Je ni kwa kiwango gani tunaweza kusema kwamba kufika kilele sio lengo kuu katika tendo la ndoa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati fulani wa likizo, tulikwenda kutembelea minara au sehemu maalum tulizopendekezewa.
Wakati tulipokuwa huko tukijifurahisha tulijiuliza iwapo eneo hilo ndilo tulilopaswa kwenda.
Je! tulilifurahia ziara hiyo? Kwa hali yoyote, tuliporudi nyumbani, tukaambiana "Nadhani hivyo ndivyo ilivyokuwa"
Tunapozungumzia kufika kilele wakati mwingi mambo kama hayo hujitokeza.
Je Kilele cha wanawake ndio lengo la kushiriki tendo la ndoa?
Hali hii huonekana kama mwisho wa tendo la ndoa. Pengine kwa sababu ya ushawishi wa waanzilishi wa somo la ujinsia Masters na Johnson ambao waliona kama tamati ya mzunguko wote wa hisia za tendo la ndoa.
Uzoefu ambao George Bataille katika insha yake kuhusu 'mihemko ya kingono' aliita le petite morte, akiashiria wakati ambapo mtu hupoteza fahamu kwa muda mfupi wa sekunde mbili huku akikaza misuli .
Ukweli ni kwambo ni hali ya kusisimua zaidi ambayo hutokea wakati wa kipindi cha 'msisimko wakati wa tendo la ndoa. Kwa kweli ni hali ya kipekee ambayo uzoefu wake hauwezi kuhamishwa kama inavyotokea na hali zengine zozote za binadamu.

Chanzo cha picha, MALAYALAMEMAGAZINE.COM
Kupitia matamshi yetu wenyewe binadamu huelezea uzoefu au hali za kihemko. Matamshi hayo yanaashiria kwamba tunachukulia kilele kama lengo la kushiriki tendo la ndoa.
Je utafiti uliofanywa kuhusu kufika kileleni unasemaje?
Kwa njia hii, ripoti za mtaalam wa masuala ya jinsia Alfred Kinsey (kati ya miaka ya 40 na 50) zilitegemea, kwa kiasi kikubwa kipimo hiki cha tendo la kujamiiana ambapo tamati yake ni kutokwa kwa mbegu za kiume upande wa wanaume huku wanawake wakiwa na unyevu katika sehemu zao za siri.
Tatizo kuu ni kwamba imani za utamaduni wetu kuhusu kufike kilele unafanana na ule wa kiume: Ambapo mtu anapofika kilele hisia zinapanda kwa ghafla kupitia kuonesha vitendo kabla ya kukaza misuli na baadaye kumwaga mbegu za kiume. Hivyobasi wanawake wengi, wanapojaribu kulinganisha uzoefu wao wenyewe, hugundua kuwa haufanani.
Waanzilishi wa saikolojia ya kisasa ya masuala ya kujamiiana walisema kuwa kufika kileleni kwa wanawake kulionekana kulikuwa tofauti ikilinagnishwa na wanaume.
Kwa hivyo, itakuwa sahihi kwetu kuanza kujenga wazo halisi zaidi ya taswira, kufika kileleni inayohusiana zaidi kama hali au uzoefu wa msisimko wa hali ya juu, kilele na tofauti kubwa kwa kiwango na uwasilishaji, ambayo si mtazamo tulionao kwa kawaida.
Karibu nayo kuna safu ya majadiliano ambayo wino mwingi umemwagika katika uchunguzi mchache uliofanywa katika suala hili.
Tatizo la kuhusisha tendo la ndoa na uzazi
Hisia ya kufikia hatua ya kilele miongoni mwa wanawake imefikiriwa kuwa na mshindo mkubwa.
Wazo hili lilitolewa na mtaalam bingwa wa kisaikolojia Sigmund Freud, wakati alipowaza kwamba mshindo uliosababishwa na watu wawili kujamiana ndio uliofanana na ukuaji kamili wa kijinsia.
Hili lilikuwa wazo lililoshirikishwa na uzazi kama dhana ya ngono yenye afya. Hii imefanya iwe vigumu kutumia dhana tofauti katika uchunguzi mwingine.

Chanzo cha picha, VIRALNIGERIA
Pia kuna mijadala chungu nzima kuhusu kutumia mafuta ya kuondoa ukavu mbali na sehemu za siri za wanawake kuwa tayari kwa tendo la ndoa suala ambalo bado haijatatuliwa.
Tunaweza kusema kwamba kumekuwa na upungufu wa utafiti wa masuala ya tendo la ndoa kwasababu ya tamaduni zetu, hususan iwapo masuala hayo yanagusia wanawake.
Mwanamke pia hufika kilele wakati wa tendo la ndoa, na mchakato wote wa kufika kilele una vyanzo sawa na wakati mwanaume anapofika katika hali hiyo.
Tangu karne ya 17 , sehemu za siri za mwanamke zimefafanuliwa katika jarida la XIX Skene Glands, kwa heshima ya rais wa jamii ya wakunga nchini Marekani Alexander Skene ,ambaye ndiye mtafiti bingwa wa sehemu za siri za wanawake.
Itakumbukwa kwamba tafiti za hivi karibuni zimekuwa hazitumii neno 'Female Prostate' na hadi kufikia sasa hakuna neno la moja kwa moja kuelezea mfumo wa wanawake wakati ukiwa tayari kushiriki tendo la ndoa - hali inayosababisha kuchelea kwa tafiti za tendo la ngono.
Katika idadi kubwa ya wanawake, tezi zinazosababisha unyevu wakati wa tendo la ndoa hazionekani na ishara za kufika kilele mara nyingi hazionekani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Yote ni matukio ya mwitikio wa kijinsia chini ya tafiti hizi huku ushahidi mchache ukipatikana kwa sababu ya upinzani ambao umekuwepo katika tafiti za ngono kila wakati.
Kuna upendeleo fulani kwamba utafiti wa tendo la ndoa unaweza kufichua tabia yake ya kushangaza.
Hatahivyo, hilo ni jambo ambalo sayansi haiwezi kuliteka nyara, hususan kwasababu tabia hiyo ni ya uzoefu, ya kimazingira na ya makusudi, na kile sayansi inachofanya ni kusoma vigezo vya malengo yake na kuvipatanisha ili viweze kuwa na faida katika kutatua shida.
Mwitikio wa kijinsia ni jambo la kusisimua, jambo la kihemko na mabadiliko muhimu ya kisaikolojia, ya mwili na tabia.
Miongoni mwao, inaulizwa ikiwa mshindo wa mwanamke ni wa uke au wa kibinadamu. Kwa kuzingatia hii, tunaweza kusema kuwa inaweza kuwa ya uke, ubongo, kuota ... na aina nyingine elfu za kuamka kihisia.














