Agnes Sithole: Mwanamke aliyepambana na sheria za ndoa zinazo wadhulumu wanawake Afrika Kusini

A photo of Agnes Sithole

Chanzo cha picha, Agnes Sithole

Agnes Sithole amekuwa shujaa ambaye hakutarajiwa kwa maelfu ya wanawake weusi nchini Afrika Kusini.

Akiwa na miaka 72, alimpeleka mahakamani mume wake ili kumzuia asiuze nyumba yao kinyume na matakwa yake- na katika mchakato huo alipambana na sheria za miongo kadhaa za enzi za ubaguzi wa rangi kupata haki yake.

Aliolewa na Gideon, mpenzi wake wa zamani tangu walipokuwa wanafunzi wa shule ya upili mwaka 1972, lakini mambo yalibadilika akajipata anavumilia katika ndoa iliyozongwa na uzinifu kwa miongo kadhaa.

"Amekuwa kwenye mahusiano tofauti lakini ilo halikuniathiri hadi kati ya mwaka 2016 na 2017, wakati alitaka kuuza mali yetu yote," anasema. "Jibu lake kila wakati ni kwamba - hiyo ilikuwa nyumba yake, mali yake, na mimi sina chochote."

Alipoona anaelekea kupoteza nyumba yake, Agnes aliamua kukabiliana kisheria na mume wake mnamo mwaka 2019, katika mahakama ya Afrika Kusini, hatua ambayo sio ya kawaida miongoni wa wanawake weusi wa kizazi cha

''Wakati huo nilikuwa na miaka 72 - nilikuwa niende wapi au nianzie wapi? Kwa hivyo chaguo langu la pekee lilikuwa kupigana au kujikuta niko barabarani na umri wangu huu, "anasema." Nadhani uhitaji ulinifanya niwe jasiri. Laiti haingelikuwa hivyo basi labda nisingechukua hatua hiyo. Ilibidi nisimame kidete na kusema hapana. "

'Wanawake hawakua na chaguo'

Agnes aliolewa wakati Afrika Kusini ilikuwa ilipokuwa kiongozwa na Wazungu walio wachache hivyo basi wapenzi hao weusi moja kwa moja walioana kupitia mfumo unaoitwa "out of community of property",ambao uliwapa wanaume haki zote za mali," anaelezea Agnes.

Agnes na mume wake siku ya harusi yao

Chanzo cha picha, Agnes Sithole

Maelezo ya picha, Agnes aliolewa na Gideon, mpenzi wake wa shule ya upili mwaka 1972

Marekebisho ya sheria ya mali katika ndoa iliyofanywa mwaka 1988 iliruhusu wanandoa weusi kubadilisha hali ya ndoa yao kuwa "katika jamii" - kutoa haki sawa za mali kwa wanawake.

Hata hivyo, sheria hiyo ilikuwa na masharti. Wanawake weusi walitakiwa kupata idhini kutoka kwa waume zao, walipie ombi hilo, na kuliwasilisha ndani ya kipindi cha miaka miwili.

"Tulijua kwamba sheria imebadilika kwa kila mtu," anakumbuka Agnes. "[Baadae], nilipogundua sheria imenidanganya nikaamua kukabiliana na hili suala kwa nguvu zote."

'Mimi ni mpambanaji'

Agnes alizaliwa Vryheid, mji mdogo wenye migodi ya mkaa wa mawe uliopo kaskazini mwa KwaZulu-Natal.

Kote nchini kulikuwa na mgawanyiko wa wazi wa kiuchumi kati ya jamii katika miaka ya 1940. Baba yake alikuwa akisafisha treni na "kuwapikia chai wakuu wake weusi ofisini". Mama yake alikuwa "mfanyakazi wa ndani" ambaye alipika na kuosha vyombo vya "familia za kizungu zenye uwezo".

Agnes na baba yake akiwa amembeba dada yake mdogo, nje ya nyumba yao.

