Mzozo Afghanistan: Wafanyakazi wote wa serikalini watakiwa kubaki nyumbani

"We are all together, we broke the oppression" - signs at protest in Kabul

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Baadhi ya wanawake walifanya maandamano kupinga marufuku hiyo

Meya mpya wa mji mkuu wa Kabul nchini Afghanistani amewataka wafanyakazi wote wa kike kubaki nyumbani labda kwa ajira zile ambazo wanaume hawawezi kuzifanya.

Hamdullah Noman alisema Watalibani wamebaini kuwa ni muhimu kuwasitisha wanawake kufanya kazi kwa muda.

Marufuku mpya iliyowekwa kwa wanawake wa Afghanistani inatokana na msimamo kutoka serikali mpya ya kiislamu.

Wakati wa utawala wao wa awali miaka ya 1990 wanawake walikatazwa kusoma na kufanya kazi.

Baada ya kulidhibiti taifa hilo mwezi uliopita kufuatia kuondoka kwa majeshi ya Marekani , Watalibani walisema "haki za wanawake zitaheshimiwa kwa kuzingatia sheria za kiislamu. ".

Lakini Taliban wanatumia mfumo wa jinsi wanavyotafsiri wao sheria ya kiislamu.

Tangu waingie madarakani wanawake wanaofanya kazi waliambiwa kukaa nyumbani mpaka hali ya kiusalama itakapotengamaa na wapiganaji wa Taliban wamekuwa wakiwapiga wanawake wanaoandana dhidi ya utawala mpya unaowapendelea wanaume tu.

Makundi ya kiislamu yanaonekana kufunga wizara ya masuala ya wanawake na kuweka idara ambayo awali ilikuwa ina sheria kali za kidini.

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Na mwishoni mwa wiki, shule za sekondari zimefunguliwa lakini zikiwa na wanafunzi na walimu wa kiume tu darasani.

Serikali ya Taliban imesema inafanyia kazi mpango wa kufungua shule za wasichana .

Kwa mujibu wa meya wa Kabul kuwa moja ya tatu ya wafanyakazi ni wanawake ambao ni sawa na idadi ya 3,000 . Alisema baadhi wataendelea kufanya kazi .

"Kwa mfano wanawake wanaofanya kazi katika vyoo vya wanawake ambako wanaume hawawezi kwenda kusafisha,".

wahudumu

"Lakini kwa nafasi nyingine , wanaume watafanya hizo kazi , tumewaambia wanawake kubaki nyumbani mpaka hali itakapokuwa shwari. Watalipwa mishahara yao," aliongeza kusema.

Siku ya Jumapili, kulikuwa na maandamano ya wanawake wachache nje ya wizara ya masuala ya wanawake wakati kundi lingine la wanawake likiwa limeitisha mkutano na waandishi wa habari kutaka haki yao .

Mmoja kati ya waliokuwa wanaandamana alisema alisema " hatutaki wizara hii kuondolewa . Kuondolewa kwa wanawake ina maanisha kuwa ni kuondolewa kwa binadamu ."

Katika kutenganisha maendeleo , tume huru ya haki za binadamu ya Afghanistan ilisema haiwezi kutekeleza majukumu yake tangu Taliban ianze kutawala.

Shirika hilo limesema katika taarifa yake kuwa majengo, magari na komputa ; vyote vimechukuliwa na Taliban.