Hali ilivyo wakati wa kujifungua chini ya utawala wa Taliban

Afghan mother and baby with doctor, illustration

Rabia amembeba mtoto wake mchanga, siku chache tu baada ya kujifungua katika hospitali ndogo mkoa wa Nangarhar mashariki mwa Afghanistan.

"Huyu ni mtoto wangu wa tatu, lakini nilichopitia kilikuwa tofauti kabisa. Ulikuwa uzoefu mbaya," anasema.

Katika kipindi cha wiki chache, kitengo cha kuzaa, Rabia alichojifungua mtoto wake, kilikuwa kimebadilika na kukosa hata huduma za msingi tu.

Hakupewa dawa ya kupunguza maumivu, hakupewa dawa wala chakula.

Hospitali ilikuwa na kiwango cha juu cha joto kilichofikia nyuzijoto 43 za selsiasi (109F) - umeme ulikuwa umekatwa na hakukuwa na mafuta ya kuwezesha jenereta kufanya kazi.

"Tulikuwa tukitoa jasho kama tunaoga, " anasema mkunga wa Rabia, tunayempa jina la Abida, ambaye alifanya kazi bila kuchoka gizani kumzaa mtoto wake kwa kutumia taa ya simu ya rununu.

"Ilikuwa ni moja ya uzoefu mbaya zaidi niliyowahi kupitia katika kazi yangu. Ilikuwa uchungu sana. Lakini hii ndio kazi yetu kila usiku na kila siku hospitalini tangu Taliban ichukue madaraka."

Kufanikiwa kijifungua kunamaanisha Rabia ni moja wapo ya wenye bahati.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Afghanistan ni mojawapo ya nchi yenye idadi kubwa ya vifo vya akina mama na watoto wachanga duniani, na wanawake 638 wanafariki dunia kwa uzazi kati ya 10,000 wanaokuwa hai.

Hata hivyo, hali inaendelea kuwa mbaya zaidi.

Pia, maendeleo yaliyofanywa juu ya utunzaji wa mama na mtoto mchanga tangu Marekani kuvamizi nchi hiyo mamo mwaka 2001 yameanza kujitokeza tena kwa haraka sana.

"Sasa kuna haja ya uharaka. Ninahisi uzito wa hilo," anasema mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Natalia Kanem.

Afghan women in burkas, with baby, illustration

UNFPA inakadiria kuwa, bila msaada wa haraka kwa wanawake na wasichana, kunaweza kuwa na vifo vya akina mama vya ziada 51,000, mimba zisizotarajiwa milioni 4.8, na mara mbili ya watu ambao hawataweza kupata huduma za kliniki za uzazi wa mpango kati ya sasa na mwaka 2025.

"Vituo vya afya ya msingi kote Afghanistan vinaporomoka ... kwa bahati mbaya, viwango vya vifo vya akina mama, viwango vya vifo vya watoto vitaongezeka," anasema Dkt. Wahid Majrooh, mkuu wa afya ya umma, ambaye ndiye waziri pekee aliyebaki katika wadhifa huo tangu kuanguka kwa utawala wa serikali mwezi uliopita.

Ameahidi kupigania afya ya Waafghan, lakini anakabiliwa na changamoto si haba.

Taifa hilo limekuwa lililojitenga na ulimwenguni.

Wakati wanajeshi wa kigeni walipoanza kujiondoa, Taliban waliingia madarakani na kulisababisha kusitishwa kwa misaada ya kigeni ambayo inafadhili sana mfumo wa huduma ya afya wa Afghanistan.

Wafadhili wa nchi za Magharibi ni pamoja na Marekani na makundi kama vile WHO, wakitaja ugumu wa kuwasilisha fedha na vifaa vya matibabu kwa Taliban kupitia uwanja wa ndege wa Kabul wenye machafuko.

Upatikanaji wa vifaa vya kuokoa maisha na dawa kwa afya ya uzazi ya wanawake kumeathirika sana.

