Mwaka mpya 2022: Unabii wa wahubiri wa Nigeria Enoch Adeboye, Oyedepo, Olukoya, katika mwaka 2022

Chanzo cha picha, Facebook @Pastor Adeboye, Oyedepo, Olukoya
Kila mwakaunapoisha wahubiri na 'manabii' wa makanisa mbali mbali wakiwemo kutoka mataifa ya Afrika hutoa maono yao wanayoyaita unabii kuhusu mambo yatakavyokuwa katika mwaka unaofuatia iwe kwa watu binafsi , kwa nchi zao , Afrika na dunia nzima.
Nchini Nigeria viongozi wengi wa kidini wameanza kutoa unabii wao kwa ajili yam waka 2022 kama seheu ya utaratibu wao wa kila mwaka.
Unabii wa mwaka 2022 una misingi ya yale ambayo wachungaji na wahubiri wamekuwa wakiyabashiri kutokea katika mwaka 2022 wakati watu wakiupokea mwaka mpya. Baadhi nchini Nigeria wameanza kusaka taarifa za unabii wa wahubiri na viongozi wao wa kidini.
Wanigeria wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu mara kwa mara kujua ni nini wachungaji wao watakachokisema katika jumbe zao za unabii kuhusu mwaka mpya.
Na mwaka hu mambo hayakuwa tofauti kwani wamekuwa wakiwatarajia watoe unabii wao. Na huu ni baadhi ya ujumbe kama ulivyotolewa na wahubiri, wachungaji na manabii kuuhusu mwaka 2022
Unabii wa mchungaji Enoch Adeboye

Chanzo cha picha, Facebook @pastor E.A Adeboye
Mkuu wa Kanisa la Wakristo la Mungu- Christian Church of God, RCCG, Pastor Enoch Adeboye al maarufu Daddy G.O ametoa unabii kumuhusu yeye binafsi, Nigeria na mataifa ya kigeni.
Redeemed Christian Church of God linadaiwa kuwa ndio kanisa kubwa zaidi nchini Nigeria.
Alichokisema kumuhusu yeye binafsi
- "Zaidi ya 80% ya miradi yake itakayoanzishwa 2022."
- "Mwaka huu utakuwa mwaka wa kujitokeza kwa nyota ambazo hazikuwahi kuonekana kabla."
- "Kwa yoyote yatakayofanyika, mwaka huu utakuwa mwakwa wa mafanikio (ya kisayansi na kifedha) ."
- "Viwango vya vifo vya watoto wachanga vitapungua kwa 50%."
Kuihusu Nigeria
- "Hautatengeneza mayai ya kukaangwa bila kupasua mayai ."Alisema Mchungaji katika unabii wake.
Kuhusu mabara
"Suala la uhamiaji litakuwa na mabadiliko mapya katika mwaka mpya ."
"Vimbunga vikali viwili (kimoja kikitoka Atlantic na kingine kikongine kutoka Pacific) vitatokea wasipovizuwia, athari zake zitakuwa ni mbaya sanana za kutisha ."
Unabii wa David Oyedepo 2022

Chanzo cha picha, Facebook @david Oyedepo
Askofu David Oyedepo wa kanisa la Imani inayoish- Living Faith Church pia alikuwa miongoni mwa viongozi wa kidini waliotoa unabii wao kwa ajili ya mwaka 2022.
Oyedepo alitoa unabii uliokuwa na mada : Maazimio ya unabii na yalikuwa ni zaidi ni kuhusu watu binafsi, unabii alioutoa kupitia ukurasa wake wa Twitter.
David Oyedepo anasema "mwaka huu wa 2022 utakuwa ni mwaka wa kutoa shukran kwa watu majumbani mwao n ani mwaka utakao kuwa tofauti kwa maisha ya watu ."
Pia amezungumziakuhus wazazi kufurahia matunda ya kazi yao, nyumba zilizovunjika zitarejeshwa tena na mengine.
Unabii wa Mchungaji mkuu wa kanisa la Mlima wa Moto -Mountain of Fire -Daniel Olukoya 2022

Chanzo cha picha, Facebook @Daniel Olukoya
Mkuu wa kanisa la Mountain of Fire na kanisa la miujiza , Dkt. Daniel Olukoya ametoa vipengele 37 vya unabii kwa ajili ya mwaka 2022 na baadhi yake vinahitaji,
- "Maombi ili kuwaepuka marafiki wanafiki wa mataifa yanayokataa kufikia makubaliano na kusalitiana na kuingia vitani."
- "Kusali dhidi ya kuporomoka kwa uchumi na njaa kali ."
- "Kusali dhidi ya kuyumba kwa siasa ambako kutawafanya watu wengi wakanganyikiwe ."
- "Kuomba dhidi ya vifo vya ajabu visivyojulikana.
- "Kanisa linahitaji maombi dhidi ya kuongezeka kw amauaji ya Wakristo ."
Unabii wa mwaka mpya kwa Nigeria na Afrika
Kwa miaka mingi , kutolewa jwa unabii wa wahubiri wa injili kwa ajili ya Nigeria na katika baadhi ya maeneo ya Afrika limekuwa ni jambo lililozoweleka kila wanapovuka mwaka.
Hatahivyo wakosoaji wanasema baadhi ya unabii ni ubashiri tu kwa misingi ya mambo ambayo yatatokea kabla ya mwaka mpya.
Wakati huo huo wakosoaji wengine wanasema viongozi wa kidini hawakuweza kubashiri mapema baadhi ya mambo ambayo yanatokea mwaka ujao, kwa mfano janga la Covid-19.












