Uchaguzi wa Urusi: Mambo matano unayohitaji kujua

Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi inafanya uchaguzi wa bunge na tawala za mitaa kutoka Ijumaa Septemba 17 hadi Jumapili Septemba 19 Septemba.
Rais Vladimir Putin amesema hili ni "tukio muhimu zaidi katika maisha ya jamii na nchi".
Lakini kwa nini uchaguzi huu ni muhimu sana?
Ili kusaidia kuelezea -Haya hapa mambo matano unayohitaji kujua.
1. Nani anachaguliwa na nani anapiga kura?

Chanzo cha picha, Getty Images
Viti vyote 450 katika bunge la Urusi ambalo pia linafahamika kama State Duma vinagombaniwa.
Urusi ina mfumo wa uongozi wa bunge na rais.
Rais ana nguvu halisi katika kuamua mkondo wa kisiasa na kiuchumi kwa maendeleo ya nchi lakini bunge lina jukumu muhimu ya kupendekeza sheria mpya.
Urusi ni serikali ya shirikisho inayojumuisha maeneo 85 - jamhuri au mikoa. Halmashauri za mitaa au mabunge ya mitaa, kama zinavyoitwa katika hali zingine, zina jukumu muhimu katika maendeleo ya mkoa, kwani zinadhibiti matumizi ya ndani na kuathiri moja kwa moja maisha ya watu ya kila siku.
Hii ndio sababu mtu yeyote anayechaguliwa katika bunge la majimbo ana umuhimu sawa na bunge la kitaifa. Wakati huu sehemu zingine za nchi zitafanya uchaguzi wa mitaa - ikiwa ni madiwani wa eneo hilo au wabunge wa mitaa (39 kati ya mikoa 85) au magavana wa mitaa (mikoa tisa na jamhuri).
Urusi ina mfumo mchangannyiko wa upig kura - nusu ya wabunge katika bunge la Duma wanachaguliwa kupitia orodha ya chama na nusu nyingine ya wabunge kupitia uteuzi wa kitaifa
Kuna zaidi ya watu milioni 108 waliojisajili kupiga kura nchini Urusi. Pia kuna zaidi ya wapiga kura milioni mbili wa Urusi walioko nje ya nchi. Kuna tarajiwa kuwa na zaidi ya vituo 95,000 vya kupiga kura.
Urusi ni nchi kubwa iliyo na zaidi majira 11 - wakati vituo vya kupiga kura vitakuwa vinafunguliwa katika eneo la mashariki ya mbali huko Kamchatka, watu wengi wa Urusi upande wa Ulaya mgharibi mwa nchi watakuwa hawajalala.
2. Kwa nini uchaguzi unafanyika siku tatu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Uchaguzi hua unafanyika Jumapili nchini Urusi na huchukua siku moja.
Lakini kutoka mwaka jana kanuni zimebadilika ili kuzingatia vizuizi vya Corona kama ilivyofanyika wakati wa kura ya maamuzi mwaka 2020 imeamuliwa uchaguzi mkuu ufanyike kwa siku tatu ili watu wasikaribiane.
Ndio sababu uchaguzi ulianza Ijumaa Septemba 17 a utaendelea hadi Jumapili Septemba 19.
Katika baadhi ya maeneo ya Urusi watu wanaweza kupiga kura kwa njia ya kielektroniki kupitia tovuti ya tume ya uchaguzi.
3. Nani anashiriki?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna mamia ya wagombea huru wanaoshiriki katika uchaguzi huu.
Kampeni hii imetiwa dosari na visa vya wagombea wengi wa upinzani kuzuiwa kuwania viti.
Mamlaka za Urusi zinasisitiza walizuiwa kwa sababu wanakabiliwa na uchunguzi wa uhalifu unaoendelea.
Miongoni mwa wagombea waliozuiliwa ni wale ambao waliwahi kuchaguliwa katika bunge la majimbona wale ambao hawajawahi kugombea.
Rais mwenyewe hatagombea - kwa sababu rais hawezi kuchaguliwa kwenda bunge lakini atapiga kura yake
4. Je! "Smart voting" ni nini na Google ina uhusiano gani nayo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo mwaka wa 2018, mwanasiasa wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny na wafuasi wake walikuja na zana ya upigaji kura ya busara inayoitwa "Smart Voting" ambayo waliamini ilipunguza nafasi za chama tawala kuongeza muda wake wa kusalia madarakani.
Walibuni programu tumishi ambayo iliwashauri wapiga kura wampigie kura mgombea yupi ili kuzuia wagombea wanaoungwa mkono na mamlaka kuchaguliwa
Navalny na timu yake walisema mfumo huo ulithibitika kuwa mzuri katika chaguzi zingine za mitaa - madai ambayo yalipingwa na vyama vingine vya upinzani na mamlaka.
Katika majira ya joto mashirika yote yaliyohusishwa na Alexei Navalny, ambaye amekuwa gerezani tangu Januari, yalipigwa marufuku nchini Urusi, baada ya kutajwa kuwa na msimamo mkali na kufanya kama maajenti wa kigeni.
Mapema mwezi huu wa Septemba mwangalizi wa vyombo vya habari wa serikali ya Urusi alifungia wavuti wa " smart voting", akisema jukwaa hilo linatumika kuendelea na shughuli za shirika lililotambuliwa kuwa na "msimamo mkali".
"Smart voting" alitoweka katika injini kuu ya utaftaji ya Urusi Yandex lakini aliendelea kuja kwenye Google nchini Urusi.
Siku moja kabla ya kuanza kupiga kura kulikuwa na ripoti za watoa huduma wakuu wa rununu wa Urusi kuanza kuzuia upatikanaji wa huduma tamba ya Google Docs, baada ya mshirika wa mkosoaji wa Kremlin aliyefungwa Jela Alexei Navalny, kuchapisha orodha ya wagombea wa Duma waliopendekezwa.
5. Matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa lini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Hii inategemea maeneo.
Katika baadhi ya maeneo matokeo yanatarajiwa Jumatatu Septemba 20 lakini katika maeneo mengine kura inachukua muda mrefu kuhesabiwa.
Pia kuna uwezekano wa chaguzi zingine mitaa - za magavana wa mkoa au wakuu wa jamhuri- watu wakashiriki duru ya pili ya uchaguzi













