Je wadudu wana hisia kuliko vile wanavyoonekana?

Chanzo cha picha, Alamy
Siku moja tulivu mwaka 2014, David Reynolds alisimama kuzungumza kwenye mkutano muhimu. Ulikuwa ukifanyika kwenye ukumbi wa mjini Chicago - Ukumbi mzuri sana, umepambwa kwa ngazi za marumaru, nguzo za zamani za futi 75 na dari zilizoinuliwa.
Kama mtu anayesimamia udhibiti wa wadudu katika majengo ya umma ya jiji mingoni mwa mambo mengine, Reynolds alikuwa huko kuzungumzia kuhusu bajeti yake ya mwaka .
Lakini kabla ya kuanza kuzungumza, kitu kikaonekana kwenye ukuta, mende mweusi akaonekana akitembea juu ya ukuta mweupe.
Ni kama alikuwa anamdhihaki
"Kamishina wa bajeti yako ni gani kwa mwende? Diwani mmoja akakatiza hotuba kulingana na ripoti kwenye jarida la The Chicago Tribune. Kukawa vicheko na watu kukimbia kumtokomeza yule mende.
Hakuna mtu aliweza kuhoji uwepo wa yule mende pale, japo ilikuwa kwa bahati mbaya. Lakiani kisa hicho ni cha kuchekesha kwa sababu tunawachukulia wadudu kama roboti.
Kuna ushahidi kuwa wadudu wanaweza kuwa na hisia kiwango fulani. Wanaweza kuwa wenye furaha yanapotokea mambo mazuri ya ya ghafla au wanaweza kukumbwa na huzuni wakati vitu vibaya vinafanyika. Wanaweza kuogopa au kujibu maumivu sawa na wanyama wengine.
Scott Waddell, profesa katika chuo cha Oxford anasema kuwa baadhi ya utafiti umepata kuwa wadudu humakinika juu ya kile wenzao wanafanya na wana uwezo wa kujifunza. Nchini Uingereza havi majuzi serikali ilitambua kuwa kaa na kamba wana hisia na kupendekeza iwepo sheria ya kuwapiga marufuku watu kuwachemsha wakiwa hai
Kwa hivyo ni ka njia gani mtu hutambua hisia kwenye mdudu? Tunaweza kujua kuwa hawaitikii moja kwa moja? Na kama wao ni viumbe nyeti, tunaweza kuwatendea tofauti?

Chanzo cha picha, Alamy
Sharti la mageuzi
Wadudu wako katika kundi la viumbe wenye miguu sita walio na miili iliyogawanyika. Wako aina ya zaidi ya milioni moja wakiwemo kereng'ende, nondo, mende, nyuki, vipepeo na hata chawa wa kichwa.
Wadudu wana viungo vingi sawa na vya wanadamu - moyo, ubongo, matumbo na vingine vingi lakini wadudu hawana mapafu na tumbo. Na badala ya kuwa na mishiba ya damu, viungo vya miili yao huelea kwa mchuzi wa aina fulani ambao husafirisha chakula na kuondoa uchafu.
Licha ya ubongo wa wadudu kubadlika kwa namna sawa na ya wanadamu kuna tofauti kubwa. Wakati ule wa mwanadamu ni mkubwa na unatumia asilimia 20 nguvu za mwili, ule wa wadudu ni mdogo mara milioni kadhaa ya ule wa wanadamu.
Hisia ni kama program ya mnyama kana kwamba ikiwakishwa inaweza kubadilisha kile tunafanya. Inaaminika kuwa hisia tofauti zimeibuka wakati tofauti katika historia ya mabadiliko lakini kwa kiwango kikubwa zilituwezesha kuwa na tabia kwa njia ambazo zitaboresha uwezo wetu wa kuishi au kuzalisha.
Geraldine Write, profesa katika chuo cha Oxford anatoa mfano wa njaa ambao ni hali ya akili inayokusaida ufanye uamuzi ulio wa busara kama ule wa kutafuta chakula.

