Kwanini Wanigeria wananunua pakiti ya taulo mbili tu za kike?

Chanzo cha picha, Getty Images
Hakuna mwanamke duniani anayepata hedhi na akatumia taulo za kike mbili tu za kujisitiri.
Pakiti ya kawaida ya taulo nane haitoshi, lakini nchini Nigeria mfuko, au pochi ndogo ya plastiki, iliyo na pedi mbili sasa inauzwa kwa wingi kama chaguo la bei nafuu.
Katika nchi tajiri, mfuko unaweza kuchukuliwa kuwa rahisi, mbadala wa kubebeka, lakini nchini Nigeria unaonekana kama jambo linalogusa zaidi.
Kuonekana kwa taulo hizo katika pakiti hizi ndogo "lilikuwa jambo la kusumbua akili", kulingana na mwanaharakati wa afya ya wanawake Dkt Chioma Nwakanma.
Haziwakilishi urahisi bali ni chaguo gumu zaidi kwani baadhi ya wanawake hawawezi kumudu kugharamia kipindi chao chote.
"Hata ilipokuwa pakiti ya taulo nane wakati mwingine haitoshi, kwa hivyo sasa watu wananunua pakiti hiyo na kuanza kuchagua siku gani ya kuitumia," Dkt Nwakanma aliambia BBC.
"Chaguo jingine ni- tishu na vitambaa - sio safi na ni chafu sana kwa hivyo haiwezekani kufikiria kinachoendelea."
Kuongezeka kwa mifuko hii ya bidhaa muhimu na vyakula vilivyochakatwa nchini Nigeria vinatoa picha halisi kuhusu gharama ya maisha.
Huku mfumuko wa bei wa kila mwaka ukiongezeka kwa asilimia 18 mwezi Machi mwaka jana, na mfumuko wa bei wa chakula ukifikia 23%, kupanda huku kwa gharama ya maisha kumeunda kile kinachoitwa na wengine kama "sachet economy".

Mbali na taulo za kike, kila kitu kutoka chakula cha watoto hadi mafuta ya kupikia hadi nafaka ya kifungua kinywa sasa inaweza kununuliwa kwa sehemu ndogo, ambazo ni nafuu zaidi kwani ongezeko kubwa la bei limezidi kupanda kwa mishahara.
"Nilikuwa nikinunua vitu kwenye katoni ili vidumu kwa muda mrefu zaidi. Sasa nimeanza kununua sacheti yoyote ambayo ni nafuu," Chika Adetoye, ambaye ana wasiwasi wa kumudu chakula cha kutosha kwa ajili ya watoto wake watatu.
Jambo hilo la sachet lilianza kuonekana mwishoni mwa 2020 huku picha zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii za bidhaa ambazo watumiaji waliamini kuwa hazijaonekana kwenye pakiti ndogo hapo awali, pamoja na pombe ya Baileys cream.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Lakini pamoja na bidhaa zilizosindikwa viwandani, kupanda kwa bei pia kumeathiri mazao mapya.
Katika masoko, wafanyabiashara wanasema wanapitisha gharama tu. Hawawezi kukumbuka mara ya mwisho walilazimika kulipa kiasi hiki ili kuhifadhi.
Soko la Oyingbo lenye pilika nyingi huko Lagos ni mahali maaruf kwa biashara, lakini hizo ni ngumu kupata sasa.
Gunia la mboga hizo maarufu kama majani machungu limeongezeka maradufu katika mwaka uliopita, mfanyabiashara Nancy Ike aliambia BBC.
"Vitu ni ghali sana, watu hawawezi kumudu," alisema.
Mnamo mwaka wa 2015, benki kuu ya nchi hiyo ilitoa orodha ya bidhaa 41, ikiwa ni pamoja na mchele, majarini na nyanya.
Wazo lilikuwa kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje na kuhimiza uzalishaji wa ndani. Tangu wakati huo mamlaka imepanua na kurekebisha orodha, na kuongeza uzalishaji wa sukari na ngano Aprili mwaka jana.
'Biashara inataka kuongezewa nguvu'
Mipaka ilifunguliwa tena mnamo Desemba 2020 lakini bado kuna uhaba.
Wakati mahitaji yanapozidi ugavi, nadharia ya msingi ya kiuchumi inaonesha kwamba bei zitapanda.
Wakati huo huo bei za juu zina athari kubwa kwa maisha ya watu. Benki ya Dunia inakadiria kuwa kwa kipimo chake mfumuko wa bei wa hivi majuzi uliwasukuma Wanigeria wengine milioni saba katika umaskini. Idadi ya jumla sasa ni zaidi ya milioni 100 - takriban nusu ya idadi ya watu.
Ongezeko la mfumuko wa bei linaweza kuwa limepita kilele chake, lakini haijulikani lini litashuka hadi viwango vinavyoweza kudhibitiwa zaidi.












