Kuanzia Bill Gates hadi Oprah Winfrey na wengine-Hivi ndivyo matajiri wa dunia wanasababisha uchafuzi wa hali ya hewa

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwaka 2018 Stefan Gössling na kikosi chake walitumia miezi kadhaa kukagua mitandao ya kijamii ya watu matajiri na mashuhuri, kuanzia kwa Paris Hilton hadi Oprah Winfrey.
Profesa huyo wa masuala ya utalii kutoka chuo cha Linnaeus nchini Sweden alikuwa akitafuta ushahidi kuhusu ni mara ngapi wao husafiri kwa ndege.
Jibu ni mara nyingi. Bill Gates, mmoja wa watetezi wakuu wa mazingira alisafiri kwa kutumia ndege mara 59 mwaka 2017 ambazo ni jumla ya kilomita 343, 500, mara 8 zaidi kama angeizunguka dunia, safari zilizozalisha tani 1600 za gesi chafu sawa na gesi waliyozalisha watu 105 nchini Marekani kwa mwaka.
Lengo lake Gössling's ni kujaribu kuelewa matumizi binafsi ya watu matajiri ambao mara nyingi maisha yao yana usiri.
Miongo michache iliyopita imeweka wazi kutokuwepo usawa duniani. Tangu utokee mdororo wa uchumi mwaka 2008 hadi janga la sasa na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa, majanga yanaedelea kuwakumba kwa kiwango kikubwa watu maskini .
Lakini mijadala kuhusu namna ya kutatua kutokuwepo usawa kwenye matumizi mara nyingi hupuuzwa.
Takwimu ni za kushangaza. Asilimia 10 ya watu matajiri zaidi dunaini, walichangia karibu nusu ya gesi chafu duniani mwaka 2015 kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2020 kutoka Oxfam na taasisi ya mazingira ya Stockholm.

Chanzo cha picha, Getty Images
Asilimia moja ya matajiri duniani walichangia asilimia 15 ya gesi chafu ikiwa ni mara mbili zaidi ya asilimia 50 ya watu maskini zaidi duniani ambao wamechangia asilimia 7 tu na ndio waathiriwa zaidi wa mabadiliko ya hali ya hewa licha ya kuchangia kiwango kidogo sana katika mabadiliko hayo.
Dario Kenner mwandishi kwa jarida la Carbon Inequality:
Wajibu wa matajiri kwenye mabadiliko ya hali ya hewa, alibuni jina wasomi wa uchafuzi, kuwalezea watu matajiri katika jamii ambao wanawekeza sana kwenye mafuta ya kisukuku na pia kuchangia athari mbaya kwa hali ya hewa kutokana na mitindo yao ya maisha inayochangia uzalishaji mkubwa wa kaboni.
Jinsi mambo yalivyo, watu wengi kwenye nchi tajiri wanaishi maisha yanayochochea mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa mfano wakati unaangalia gesi chafu kutoka kwa bidhaa zinazoagizwa, mtu anayeishi nchini Uingereza huchangia tani 8.5 za gesi ya kaboni kwa mwaka, kiwango ambacho kinapanda hadi tani 14.2 nchini Canada.
Ili dunia iweze kusalia katika viwango vya nyuzi joto 1.5, viwango vya gesi vinastahili kushuka kwa tani 0.7 kwa kila mtu ifikapo mwaka 2050.
Matumizi ya mtu binafsi ni suala lililoo mwiba kulijadili. Linaweza kwa haraka kupoteza mwelekeo na kuwa iwapo mabadadiliko ya hali ya hewa yanahusu vitendo vya watu binafsi au mabadiliko ya mifumo kutoka kwa serikali na makampuni.
"Watu matajiri walionyesha mfano wa matumzi ambao kila mtu anaenzi na ana nia ya kuyatimiza. Hapo ndipo mathara yapo," anasema Halina Szejnwald Brown, profesa wa masuala ya mazingira katika chuo cha Clark nchini Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa mfano usafiri wa ndege. "Mara unaposafiri kwa ndege unaingia kundi la wasomi duniani," anasema Gössling. Zaidi ya asilimia 90 ya watu hawajasafiri kwa ndege na asilimia 1 ya watu duniani wamechangia asilimia 50 ya gesi chafu kutokana na usafiri wa ndege.
Magari ya SUV yanayosafirisha marais, wafanyabiashara na watu mashuhuri na famailia za utajiri wa wastani mijini, pia nayo yamekuwa ishata ya maisha ya mafanikio licha ya athari zilizopo kwa mazingira. Yakiwa na mauzo ya asilimia 42 kote duniani mwaka 2019 magari ya SUV yalikuwa ndio sekta iliyosababisha kuongezeka kwa gesi chafu mwaka 2020. Kuongezeka ununuzi wa magari ya SUV mwaka uliopita kulifuta mafanikio yaliyokuwa yamefikiwa kutokana na magari yanayotumia umeme.
Barani Ulaya karibu asilimia 11 ya gesi chafu kutoka manyumbani ilitoka kwa asilimia 1 ya wazalishaji wanaomiliki nyumba kubwa na kadhaa.
