Covid-19: Vita vigumu dhidi ya tabia ya kutema mate nchini India

Chanzo cha picha, Getty Images
Mapema mwaka huu, Raja na Priti Narasimhan walianza safari ya barabarani kote nchini India wakiwa na ujumbe mmoja: acha kutema mate hadharani. Wawili hao walibeba kipaza sauti na kutangaza ujumbe wao kutoka ndani ya gari lililokuwa na maandishi ya kupinga kutema mate.
Iwapo umeishi nchini India, unaweza kuelewa ni kipi wawili hao wanapinga. Mate kila mahali barabarani, wakati mwingine ni kohozi, wakati mwingine damu nyekundu kutokana na kutafuna tumbaku, utaona hayo hata kwenye kuta za majengo makubwa . Hata inatishia daraja la kihistoria la howrah jijini Kolkata.
Kwa hivyo wawili hao husafiri nchi nzima, kwa lengo la kulinda mitaa na majengo yake na madaraja kutoka kwa watema mate. Wanaishi katika jiji la Pune, na wamejitolea kupinga tabia ty kutema mate tangu 2010. Wameshiriki kwenye kampeni za mitandaoni na nje ya mtandao, jitihada za kusafisha na manispaa za mitaa yote hayo wamefanya.
Majibu kwa jitihada zao yametofautiana kuanzia kutojali hadi hasira. Bwana Narasimhan anakumbuka mtu mmoja aliyemuuliza: "Tatizo lako ni lini? Ni mali ya baba yako?"
Lakini janga la Covid-19 ambalo liliikumbaa India limebadilisha mambo kadhaa, Bi Narasimhan anasema baadhi ya watema mate wameomba msamaha.
"Hofu ya janga hilo imewafanya wafikirie," anasema.
Nchi ya kutema mate'
Vita nchini India dhidi ya kutema mate kwenye mitaa yake vimekuwa vya nusu nusu. Jiji la Mumbai limejaribu zaidi, na kunao wakaguzi wa hiari ambao hukemea watu wasiteme mate, kutupa takataka au kwenda haja ndogo hadharani. Lakini kosa la kutema mate kwa muda mrefu limepuuzwa kwa kiasi kikubwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kisha ikaja Covid, hatari yake ya kusambaa kwa njia ya hewa na tabia za wanaume wa India kutema mate popote wanapochagua. Maafisda wakachukua hatua, wakiwaadhibu watema mate kwa faini kubwa na hata viifungo jela, yote hayo chini ya sheria za kudhibiti majanga. Hata Waziri Mkuu Narendra Modi aliwashauri watu kutotema mate katika maeneo ya umma.
Hii ilikuwa tofauti sana na mwaka 2016, wakati waziri wa afya akijibu swali kuhusu tabia hiyo ya kutema mate ambapo aliliambia bunge: " India ni nchi inayotema mate. Tunatema mate tunapochoka, tunatema mate tunapokasirika au tunatema mate hivyo tu. Tunatema mate popote na kila mahali na tunatema mate wakati wote na saa zisizo za kawaida."
Na tabia hiyo sana ni ya wanaume. Wanaume Wahindi wanastarehe za miili yao, ana sema mwandishi Santosh Desai, "na kila kitu kinachotoka mwilini mwao".
"Kuna urahisi wa kujisaidia hadharani," anasema. "Ikiwa sina raha, nitachukua hatua mara moja, wazo la kujizuia halipo kabisa."

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini kwa nini kutema mate hadharani?
Bw Narasimhan anasema amegundua kuwa sababu ni tofauti kuanzia hasira hadi "kupitisha muda tu" (hawana kitu bora cha kufanya), au kwa sababu tu wanaweza - "wanahisi ni haki yao ya kutema mate", anasema.
Baadhi ya wanahistoria wanaamini kwamba tabia hii inaweza kutokana na Hindu nadhana za juu za kudumisha usafi wa mwili kwa kutoa chochote kichafu.
Vita dhidi ya kutema mate
Inatokea kwamba kulikuwa na wakati watu walikuwa wakitema mate kila mahali. Nchini India, kutema mate kulisherehekewa katika makazi ya kifalme.
Barani Ulaya katika zama za kati, ungeweza kutema mate wakati wa chakula, kama ilikuwa chini ya meza.
Mkaguzi wa afya huko Massachusetts, alipouliza mwaka wa 1908 kwa nini mafundi cherehani walitema mate sakafuni katika kila kiwanda alichotembelea, alijibiwa, "Bila shaka wanatema mate sakafuni; unatarajia wateme wapi, katika mifuko yao?"

Chanzo cha picha, Getty Images
Ilikuwa ni sababu ya kuenea kwa ugonjwa wa kifua kikuu ndiko kulileta pigo kwa tabia hiyo katika nchi za Magharibi. Uelewa mwishoni mwa Karne ya19 hadi mapema Karne ya 20 ulichukua jukumu muhimu, anasema mwandishi wa habari Vidya Krishnan, mwandishi wa kitabu kinachokuja cha Phantom Plague: How Tuberculosis Shaped History.
"Ufahamu wa jinsi vijidudu vinavyoenea ulileta desturi mpya za kijamii. Watu walijifunza kuzuia chafya na vikohozi, kukataa kusalimiana kwa mikono, na kumbusu mtoto ni tabia iliyochukiwa.
Bi Krishnan anasema kuongezeka ufahamu huo kulisababisha "mabadiliko ya tabia" miongoni mwa wanaume, kwa kuwa walikuwa ni wao na bado ndio wenye tabia ya kutema mate hadharani katika kiwango ambacho husababisha magonjwa ya kuambukiza kama kifua kikuu kuenea".
Lakini India inakumbwa na vizingiti vingi, Bi Krishnan anasema. Majimbo yake hayajajaribu sana kukomesha tabia hiyo. Na kutema mate bado kunakubalika kijamii - iwe ni tumbaku ya kutafuna, wanamichezo wanaotema mate kwenye kamera au filamu za Bollywood za wanaume wakitema mate huku wakipigana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wataalamu wa afya wameonya kwamba kuwaadhibu tu watu, bila kujaribu kuelewa kwa nini wanatema mate, hakutashinda vita dhidi ya tabia hiyo.
Na miaka miwili ya janga la Covid-19, bidii ya kupambana uraibu huu inapungua. Lakini Raja na Priti Narasimhan hawajakata tamaa katika vita vyao vya mitaani.
Watu wengi bado hawajui inaweza kuchangia kuenea kwa Covid-19, wanasema - na hilo ni jambo ambalo wanaweza kubadilisha kidogo.