Chanzo cha picha, Alamy
Wazo la Uzushi
Wakati Waddell alianzisha utafiti wake kwanza mwaka 2001, alikuwa na lengo moja akilini. Alikuwa anataka kujua ikiwa nzi ni bora katika kukumbuka mahala pa kupata chakula wakati hawajala kwa muda.
Waddell kwa uangalifu aliamua kutumia neno motisha badala ya njaa kuelezea hali ya akili ya nzia - akisema kuwa walipata motisha ya kupata chakula ikiwa chakula hicho kimefichwa suala ambalo huwaletea watu matatizo.
Kwa wanadamu wale wamepitia kiwewe huwa wako tayari kukumbana na hali mbaya na ilo limeonekana miongoni mwa wanyama kadhaa wakiwemo panya, kondoo, mbwa na hata ng'ombe. Lakini hakuna ye kufikia kungalia iwapo wadudu wana tabia kama hiyo.
Kwanza watafiti walifunza nyuki kuhusisha aina fulani ya harufu kwa zawadi ya sukari na wegine kwa maji yenye ladha mbaya.
Kisha wanasayansi wakagawana kwa makundi mawili. Kundi moja lilitikiswa kwa nguvu hisia ambayo nyuki wanaichukia kuwa tayari kushambulia adui. Kundi la pili la nyuki likaachwa kufurahia kinywaji kile cha sukari.

Chanzo cha picha, Alamy
Kufahamu iwapo hali hiyo iliathiri hisia za nyuki, Wright aliwaweka nyuki wale kwenye harufu tofauti. Wale waliokuwa na wakati mzuri walionesha ishara ya kuitisha kinywaji kingine kitamu. Lakini nyuki walikuwa wamekasirika hawakuonesha ishara kama hiyo.
Ukweli usio wa kufurahisha
Maisha ya ndani ya wadudu mara nyingi huwa ni ya uchungu.
Kuna ushahidi mwingi na hata kwa mabuu kuwa huwa wanahisi uchungu - tukiwabana wanajaribu kutoroka na pia hata kwa wadudu waliokomaa. Kama kawaida ni ishara kuwa hali hii isiyo ya kawaida huwa inachukuliwa kama uchungu wa hisia.
Kuna ushahidi kuwa wadudu kwa uhakika wanaweza kuhisi uchungu vile tunavyojua na sio hivyo tu, wanaweza kuhisi uchungu mwingi sawa na wanadamu.
Kidokezo kimoja nikuwa ikiwa utawafunza wadudu kulinganisha harufu fulani na kitu kisicho kizuri, waanweza kutoroka wakati watakapotambua harufu hiyo.
Wakati wadudu fulani wanapozuiwa kutoka huwa wanakata tama na kuonyesha tabia sawa na huzuni.

Chanzo cha picha, Alamy
Swali na namba
Kwa sasa wadudu ndio wanyama wanaoteswa zaidi duniani wakiuawa wengi zaidi. Hawa ni pamoja na wadudu quadrillioni 3.5 wanauawa kwa sumu kwenye mashamba ya Marekani kila mwaka.
Wadudu trilioni mbili wanakanyagwa na magari kwenye barabara za Uholanzi na wengine ambao idadi yao haijulikani.
Licha ya kuwa hakuna data kamaii kuhusu athari za dawa za kuua wadudu, kitu kimoja kinakubaliwa sana - idadi ya wadudu tunaowaua ni wengi.
Tunaishia katika kipindi ambacho idadi kubwa ya wadudu wanatoweka kwa kasi ya juu. Robo tatu ya wadudu wanaoruka nchini Ujerumani wametoweka katika kipindi cha miaka 25 iliyopita na ripoti moja iligundua kuwa familia 400,000 huenda zikatoweka kabisa.
Kuna wito wa dunia nzima wa kupiga marufuku dawa za kuua wadudu ili kulinda wadudu fulani kama hatua iliyochukuliwa Ulaya ya EU-wide embargo ya kulinda nyuki.












