Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita nchini Ethiopia: Jinsi Waziri Mkuu Abiy alivyoongoza vita kuwasukuma nyuma waasi
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliibua kumbukumbu ya wafalme wa nchi hiyo kwa kwenda mstari wa mbele kuongoza vita dhidi ya waasi wa Tigray ambao walikuwa wametishia kumpindua.
Katika hali ambayo kwa mwanamume aliyetangazwa mshindi wa 100 wa tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2019, Bw Abiy alipigwa picha na kurekodiwa video akiwa katika sare za jeshi akitembea vichakani na sehemu zenye milima, akitazama kwa kutumia daribuni na kuwahutubia wanajeshi chini ya miti.
"Wale wanaotaka kuwa miongoni mwa watototo wa Ethiopia, watakaokumbukwa na historia, simameni na kutetea nchi yenu leo, tukutane mstari wa mbele," alisema
Kjetil Tronvoll, profesa wa masuala ya mizozo chuo cha Oslo New Unieversity College nchini Norway, alisema hakuna shaka kuwa uamuzi wa Bw Abiy ulisaidia kugeuza wimbi dhidi ya vikosi vya TPLF.
"Licha ya kwamba picha zilionyesha kuwaa likuwa karibu na mstari wa mbele na wala sio mbele kabisa, uamuzi wake ulizaa matunda," alisema.
"Uliwaongezea motisha majenerali wake, kuibua utaifa, ukachangia mashujaa kama Haile Gebrselassie kujitokeza kuunga mkono jitihada za vita na maelfu ya watu wakajitoza kujiunga na jeshi na makundi yanye siliha kutoka eneo la Amhara."
Mashambulizi kwa kutumia ndege zisizo na rubani.
Mapigo yaliyoikumba TPLF ni makubwa. Wapiganaji wke walikuwa karibu na mji wa Debre Birhan, karibu kilomita 130 kutoka mji mkuu Addis Ababa, kabla ya kusukumwa nyuma karibu umbali wa kilomita 400 kwenda Weldiya. Inamaanisha waasi walipoteza miji muhimu ya baraara ya A2 inayounganisha ngome ya huko Tigray na mji mkuu.
Prof Tronvoll alisema kuwa wakati Bw Abiy aliongozo vikosi vyake ardhini, ndege zisizo na rubani zilizoripotiwa kununuliwa kutoka China, Utuki na Iran, zilitekeleza wajibu mkubwa katika kuwasukuma nyuma TPLF. Ndege isiyokuwa na rubani ya China ya Wing Loong II ilitajawa kuwa yenye uwezo mkubwa wa kushambulia vifaru, mizinga na kuangusha makomu dhidi ya wanajeshi walio ardhini.
Wakati huo huo, serikali ilikataa shinikizo kutoka Marekani na Muungano wa Ulaya kufanya mazungumzo na kuzitaja nchi za magharibi kama washirika wa TPLF, mtazamo ambao pia uliungwa mkono na Bw Gebrselassie mwanariadha wa zamani wa Ethiopia.
"Tumeona vile Iraq, Syria, Yemen na Libya zimeharibiwa au kusambaratishwa. Lakini Ethiopia ni nchi ya watu million 120. Kwa hivyo jitihada zozote za kuivuruga nchi zitawarudia," alivimbia viombo vya habari vya serikali.
Umaarufu waongezeka
Mwezi Novemba Bw Abiy alifananish jitihada za TPLF za kuipindua serikali yake na wavamizi wa Italia walioshindwa kwenye vita vya Adwa mwaka 1896 na jeshi la Emperor Manelik II, muasisi wa Ethiopia ya sasa aliyetokea kabila la Amhara.
TPLF lilikuwa vuguvugu la msituni lililoingia madarakani nchini Ethiopia mwaka 1991. Lilitawala hadi mwaka 2018 wakati Bw Abiy aliingia madarakani kufuatia maandamano makubwa kupinga utawala wake dhalimu. Kisha likarudi ngome yake huko Tigray na kutoka huko likaanza uasi mwaka uliopita kufuatia tofauti kubwa na Bw Abiy juu ya mageuzi yake.
Mchambuzi Abdurahman Sayed anasema Bw Abiy alijizolea heshima kubwa kutoka kwa Waethiopia wengi kwa kweda mstari wa mbele kupigana vita kuwa kuwa umaarufu wake ulikuwa ukididimia wakati waasi walikuwa wakisonga mbele.
"Kwa kuondoka makazi yake rasmi na kujiunga na jeshi, Bw Abiy alituma ujumbe kuwa alikuwa amejianda kufa kwa ajili ya Ethiopia ikiwa itawezekana," alisema
"Anavutiwa sana na historia wa wafalme wa Ethiopia na wakati mmoja alisema mama yake alitabiri kuwa atakuja kuwa mfalme wa saba. Wafalme walikuwa wakiongoza wanajeshi wao kwenda vitani, na amefanya kitu sawa na hicho."
Prof Tronvoll anasema vitendo vya Bw Abiy havikustahili kwa mshindi wa tuzo ya amani, tuzo aliyopewa mwaka 2019 kwa kumaliza ukatili na Eritrea na kuleta mageuzi ya kisiasa nchini Ethiopia baada ya miongo ya ukandamzaji.
Vita vya barabara muhimu
Bw Abiy alijiunga na vita mwishoni mwa mwezi Novemba ambapo vikosi maalum na makundi yaliyojihami kutoka eneo la Afar walikuwa wamesababisha maafa makubwa kwa TPLF.
Jamii ya Afar ambao ni majirani wa Tigray, kitamaduni wanatajwa kuwa wapiganaji. Karibu kila mwanamune kutoka jamii ya Afar anastahili kuwa na bunduki kutoka umri wa miaka 15.
Waligeuka kuwa pingamizi kubwa kwa TPL na kwa mara ya kwanza wanawake wa Afar walijiunga na vita, alisema Bw Abdulrahman.
"Ilionyesha kiwango cha chuki dhidi ya TPLF kutokana na ukatilia wapiganjai wake walisababisha huko Afar wakati walijaribu kuvuka kutoka Tigray karibu miezi sita iliyopita"
Bw Abdurahman anataja hili kama hatua kubwa kwe mabadliako vitani, kwa sababu iliwazuia TPLF kufika kwenye mpaka na Djibouti. Ethiopia ni nchi iziyo na bandari na bandari ya Djiboiti ni muhimu zaidi kwa uchumi wake.
"Iwapo TPLF wangechukua udhibiti wa bandari kuu kwenda mpakani. Uchumi wa Ethiopia ungeporomoka , hakuna bidhaa zingefika Addis Ababa na uwezekano wa mji mkuu kuingia mikononi mwa Tigriya ungekuwa mkubwa."
Bw Abiy alirudi kutoka mstari wa mbele baada ya karibu wiki mbili, lakini ofisi yake ikatangaza wiki hii kuwa amerejea tena kuongoza jeshi katika kuyateka maeneo zaidi eneo la Amara. Kwa upande wake TPLF ilisema iliutwaa mji wa kihistoria wa Lalibela.
Bw Abdurrahman anasema Bw Abiy hakuwa na lingine ila kupigana vita kuwa kuwa TPLF walikuwa na lengo la kupata tena madaraka kwa kutumia nguvu.