Hata hivyo, ni bahati mbaya mara mbili kutokana na kuenea kwa virusi vya corona.

"Hakuna maandalizi ya uwezekano wa kukabiliana na wimbi la nne la Covid-19," anasema Dkt. Majrooh.

Katika kitengo cha kuzaa cha Abida, kusitishwa kwa misaada ya kifedha kunamaanisha kuwa hawawezi pia kuendesha huduma ya magari ya kubeba wagonjwa.

Hakuna pesa ya mafuta.

"Siku chache tu zilizopita, mama alikuwa amepata uchungu akiwa karibu kujifungua na aliomba kwa haraka gari la wagonjwa kwasababu ya maumivu mengi. Ilibidi tumwambie atafute teksi, lakini hakuna iliyopatikana."

Hatimaye alipofanikiwa kupata gari, alikuwa tayari amechelewa sana - alijifungua ndani ya gari na akapoteza fahamu kwa saa kadhaa kwasababu ya maumivu makali aliyokuwa nayo na joto kali.

Hatukufikiria angefanikiwa kunusurika.

"Lakini mtoto pia alikuwa katika hali mbaya sana, na hatukuwa na kitu cha kuwafanyia yeyote kati yao," Abida anasema. Kwa bahati nzuri, binti mchanga na mwanamke huyo walinusurika.

Baada ya siku tatu na kupona katika hospitali ambayo haikuwa inapokea ufadhili wowote, mwanamke huyo aliruhusiwa kwenda nyumbani.

"Tunafanya kazi kwa muda mrefu sana, mchana na usiku, ili kutengeneza mfumo huo lakini tunahitaji fedha," anasema Dkt. Kanem wa UNFPA.

Afghan birth centre, illustration

UNFPA inatafuta $ 29.2m (£ 21.1m) kama sehemu ya rufaa ya UN kwa $ 606 milioni kujibu mahitaji ya kuokoa maisha ya wanawake na wasichana wa Afghanistan.

Ni hakika kwamba, kutokana na hitaji kubwa la msaada wa kibinadamu, njia salama itapatikana ya usafirishaji wa bidhaa muhimu za matibabu na huduma za afya na kutoa huduma za kliniki za kutembea sehemu mbalimbali.

UNFPA ina wasiwasi kuwa kuongezeka kwa hatari ya ndoa za utotoni kutazidisha kiwango cha vifo.

Kuzidisha umasikini, wasiwasi juu ya wasichana kutoweza kwenda shule, na hofu juu ya ndoa za kulazimishwa kati ya wanamgambo na wasichana au wale ambao ndio wamebalehe, nako ni tatizo jingine.

Vizuizi vipya vya Taliban kwa wanawake vinalemaza zaidi mfumo dhaifu wa utunzaji wa afya.

Katika maeneo mengi ya Afghanistan, wanawake wanalazimika kufunika nyuso zao na niqab au burka.

Lakini cha kutia wasiwasi zaidi ni ripoti kwamba hospitali na kliniki zinaamriwa kuruhusu wafanyikazi wa kike tu kuwahudumia wagonjwa wa kike.

Mkunga mmoja, ambaye anataka kutotambuliwa, aliambia BBC kwamba daktari wa kiume alikuwa amepigwa na Taliban kwasababu alihudumia mwanamke akiwa peke yake.

Anasema kuwa, katika kituo chake cha matibabu mashariki mwa nchi, "ikiwa mwanamke hawezi kuonekana na daktari wa kike, daktari wa kiume anaweza kumuona tu mgonjwa wakati ambapo watu wengine wawili au zaidi wapo."

Wanawake pia wameamriwa wasiondoke nyumbani bila "mume au jamaa wa kiume."

Mume wangu ni mtu masikini anayefanya kazi ili kuweza kulisha watoto wetu, kwahiyo, kwanini nimuombe aende nami kwenye kituo cha afya? " anasema Zarmina, ambaye ni mjamzito wa miezi mitano katika mkoa wa Nangarhar.

