Mzozo wa Ukraine: Unazijua hati fungani za vita, namna gani zitaisaidia Ukraine kukabiliana na mshambulizi ya Urusi?

Wanajeshi

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukiendelea, serikali ya Volodymyr Zelensky inakimbizana na muda ikiangalia namna ya kuviwezesha kwa silaha vikosi vyake vya kijeshi na ulinzi wenye gharama kubwa wa nchi yake.

Hali ni ngumu: baada ya uwekezaji mkubwa na kisasa wa nguvu za kijeshi za Urusi, Waukraine wanazidiwa katika silaha na katika idadi ya askari, bila kuangalia uwezo wa Ukraine kwenye silaha za anga, ambao uko chini ukilinganisha na Urusi.

Kwa kuongezea, uchumi wake umedorora kutokana na vita, na uwezo mdogo wa makusanyo na kupanda kwa bei ya bidhaa kama vile mafuta.

Katika muktadha huo, Wizara ya Fedha ya Ukraine ilitangaza wiki hii kwamba watageukia njia za zamani za kifedha ili kusaidia vikosi vyao: kinachojulikana kama "dhamana za kivita" au hati fungani za kivita.

"Wakati huu wa uchokozi wa kijeshi wa Shirikisho la Urusi, Wizara ya Fedha inaruhusu raia wa kigeni, makampuni na wawekezaji kusaidia bajeti ya Ukraine kwa kuwekeza katika "dhamana za serikali za kijeshi," wizara hiyo ilielezea kupitia akaunti yake ya Twitter.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Kwa mujibu wa Serikali ya Zelensky, kila dhamana au hati fungani itakuwa na thamani ya fedha ya Ukraine, hryvnias 1,000 sawa na dola $ 33) na kiwango cha riba "kitaamuliwa katika mnada."

"Mapato kutokana na dhamana hizo yatatumika kukidhi mahitaji ya Majeshi ya Ukraine," aliongeza.

Katika mkutano na wawekezaji wa kigeni, rasilimali zake zilitoa pia ishara za uhakikisho kwa soko, kwamba haitashindwa kushughulika na madeni yao yaliyopo.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wawekezaji wana wasiwasi kwamba uvamizi wa Urusi utaishinikiza Kiev kuacha kulipa madeni yake. Kwa sababu hiyo hiyo, katika siku za hivi karibuni kumekuwa na kushuka kwa kasi kwa bei za hati fungani nchini Ukraine.

Kukabiliwa na hali hii ngumu, "hati fungani za vita" vinaonekana kuwa njia nzuri ya (angalau,) kufadhili ulinzi wao. Chanzo hicho cha fedha - kilichoanza kutumika Jumanne - kilifanikiwa kukusanya takriban dola milioni 270 kwa siku moja.

Lakini hati fungani hizi ni kitu gani na wakati gani vimetumika katika historia ya hivi karibuni?

Maana yake nini?

Hati fungani za vita, sawa tu na hati fungani zingine za kukabiliana na madeni - ni nyenzo inayotumiwa na serikali kukopa fedha kutoka kwa umma mfano wawekezaji (binafsi au taasisi), ambayo itayarudisha madeni hayo katika kipindi fulani ikiambatana na riba.

Katika mazingira haya, fedha zitokanazo na hati fungani za vita hutumika kufadhili shughuli za kijeshi katika kipindi cha vita.

Kifaru

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika hili, fedha hizi hutumiwa hasa kufadhili shughuli za kijeshi wakati wa vita.

Kwa kawaida, zoezi hili la ukusanyaji wa fedha hulipa kiwango cha chini cha wastani na kwa asilimia kubwa kina hatari kwa sababu, ikiwa nchi itashindwa vita, inawezekana pia na pesa zilizowekezwa 'zikaenda na maji'.

Hivyo, kawaida wananchi ama wawekezaji huwekeza fedha zao kwenye njia hii kwa sababu ya uzalendo wao na hisia zao kutaka kusaidia katika ulinzi wa nchi.

Ukraine, kwa mfano, imetoa wito wa watu kuunga mkono taifa lao "katika nyakati ngumu."

Hati fungani za vita pia ni njia ya kudhibiti mfumuko wa bei kwa kuchukua pesa kutoka kwenye mzunguko kuchochea uchumi katikati ya vita.

Ni nyakati gani nyingine katika historia njia hii imetumika?

Hii si mara ya kwanza katika historia njia hii ya kupata fedha imetumika kusaidia jeshi la nchi fulani wakati wa vita.

Marekani pia ilitoa dhamana kama hizo kufadhili baadhi ya matumizi ya ulinzi wake wakati wa Vita Kuu ya Kwanza na ya pili ya Dunia.

Propaganda

Chanzo cha picha, Getty Images

Kati ya mwaka 1917 na 1918, serikali ya Marekani ilitoa kile kinachojulikana kama "Hati fungani za Uhuru," na kufanya kampeni kubwa ili kutangaza dhamana hizo kwa wito wa kizalendo. Kampeni hiyo ilihusisha wasanii maarufu, ikiwemo Charles Chaplin na mwigizaji Ethel Barrymore.

Leo inaaminika kuwa chanjo hicho cha fedha kilikuwa muhimu kwa ajili ya kutafuta fedha katika ulinzi wa nchi.

Mwaka 1940, historia ilijirudia.

Ingawa uwezekano wa kukusanya kodi kwa ajili ya kufadhili Vikosi vya Jeshi ulifanyiwa tathmini, hati fungani hatimaye zilitumika tena - wakati huu ziliitwa "Hati fungani za Vita" au "Hati fungani za Ushindi" - baada ya shambulio la Japan la Pearl Habour mnamo 1941.

Uingereza ilitoa hati fungani za vita mwaka 1917

Chanzo cha picha, Getty Images

Maneno mengi ya propaganda ya kuvutia uwekezaji huu yalisomeka: "Ikiwa huwezi kupigana, unaweza kusaidia nchi yako kwa kuwekeza kama vile unawekeza 5% kwenye dhamana ya serikali ... Tofauti na mwanajeshi, mwekezaji hawi kwenye hatari yoyote."

Vyombo vya habari vya nchi hiyo pia vilijiunga kupigia debe njia hiyo ya ukusanyaji fedha

Wakati huo, gazeti la kisiasa la Uingereza The Spectator liliandika: "Ni watu wa Uingereza ambao lazima watoe fedha za kusaidia vita."

Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi