Putin na Macron wazungumza tena kwa simu

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron walizungumza tena kwa simu Jumapili, katika simu iliyochukua saa moja na dakika 45, ofisi ya rais wa Ufaransa inasema.
Bado hatujapewa maelezo ya kile kilichojadiliwa. Viongozi hao walizungumza kwa njia ya simu siku ya Alhamisi, katika mazungumzo ambayo yalimwacha Macron na hisia kwamba lengo la Putin lilikuwa kuchukua Ukraine nzima, kulingana na afisa wa Ufaransa.
Macron ni mmoja wa viongozi kadhaa wa dunia ambao wamezungumza na Putin siku za hivi karibuni wakitumai kukomesha mapigano nchini Ukraine.
Mapema Jumapili, Putin alizungumza na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye aliomba kusitishwa kwa haraka kwa uhasama.
Kulingana na msomaji wa Kremlin wa wito huo, Putin alimwambia Erdogan kwamba wapatanishi wa Ukraine wanapaswa kuzingatia "mbinu ya kujenga" zaidi katika mazungumzo, "kwa kuzingatia kikamilifu ukweli unaojitokeza".
"Ilisisitizwa kuwa kusimamishwa kwa operesheni hiyo maalum kunawezekana tu ikiwa Kyiv itasimamisha shughuli za kijeshi na kutekeleza matakwa ya Urusi," ilisema Kremlin. Urusi imekuwa ikiita uvamizi wake "oparesheni maalum".
- Urusi na Ukraine: No-fly zone-Inacho maanisha na kwanini nchi za magharibi haziwezi kuchukua hatua
- Urusi na Ukraine: Nini kitatokea ikiwa Urusi itadhibiti maeneo yote ya Ukraine?
- Ukraine ilitoka vipi kuwa nchi ya tatu kwa nguvu za nyuklia duniani hadi hali yake ya sasa