Abida anasema mahitaji ya kuwa na kiongozi wa kiume inamaanisha kwamba, hata kukiwa na mkunga lakini katika kliniki isiyo na rasilimali ya kutosha, wanawake wengi kama Zarmina hawawezi kupata huduma muhimu.

Vivyo hivyo, wafanyikazi wengi wa kike wanaotoa huduma za afya hawawezi kwenda kazini.

WHO inahesabu kuwa kuna madaktari, wauguzi na wakunga 4.6 kwa kila Waafghan 10,000 - karibu mara tano chini ya idadi inayohitajika ikiwa ni "kizingiti kikubwa kwenye suala la wahudumu wa kutosha".

2px presentational grey line

Pia unaweza kusoma zaidi kuhudu Taliban:

2px presentational grey line
Pregnant Afghan woman, illustration

Wafanyakazi wa huduma ya afya ya umma hawajapata mshahara wao kwa angalau miezi mitatu.

Abida ni mmoja wao.

Lakini hata bila mshahara, anatarajia kuendelea kufanya kazi kwa miezi mingine miwili.

"Nimeamua kufanya hivi kwa wagonjwa wetu na kwa watu wetu ... lakini bila ufadhili, sio tu kuwa kunatupa sisi wasiwasi, lakini hata kwa wagonjwa pia. Wao ni maskini sana," anasema.

"Waafghani husikia mengi juu ya majeruhi yanayotokea wakati wa vita. Lakini ni wachache wanaozungumza juu ya wanawake na watoto wangapi wanafariki kutokana na vifo vinavyoweza kuzuilika vinavyohusiana na uzazi," anasema Heather Barr, mkurugenzi mwenza wa idara ya haki za wanawake katika shirika la Human Rights Watch.

Katika ziara ya Kabul mnamo mwezi Mei, anasema hospitali moja ilijaribu kulinda mishahara ya wafanyikazi kwa kupunguza kila kitu.

Wanawake wengi wanaofanyakazi walilazimika kununua vifaa vyao vya kuzalisha.

Mwanamke mmoja alitumia karibu dola 26 kwa vitu kama glavu, maji yanayotumika wakati wa kujifungua na bomba vikiwa mkononi mwake.

Alikuwa ametumia pesa yake ya mwisho na alisisitizwa sana kwasababu ikiwa angehitajika kufanyiwa upasuaji, alipaswa kununua vifaa vyake mwenyewe," Barr anasema.

"Kabla ya Taliban kuingia madarakani, kliniki ya afya ilinigundua kuwa na utapiamlo na upungufu wa damu wakati nilikuwa mjamzito," anasema Lina, 28, ambaye ni mjamzito na anaishi katika kijiji kidogo katika mkoa wa Herat.

Mara tu Taliban alipochukua udhibiti wa mkoa huo, mumewe - mchungaji - alipoteza kazi.

Akiwa na pesa kidogo na kuogopa kundi la Taliban, Lina hakutembelea kliniki hadi mfuko wa maji ulipopasuka.

"Mume wangu alinipeleka huko na punda. Mkunga alisimamia shida zangu na aliweza kunizalisha mtoto wangu ambaye alikuwa na uzito mdogo," anasema.

Lina anabaki nyumbani katika "hali mbaya sana" na bila kipato chochote, hajui jinsi ya kukidhi mahitaji ya mtoto wake.

Waafghanistan wengi wanaogopa kuwa shida ya huduma ya afya nchini humo inaongezeka hadi kufikia hatua ya kutowezekana na watu wengine walio katika mazingira magumu - wanawake wajawazito, mama wachanga na watoto wadogo - wanaathirika.

"Hali inazidi kuwa mbaya kila siku inayopita," anasema Abida, ambaye sasa anaendelea na majukumu ya mkunga akiwa hana matumaini.

"Hakuna anayejua yatakayotokea kwetu."

Majina ya waliohojiwa yamebadilishwa kwasababu ya kulinda usalama wao. Picha ni kwa hisani ya Elaine Jung