Je wajua miti huwasiliana na kusogea kisiri?

Chanzo cha picha, Getty Images
Takriban miaka bilioni 4.5 iliyopita, ardhi ya sayari yetu ilikuwa tasa na isiyo na uhai.
Ilichukua miaka nyingine bilioni 2 kwa viumbe wa kwanza wenye seli moja kuonekana baharini.
Mimea inayoundwa na seli nyingi imekuwepo kwa karibu miaka milioni 800. Ili kuishi duniani, mimea ilipaswa kujilinda kutokana na mionzi na kuwa na mbegu ambazo zingeiruhusu kutawanyika kwa upana zaidi.
Ubunifu huu uliisaidia mimea kuwa moja ya mifumo ya maisha yenye ushawishi mkubwa kwenye sayari. Leo hii inapatikana katika mifumo yote mikuu ya ikolojia, na wanasayansi wanaelezea zaidi ya mimea aina mpya 2,000 kila mwaka.
Makala ya David Attenborough The Green Planet, inaangazia mimea na uwezo wao wa kututia moyo. Katika mfano mmoja tu wa hivi majuzi, wahandisi wamefanikiwa kunakili umbo la mbegu za maple yenye mabawa ili kubuni mitambo mipya ya upepo.
Mimea ina siri nyingi ambazo wanasayansi bado hawajagundua. Lakini hapa kuna uvumbuzi tano ambao ulitusaidia kuona binamu zetu wa kijani kibichi kwa njia mpya.
1. Mimea "huzungumza" kati yao
Ni bayana kuwa mimea haina sauti, hivyo haiwezi kuzungumza kama sisi. Lakini hutumia ishara za kemikali na elektroniki kuratibu majibu kwa mazingira yao.
Wakati seli za mimea zinaharibiwa, kama nyasi iliyokatwa na mashine ya kukata nyasi, hutoa vipande vya protini vinavyoweza kutambuliwa na mimea iliyo karibu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni kama mfumo wa uangalizi: wakati mmea umeharibiwa, mingine inaarifiwa kuwa kuna hatari karibu. Hii inaweza kusababisha majibu ya kinga au ulinzi mwingine.
Vile vile, mimea inaweza kugundua wasambaza mbegu katika maeneo yao na kutoa kemikali ili kuwavutia. Ishara hizi hufanya mimea kuwa na mawasiliano magumu kuelewa.
2. Mimea inaweza kusogea
Katika kitabu chake cha mwisho " The Power of Movement in Plants ", kilichochapishwa mwaka wa 1880, Charles Darwin alielezea uwezo wa mimea kuondoka au kusogea mwangaza.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanasayansi huita hii phototropism. Sasa inajulikana kuwa kusonga kwa mimea haiongozwi na mwanga tu, bali pia na maji, virutubisho, na kwa kukabiliana na wanyama wa malisho na ushindani kutoka kwa mimea mingine.
Mimea inaweza kuonekana kukwama mahali iliyokusudiwa kukaa mahali ambapo mbegu zao huota. Lakini kwa kweli, mimea daima hugeuza majani, mizizi, na shina ili kuboresha nafasi zao za kuishi.
Kwa mfano, sehemu za mashina zinazobaki kwenye kivuli hurefuka ili kuhakikisha kwamba mmea hukua kuelekea kwenye mwangaza katika mchakato unaopatanishwa na homoni. Mizizi huonyesha kinyume, na kusonga mbali na mwangaza.
3. Mimea inaweza kukua anga za mbali
Kuvuka anga na kuishi kwenye sayari nyingine ni jambo ambalo binadamu amekuwa akifikiria kwa muda mrefu, lakini sayari nyingine yenye mazingira sawa na dunia bado haijapatikana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tunajua kwamba mimea ni wataalamu wa kurekebisha mazingira ili kukidhi mahitaji ya maisha magumu zaidi. Misitu ya kwanza ilileta na oksijeni na kuondoa CO2, na kuifanya sayari kuwa na uhai.
Je, kukua mimea kwenye sayari za mbali kunaweza kufaa zaidi mahitaji yetu?
Wakati wa mshindani ya anga za mbali kati ya USSR na Marekani katika miaka ya 1950 na 1960, wanasayansi walisoma jinsi mimea inakua angani. Hadi sasa, wataalam wamekuza aina 17 ya mimea tofauti katika vyumba maalum, ikiwa ni pamoja na mahindi, ngano na nyanya.
Kubadilisha sayari ili kuifanya iwe na na uhai bado ni ngumu, lakini maendeleo yote ya sayansi ya mimea katika miaka ya hivi karibuni yanaifanya kuwa lengo linaloweza kufikiwa.
4. Moja kati ya mimea 10 hukua kwenye mmea mwingine
Wanasayansi walianza kuchunguza sehemu za juu za miti kwa kutoa mafunzo kwa nyani au kuajiri wapandaji wataalam kukusanya sampuli. Wengine hata walitumia bunduki kurusha sampuli.

Chanzo cha picha, Getty Images
Haikuwa hadi miaka ya 1980 ambapo utafiti wa juu ya miti ukawa taaluma ya kisayansi inayojitegemea wakikopa mbinu ya kukwea milima.
Inakadiriwa kuwa hadi 80% ya speshi za miti huishi maisha yao yote msituni au juu ya miti.
Na moja kati ya spishi n10 za mimea inayojulikana ya mishipa - spishi zinazotumia vyombo vinavyofanana na mshipa kusafirisha maji na virutubishi kwa mwili wote - hukua juu ya mimea mingine.
Mimea mingi hukua kwenye miti, na mti mmoja unaweza kuhimili aina 50 za miti kwa jina epiphytes. Epiphytes mara nyingi hutoa majani zaidi kuliko mti mwenyeji wao.
5. Mimea inaweza kuonyesha mabadiliko duniani
Viumbe hai vinaweza kutambua mabadiliko katika mazingira yao na mimea haswa imetumiwa kugundua mabadiliko haya kwa karne nyingi. Wakati majani yanapoanza kubadilika rangi , kawaida hutangaza kuwasili kwa miezi ya baridi na giza.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangu miaka ya 1980, viwango vya joto duniani vimekuwa vikiongezeka kama matokeo ya moja kwa moja ya uchomaji wa vitu mfano kaboni, ambayo iliwekwa na mimea mamilioni ya miaka iliyopita wakati wa uundaji wa misitu.
Tunaishi katika wakati wa mabadiliko na kuelewa jinsi mimea inavyoitikia mabadiliko ya hali ya hewa inaweza kutusaidia kujiandaa kwa siku zijazo.