Miaka michache iliyopita hata hivyo, mitindo ya maisha imeanza kubadilika. Nchini Sweden wanaharakati wa Thunberg walisaidia kuchochea kile kinaitwa flyqskam (ikimaanisha aibu ya usafiri wa ndege) suala lililosababisha watu kuhoji ni mara ngapi wanaweza kusafiri kwa ndege. Vuguvugu hili lilihusishwa na kupungua kwa asilimia 4 ya watu wanaosafiri kwa ndege kwenye viwanja wa ndege nchini Sweden mwaka 2018 - jambo lisilo la kawaida lililoshuhudiwa wakati ambapo abiria walikuwa wanaongezeka kote duniani.
Janga la covid 19 lilipunguza kwa haraka usafiri na kuonyesha kuwa simu za video zinaweza kupunguza mikutano ya ana kwa ana. Utafiti wa shirika la Bloomberg unaonyesha kuwa asilimia 84 ya biashara zina mipango ya kupunguza bajeti za usafiri wa kikazi baada ya janga la corona.
Watu pia wameanza kuzingatia athari za lishe zao na kuchangia kuongezeka kwa nyama itokanayo na mimea.
Lakini mabadiliko ni ya taratibu sama kwa dharura tuliyo nayo.
Ushuru kwa mienendo mibaya, kama usafiri wa ndege wa mara kwa mara na ulaji nyama kupita kiasi vitasaidia kuwageuza watu kuiga tabia zinazalisha kiwango cha chini cha kaboni kwa haraka, haswa wakati kuna uhusiano wa moja kwa moja kwa kuwaadhibu wanaochafua hewa na uwekezaji unaowanufaisha wengi.
Sera nyingine inayopata umaarufu ni kitu kinaitwa Choice editing, ambapo serikali zinazuia vifaa vinayozalisha gesi nyingi ya kaboni kwa mfano ndege za kibinafsi na kujengwa mashua kubwa.
Choice editing au kufanyiwa maamuzi si jambo geni. Serikali ya Uingereza kwa mfano hutumia mbinu hii kuhakikisha usalama wa umma kupiga marufuku uuzaji wa bunduki na magari yasiyo na mikanda ya usalama.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini kwa sera zote zinazolenga mienendo ya watumiaji, kawaida huwa vigumu kupunguza gesi chafu ikiwa miundo msingi haipo kuwawezesha watu kuishi maisha yanayozalisha kiwango cha chini cha kaboni.
Kuna mengi yanahitajika katika kuwa na jamii yenye malrngo ya kudumu na inavuka masuala yanayohusu kupunguza ndege za kibinafsi na mashua za kifahari.
Baadhi ya serikali zinafanya mabadiliko makubwa. Serikali ya Wales kwa mfano imezuwia uwekezaji kwenye ujenzi wa barabara mpya kutimiza viwango vya uzalishaji, Uholanzi imependekeza kupungua idadi ya mifugo kwa asilimia 30 kuzuia uchafuzi na serika za miji nchini Uingereza kama Norwich na Exeter wameanza kujenga nyumba zinazotumia kiwango kidogo cha nishati.
Wengine wamelenga wajibu wa matangazo ya biashara yanayochangia kuongezeka matumizi.
Watu hujaribu kujiweka katika nafasi fukani katika jamii kwa kujigawa kutoka wale walio chini yao, anasema Brwon, Mwaka 2021 Amsterdam ailipiga marufuku matangazo ya bidhaa zinazlsha gesi chafu ikiwemo magari ya SUV na safari fuoi za ndege na kufuata nyayo za mji kama São Paulo na Chennai ambao wamepiga marufuku au kupunguza matanagazo ya biashara kwa kutumia mabango.
Serikali na matajiri, kwa wajibu wao ulio mkubwa kwa kushawishi mienendo katika jamii pia wanaweza kusaidia kubadili fikra kuwa mabadiliko ya hewa inahusu kupoteza uhuru na ubora wa maisha. Lakuhuzunisha kuhusu hili ni kuwa masuala ambayo yameonekana kuwa ya umuhimu kwa mazingira ndiyo bora kwa maisha yetu na mshikamano wetu kijamii.
Kuounguza ulaji nyama ina manufaa kwa afya, Uwepo na magari machache ya SUV na yale yanayotumia mafuta, huongeza ubora wa hewa na kupunguza vifo vinavyotona na uchafuzi wa hewa,
'Hakuna meenye ataamka asubuhi aseme , "Ninaenda kuharibu mazingira, watu hula kwa sababu nyingi, kuhitimiza mahitaji yao, kuhisi vizuri kwa sababu wanahisi kusukumwa kufanya hivyo kupitia matangazo ya biashara au matarajio ya kijamii.
'Ni watu wachache sana wanaketi na kujiuliza swali kuhusu matumizi yao,' anasema Brown: Mimi ni nani na kipi nahitaji kufanya kuishi maisha mazuri?' Ni watu wangapi wanataka kuketi chini na kujiuliza swali kama hilo?"
Hatua za kibinafsi hazitoshi kutatua tatizo la mabadilko ya hali ya hewa, anasema Akenji, na pia kujitia hatiani na aibu havitasaidia. Lakini tunalochagua na vitendo ndio muhimu. Nafikiri zote tunastahili kuwa wanaharakati wa siasa kwa njia moja au nyingine" anasema. Tunachoenda kufanya ni kuuliza serikali zetu kutekeleza ahadi zao.
















