Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Siku ambayo 'Carlos the Jackal" na wenzie 5 walivamia makao makuu ya OPEC na kuteka watu zaidi ya 60
Walibeba mabegi makubwa ya michezo mabegani mwao. Walikuwa wanaume watano na mwanamke mmoja, wakiwa wamevalia makoti mazito wakitokea kwenye ghorofa lililokuwa karibu kabisa na katikati ya mji wa Vienna.
Ilikuwa asubuhi yenye baridi. Joto la juu zaidi ambalo lingerekodiwa katika mji mkuu wa Austria siku hiyo lingekuwa zaidi ya nyuzi joto moja.
Walipanda treni ya mwendo kasi iliyokuwa na watu wachache, ingawa walitoa tahadhari kwa abiria wengine kuwa ilikuwa safari ya kawaida.
Walishuka na kutembea hadi makao makuu ya Shirika la Nchi Zinazouza Mafuta duniani (OPEC), ambako viongozi wao walikuwa wanakutana.
Polisi kijana aliyekuwa mlangoni mwa jengo hilo aliwaona wakiingia ndani kulikuwa na makumi ya watu wakiingia, wakiwemo mawaziri, wajumbe, wakalimani na waandishi wa habari waliokuja tangu siku iliyopita.
Ilikuwa ni mida ya takriban saa 11:30 asubuhi siku ya Disemba 21, 1975, siku ambapo OPEC inaiita " sura yenye giza zaidi katika historia yake ."
Baada ya dakika chache, kundi lililokuwa limeingia tu kwenye jengo hilo la ghorofa nane likaacha historia kama mwanahistoria wa Austria Thomas Riegler alivyoiambia BBC.
Kwenye usukani alikuwa kijana wa miaka 26, mwenye sifa za raia wa Amerika Kusini, akiwa amevalia kofia ya duara aina ya bereti.
Huyu ni Ilich Ramírez Sánchez, anayejulikana zaidi kama "Carlos the Jackal."
Risasi
Katika makao makuu ya OPEC mawaziri na wajumbe wa mafuta kutoka Algeria, Ecuador, Gabon, Indonesia, Iran, Iraq, Kuwait, Libya, Nigeria, Qatar, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Venezuela walikutana hapo.
Baadhi ya waandishi wa habari 30 walikuwa wametumwa kuripoti mkutano huo ambao uliibua msisimko mkubwa kimataifa na wengine walikuwa kwenye ukumbi wakati wavamizi hao wakiulizia kuhusu chumba cha mkutano.
"Walionekana kuwa sehemu ya wajumbe wa OPEC. Hakuna aliyewajali sana," aliandika mwandishi wa habari Clyde H. Farnsworth katika makala yake kwenye gazeti la New York Times iliyochapishwa siku moja baadaye.
"Waandishi wa habari waliwaelekeza wote sita kwenye ngazi iliyoelekea kwenye ghorofa ya pili, ambapo katika muda wa saa mbili mawaziri wengi walikuwa wamefika."
Dakika moja baadae milio ya risasi ilianza kusikika kwenye ghorafa hiyo ya pili
"Carlos na wenzake waliingia upande wa mapokezi, wakafyatua risasi za onyo kwenye dari na kuwaongoza watu kwenye chumba cha mikutano, ambako mkutano wa mawaziri ulikuwa unafanyika," anasema Riegler.
Mtafiti ndiye mwandishi wa kitabu cha 'The terrible day: OPEC hostage-taking in 1975 and the beginning of modern terrorism' mwaka 1975 na sura ya When modern terrorism began kutoka kitabu cha OPEC and the Global Energy Order.
Washambuliaji
Kilichokuwa kikitokea kwenye ghorofa ile ya pili ni utekaji nyara.
Kundi la watu sita likiongozwa na "Carlos the Jackal", kwa msaada wa bunduki ndogo ndogo, mabomu ya kutupa kwa mkono na vifaa vingine walivyobeba kwenye mabegi waliyokuwa nayo na mengine kufichwa kwenye makoti yao, walikuwa wamewashikilia watu takriban watu 60.
