Mtazamo juu ya Ukraine: Kwa nini vita vya Afrika vinaangaziwa tofauti

Person holding up 'Stop War' sign

Chanzo cha picha, AFP

Katika msururu wa barua kutoka kwa waandishi wa Afrika, Mwanahabari wa Algeria mzaliwa wa Canada Maher Mezahi inaakisi namna tofauti tofauti za mizozo ya Ulaya na Afrika inavyotazamwa.

Short presentational grey line

Sisi sote ni sawa, lakini wengine ni sawa zaidi kuliko wengine.

Kauli hii imeangaziwa katika tamthilia ya George Orwell na imejitokeza bayana katika vita vilivyozuka Ulaya mashariki.

Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine umelaaniniwa sana kote duniani. Lakini kwa mtazamo wa Afrika, jinsi mataifa yenye nguvu duniani yavyoungana kukomesha mzozo huo, yamepokelewa kwa hisia mseto.

Kwa upande mmoja, vikwazo na azimio la Umoja wa Mataifa linaeleweka sana kwa sababu hakuna mtu anayetaka vita vitakavyo husisha mataifa yaliyojihami kwa silaha za nyuklia kwani hali itakuwa mbaya zaidi.

Kwa upande mwingine, kumekuwa na mshangao dhahiri katika bara letu kwamba sio migogoro yote ya kivita inapewa umuhimu ikizingatiwa kwamba kumekuwa na mengi barani Afrika.

Ndio, kuna taarifa zinazotolewa na wajumbe wa kimataifa wametumwa kushughulikia masuala hayo lakini, taarifa hizo haziangaziwi moja kwa moja kila siku, wala hakuna taarifa za moja kwa moja kwenye televisheni kutoka viongozi duniani na hakuna wito wa kujitolea kusaidia.

Mamilioni walazimishwa kutoroka

Nchini Ethiopia, miezi 16 iliyopita imekuwa jehanamu.

Kutokana na mzozo wa Tigray kaskazini mwa nchi hiyo, zaidi ya watu milioni mbili wamefurushwa makwao.

Kando na hilo maelfu ya watu wanakabiliwana njaa baada ya serikali kutuhumiwa kwa kuzuia misaada muhimu ya kibinadamu kuwafikia - jambo ambalo inapinga.

Kuna ushahidi kwamba uhalifu wa kivita huenda ilifanywa na pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki na matumizi makubwa ya ubakaji kama silaha ya vita.

Food aid being distributed

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Msafara wa chakula cha ulitatizika kufika Tigray

Na kuna migogoro mingine mingi ambayo haipati kuangaziwa.

Sehemu kubwa ya mwezi Januari nilikuwa Cameroon kwa ajili ya kombe la mataifa bingwa ya Afrika, ambako baadhi ya mechi zilichezwa katika nji wa Limbe, uliopo pembezoni mwa Mlima Cameroon.

Usafiri kuelekea eneo hilo hasa siku ya mechi ulikumbwa na wasiwasi kwa sababiu mashindano hayo yaliendelea licha ya mgogoro kuhusiana na wanamgambo wanaotaka kujitenga

Usalama uliimarishwa.

Kila baada ya kilamita moja au zaidi,

Asubuhi niliyosafiri kwenda kutazama mechi kati ya Tunisia na Mali awamu ya makundi, kulikuwa na makabilianoya risasi kilomita 20 hivi upande wa Buea.

'Vita kamili' nchini Cameroon

Mwanahabari mwenza wa Denmark, Buster Kirchner, aliishi kwa siku kadhaa katika mji huo.

"Maher,vita kamili vinaendelea,"aliniambia kwa mshangao aliporudi.

"Sio mgogoro tu, Niliona hospitali na shule zikiwa zimefungwa. Watu wanateseka sana."

Naam, kuna makala kadhaa kuhusu mizozo ya Ethiopia na Cameroon zilizochapishwa hapa na BBC na katika tovuti nyingine za habari za kimataifa lakini hatukuona ghadhabu tunazoshuhudia sasa

Kwa nini ulimwengu haujaonyesha sehemu ndogo ya wasiwasi ambao umeonyeshwa katika wiki moja iliyopita au zaidi kwa mateso ya Waafrika?

Customers wear protective face masks against the novel coronavirus at a restaurant in Algiers, on August 19, 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Baadhi yao wanaonekana kushangazwa ikiwa watu wa kipato cha kati wanaweza kuwa nchini Algeria

Utangazaji wa vyombo vya habari kuhusu vita nchini Ukraine umefichua kwa nini hali imekuwa hivyo.

Msururu wa kushangaza wa maoni yasiyojali, ikiwa si ya ubaguzi wa rangi kabisa, yalitangazwa na vyombo mbalimbali, ambavyo viko zaidi katika miji mikuu ya Ulaya au Marekani Kaskazini.

Mtangazaji mmoja alistaajabu kuona kwamba wakimbizi kutoka Ukraine walikuwa "watu waliofanikiwa, wa tabaka la kati na sio wakimbizi wanaojaribu kutoroka kutoka maeneo ya Mashariki ya Kati au Afrika Kaskazini".

Hilo lilinigusa - nchi zilizostawi zaidi ambazo nimekuwa zote zilikuwa Mashariki ya Kati.

Dai lingine la kipuuzi lilitangazwa kwenye televisheni ya Ufaransa, wakati mchambuzi alipohoji kwamba Waukraine walikuwa sawa na Wafaransa kwa sababu "wanaendesha magari sawa na sisi"

Maher Mezahi
Why is it impossible for some to imagine that Africans could drive a nice car? And why are we all required to have a position on Ukraine?
Maher Mezahi
Journalist
1px transparent line

Nikiangalia Algeria, na maeneo mengine nimwehi kufika katik akanda hiyo, najiuliza: "Kwani sisi sio sawa na Waukraine?"

Nilipofanya utafiti wa haraka nilithibitisha kuwa Ukraine na Algeria zina viashiria sawa vya maendeleo ya kiuchumi na binadamu.

Nchi zote mbili zina idadi ya watu zaidi ya milioni 40; Ukraine ni ya 55 duniani katika pato la taifa, Algeria iko katika nafasi ya 58; Ukraine inashika nafasi ya 22 katika jeshi lenye nguvu na Algeria inashika nafasi ya 31.

Sasa kwa nini mtu alisema kwamba Waukraine walikuwa "mafanikio" zaidi au wana watu wa "tabaka la kati" kuliko Waafrika Kaskazini?

Kwa nini ni vigumu kufikiria kuwa Waafrika wanaweza kuendesha gari nzuri? nchi Algeria, tunaendesha magarisawa na yale yanayoendeshwa na watu nchini Ufaransa.

Na kwa nini tunatakiwa kuwa na msimamo kuhusu Ukraine na si juu ya migogoro ya Cameroon au Ethiopia?

Binadamu ni binadamu, na vita ni vita iwe Kyiv, London, Bogota au Buea.

Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi