ya 2011.
Hata hivyo mchakato huo uliishia njiani baada ya Oktoba 2014, Bunge maalumu la katiba ambalo makamu wake mwenyekiti wakati huo alikuwa Rais Samia kupiga kura kupitisha katiba inayopendekezwa, ambayo ilipaswa kupigiwa kura ya maoni na wananchi ili kuthibitisha, lakini haikufanyika hivyo mpaka sasa.
Kwa sasa Taifa hilo linatumika katiba ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mara kadhaa, ambayo wanaoikosoa wanaiona haikidhi matakwa mengi, ikiwemo kutoa mamlaka makubwa kwa Rais














