Uchaguzi Ujerumani: Chama cha mrengo wa kushoto chapata ushindi dhidi ya chama cha Angela Merkel

Uchaguzi Ujerumani

Chama cha kisosholiti cha mrengo wa kushoto nchini Ujerumani SPD kimeshinda kwa kura chache uchaguzi wa kijimbo wa taifa hilo kwaa kukishinda chama cha waziri mkuu anayeondoka madarakani Angela Merkel , kulingana na matokeo ya mapema.

Chama cha SPD kilijipatia asilimia 25.7 za kura , huku chama tawala cha Conservative kikijipatia asilimia 24.1 ya kura hizo.

Chama cha kijani kimejipatia ushindi bora zaidi katika historia ya chama hicho , kikiibuka katika nafasi ya tatu kwa asilimia 14.8 ya kura zilizopigwa.

Muungano sasa utalazimika kuundwa ili kuunda serikali.

Kiongozi wa SDP Olaf Scholz awali alikuwa amesema kwamba chama chake kilikuwa na mamlaka kutawala , wakati kilipoanza kuchukua ushindi.

Mrithi wa Bi Merkel, Armin Laschet, ameapa kuunda serikali, lakini chama chake cha kihafidhina cha CDU kimeshuhudia matokeo mabaya zaidi kuwahi kupata katika historia.

Tangu awali uchaguzi huu haukuwa unatabiriki, na matokeo yake hayatahitimisha ukinzani uliopo.

Muhimu ni kwamba, Kansela anayeondoka madarakani hataondoka hadi muungano utakapoundwa - na hiyo inaweza kusubiri hadi Krismasi.

Moja ya jukumu kubwa la mrithi wake ni kusimamia kwanza uchumi wa Ulaya katika miaka minne ijayo, huku mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni ajenda kuu ya wapiga kura.

Wafuasi wachama cha SPD cha bwana Scholz walimsalimia kwa kufaha, muda mfupi kabla ya chama chake kuongoza ambapo aliwaambia watazamaji wa televisheni kwamba ana jukumu kubwa alilopewa na wapiga kura la kuunda "serikali nzuri, inayojali na sikivu kwa ajili ya wajerumani".

Mpinzani wake wa kihafidhina alijibu mapigo kwa kusema ni suala la kuunda muungano, sio kuhusu "idadi kubwa ya watu". "

Anasema hivi kwa sababu uchaguzi huu hauhusu pande hizo tu kuwania madaraka, vyama viwili muhimu katika hili ni chama cha Kijani na kile cha FDP kinachoungwa mono na wafanyabiashara

Angela Merkel

Ingawa vyama hivi havijafanikiwa, ila kwa pamoja vimefikisha robo ya kura, jambo linalofanya viweze kuwa sehemu muuhimu ya uundwaji wa Serikali ya mseto

Vyama hivi vinaubalika sana na vijana chini ya umri wa miaka 30 lakini inahitaji mbinu za ziada kufanya viweze kufanya kazi pamoja.

Kiongozi wa chama cha Kijani Annalena Baerbock anasema makosa waliyofanya wakati wa mwanzo wa kampeni yamesababisha kushndwa kupata kura nyingi

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Kiongozi wa chama cha Kijani Annalena Baerbock anasema makosa waliyofanya wakati wa mwanzo wa kampeni yamesababisha kushndwa kupata kura nyingi

Kwa hivyo ain ayoyote ya serikali ya mseto, vyama hivi viwili vya Kijani na FDP vinatarajiwa kuwemo.

Mseto unaoiitwa wa taa nyekundu za barabarani utaundwa na rangi za vyama; nyekundu inayovaliwa na (SPD), njano ya (FDP) na kijani - au mseto mwingine ni wa Kijamaica unaounda na rangi nyeusi (CDU), njano (FDP) na kijani.

Hii ni kwa mara ya kwanza Ujerumani huenda ikaunda 'mseto wa njia tatu' tangu miaka ya 1960s, nchi hiyo ikiingia katika zama mpya za siasa.

Mbali na muungano huo wa vyama hivyo vinne, haukuwa usiku mzuri kwa wengine wa mrengo wa kushoto na usio endelevu kwa wa mrengo wa kulia. Die Linke wa mrengo wa kushoto anaweza kujikuta hata bungeni haingii kama matokeo ya mwisho yatakuwa chini ya asilimia 5%.

Matokeo ya mapema

Ingawa kura za chama cha mrengo wa kulia cha AfD zinaonekana kupungua safari hii, kinaonekana kuwa na nguvu katika maeneo ya mashariki ya majimbo ya Saxony na Thuringia.