Kilijiita jeshi la Mapinduzi ya Kiarabu na kuhalalisha hatua yake likisema kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikuwa karibu kutambua "uhalali wa kuwepo Wayahudi katika ardhi ya Palestina."
Kulingana na Riegler, washambuliaji hao sita walifuata uongozi wa Wadi Haddad, "ambaye alikuwa kiongozi wa Palestina katika mapinduzi.
Zaidi ya sababu ya Palestina
Kulingana na mtaalamu huyo, "kwa kiasi kikubwa, utekaji nyara wa OPEC ulikuwa ni matokeo ya mapambano ya kuwania madaraka ndani ya shirika lenyewe."
Anasema kuwa aliyekuwa anawaunga mkono alikuwa na Muammar Gaddafi wa Libya ambaye alitaka mabadiliko katika sera ya bei ya shirika hilo na kutumia kundi la Haddad kama nguvu ya kuwashinikiza wapinzani wake wakuu ambao ni Saudi Arabia na Iran na huenda kulikuwa na msaada zaidi kutoka Algeria na Iraq".
Muktadha wa kimataifa
Athari za vyombo vya habari vya kimataifa kutokana na ufyatuaji risasi huo zilikuwa kubwa sana.
"Hatua hiyo ilikuwa ya umuhimu mkubwa kwa sababu uchumi wa dunia ulikuwa katika mgogoro kutokana na ongezeko kubwa la bei ya mafuta," alisema José Toro Hardy, mkurugenzi wa zamani wa Petroleos de Venezuela inayomilikiwa na serikali ya Venezuela (PDVSA).
Na hiyo ndio kwamba kati ya 1973 na 1974 zuio la usambazaji wa mafuta lililowekwa na nchi za Kiarabu lilitokea na kusababisha shida ya nishati.
Hatua hiyo, ambayo pia ilijumuisha kupunguzwa kwa uzalishaji, ilitaka kuweka shinikizo kwa nchi za Magharibi ambazo ziliunga mkono Israeli katika vita vya Yom Kippur mwishoni mwa 1973, lakini ilirefushwa kwa miezi kadhaa baada ya kumalizika kwa mzozo huo.
Vifo
Klein moja wa washambuliaji alikuwa ameagizwa kuangalia yeyote aliyekuwa kwenye mapokezi ili kuhakikisha hakuna mtu aliyekuwa na silaha.
Kijana wa i mapokezi Edith Heller alijificha nyuma ya meza yake na akaweza kupiga simu polisi "Ni OPEC. Wanapiga risasi kila mahali"
Klein aliona, akamkimbilia na kumuelekezea bastola yake.
Heller alihisi kana kwamba kichwa chake kilikuwa kimelipuka, baada ya kusogezewa bastola, alifyatua risasi kwenye kifaa cha sikio alichokuwa ameshikilia
Polisi wawili walikuwa zamu katika vituo vya OPEC ambao ni Anton Tichler na Josef Janda, ambapo, kulingana na Riegler, hawakupinga chochote, hawakuvaa sare au kuwa na redio.
Josef Janda alifanikiwa kupiga simu kuomba msaada, kisha akaificha bunduki yake kwenye droo ya meza na kuchanganyika na mateka.
Polisi mwenzie Tichler alikimbilia kwenye lifti, lakini hakuweza kujiokoa .
ilikuwa kifo cha kwanza kati ya vifo vitatu. Wengine wawili walikuwa mlinzi wa usalama wa Iraqi na mwanauchumi wa Libya.
Walichohitaji
Washambuliaji walikuwa wamedhibiti mahali hapo, kuanzia mida ya 11:50 asubuhi kikosi cha polisi wanane kutoka kitengo cha dharura kilifanikiwa kuingia.
Lakini hawakuwa na mafunzo maalumu na kiongozi wake alijeruhiwa kwa risasi, alikuwa mmoja wa watu kadhaa waliojeruhiwa katika shambulio hilo.
Klein, akiwa naJusuf walikuwa wamejiweka kwenye chumba cha kushawishi ili kuzuia hatua zozote za mamlaka, alijeruhiwa kwenye tumbo.
Watekaji nyara watano waliosalia walitumia ofisi ya maafisa wa Iraq huko Vienna, Riyadh al Azzawi, kama mpatanishi katika mazungumzo yao na serikali ya Austria.
"Waambie kwamba ninatoka Venezuela na kwamba jina langu ni Carlos. Waambie kwamba mimi ni Carlos maarufu. Wananijua," Ramírez alimwambia una nusu saa"
Mnamo 2003, Yamani alielezea kwa BBC sehemu ya uzoefu wake na Ramírez:
Alasiri walituma taarifa yao kwa serikali ya Austria na kusema: ' taarifa zetu zisipo tangazwa kwenye redio saa 4:00 (usiku), tutamuua Yamani na kutupa maiti yake barabarani.'
" Aliniambia. Saa 4:00 hawakutoa taarifa hizo na hivyo 'Una nusu saa.'" alisema Yamani
Nilimuuliza ikiwa naweza kuandika wosia wangu na nikaanza kuufanya
Dakika ishirini baada ya 4:00, alikuja na kunigusa. Nilimwona, nilitazama saa yangu na nikasema, 'Nimebakisha dakika 10.' Nilikuwa nikijadiliana.
Na akaniambia: 'Hapana, una zaidi ya hayo kwa sababu wanaeneza taarifa zetu zetu.'
Mamlaka
Riegler anasema kwamba asubuhi ya Desemba 21 Bruno Kreisky, Kansela wa Austria, alikuwa amefika mahali ambapo angesherekea likizo yake ya Krismasi lakini aligeuza baada ya kusikia tukio hilo la dharula.
Foillan anabainisha kuwa Kreisky alipokea barua kutoka kwa kundi la mateka wakitaka matakwa ya wateka nyara yatimizwe na kueleza nia yao ya kuondoka Austria pamoja nao.
Kulingana na Riegler, afisa huyo alikuwa katika mawasiliano ya karibu na mabalozi wa nchi za OPEC na akawaomba ridhaa yao katika hatua nyeti zaidi za mazungumzo.
"Ili kulisha timu yake na mateka, ambao walikuwa hawajala tangu asubuhi, Carlos aliomba sandwichi mia moja na matunda," Foillan anasema.
Wenye mamlaka walisafirisha bidhaa hizo, lakini baadhi ya sandwichi hizo zilikuwa na nyama ya nguruwe, chakula ambacho Waislamu hawali kwa sababu za kidini.
"Carlos alikataa shehena hiyo na badala yake akaagiza kuku na kukaanga."
Matokeo
Riegler anasema Saa 8:45 asubuhi mnamo Desemba 22, 1975, msafara uliokuwa umewabeba magaidi hao na mateka 33 waliosalia, wakiwemo mawaziri 11 wa mafuta, ulifika katika uwanja wa ndege wa Schwechat anasema Riegler.
Ramírez na kundi lake waliamua kwamba ndege ingeenda Algeria.
Klein alihamishwa kwenye gari la wagonjwa na aliongozana na daktari katika safari yote ya ndege.
Riegler anakumbuka kwamba mara tu upangaji wa mateka na washambuliaji ulipokamilika, "Carlos alimfuat Waziri wa Mambo ya Ndani wa wakati huo, Otto Rosch, ili kuaga.
Kreisky alisema maamuzi hayo yamefanywa kutokana na hofu mateka wangeweza kuuliwa.
Kwa hiyo ndege ilibidi irejee Algiers, ambako utekaji nyara ulimalizika Desemba 23, 1975, baada ya mazungumzo ya moja kwa moja na Bouteflika.
Watekaji nyara hao walitoroka na vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa kiasi kikubwa cha fedha kilitolewa ili kuwaachilia huru mateka hao.
Klein alihukumiwa kifungo cha miaka tisa jela nchini Ujerumani mwaka 2001
Katika kesi yake alimhusisha Gaddafi akidai Walibya walitoa hata taarifa za usalama wa eneo la mkutano.
Mnamo 1994, Ramírez alikamatwa nchini Sudan na kupelekwa Ufaransa, ambako amefungwa vifungo vitatu vya maisha kwa mfululizo wa mashambulizi katika miaka ya 1970 na 1980 lakini utekaji nyara wa OPEC hausiki na vifungo hivyo.