Chanzo cha picha, Agnes Sithole

Maelezo ya picha, Agnes na baba yake akiwa amembeba dada yake mdogo, nje ya nyumba yao.

"Nilizaliwa katika familia masikini, wazazi wangu walikuwa wajakazi. Nawalikuwa kielelezo chema kwetu," anasema Agnes.

"Tulikuwa tukienda kanisan kila wikendi. Wakati nikikua, Wakatoliki walikuwa hawaruhusiwi kutalakiana, Hata ikiwa mambo hayaendi vizuri," aliongeza. "Sikutaka kuolewa tena au kuona watoto wangu wakikuwa bila ya wazazi wote wawili nyumbani - nilikuwa nikujua hivyo."

Licha ya changamoto, Agnes aliwaona wazazi wake wanafanikiwa kwa kukaa pamoja na kuona mapambano yao yalimfanya aamue kuwa na maisha bora.

Alisomea uuguzi kabla ya kuolewa naGideon.Baadaye, baadaye alianza kuuza nguo na kufanya kazi tofauti ili kujikimu kimaisha.

Agnes (kushoto) alifanya kazi kama muuguzi kabla ya kuolewa na kuanza familia

Chanzo cha picha, Agnes Sithole

Maelezo ya picha, Agnes (kushoto) alifanya kazi kama muuguzi kabla ya kuolewa na kuanza familia

"Hivi karibuni niligundua kuwa nilikuwa peke yangu, kwa sababu mume wangu alikuwa ndani na nje ya maisha yetu," anasema Agnes, ambaye alikuwa na watoto wanne naye.

"Nilikuwa nikitoka kazini naanza kushona nguo, kununu ana kuuza nguo. Nilikuw anikifanya vitu vingi kwa wakati mmoja kwa sababu nikuwa nimejitolea kuhakikisha watoto wangu wanasoma shule," aliendelea kusema.

"Mimi ni mpambanaji, ndio hulka yangu, nimekuwa nikipambana maisha yangu yote.Badala ya kumtegemea mtu anifanyia kitu, Nilipendelea kujifanyia mwenyewe."

Agnes Sithole na watoto wake wanne

Chanzo cha picha, Agnes Sithole

Maelezo ya picha, Agnes alihoji kuwa alichangia ustawi wa familia yake wakati alipokuwa katika ndoa

Kulingana na Agnes, ndoa yao ilsambaratika karibu miaka tisa iliyopita. Alipotoka kazini jioni moja alipata Gideon hamehamia chumba cha malazi cha ziada bila maelezo yotote.

Wanandoa hao waliendelea kuishi pamoja lakini kila mmoja alishika lake.

"Tungelikutana kwenye roshani, ngazi au tukiegesha magari bila kusemezana"anakumbuka.

Agnes anasema Gideon hakuwahi kuzungumzia mpango wa kuuza nyumba na "Nilishtuka sana kuona watu wakija kangalia nyumba kwa lengo la kununua".

Alipogundua huenda akasalia bila makazi mwka 2019 akaamua kuwasilisha kesi ya kulalamikia unyanyasaji wa kiuchumia - akihoji kuwa yeye pia alichangia ustawi wa familia na kwamba ana haki ya mali.

Agnes na mume wake Gideon Sithole

Chanzo cha picha, Agnes Sithole

Maelezo ya picha, "Sijutii chochote na muhimu zaidi nimetimiza ndoa yangu,"anasema Agnes

Miaka miwili baadaye, Mahakama ya Katiba nchin Afrika Kusini Ilidumisha uamuzi wa awali wa Mahakama kuu kwamba sheria zilizopo zinawabagua wanandoa weusi hususan wanawake weusi.

Iliamua kuwa ndoa zote zilizofungwa kabla ya mwaka 1988 zitabadilishwa kuwa "in community of property" - kuwapa wanawake haki sawa za mali.

Agnes na binti yake mdogo walifuatilia uamuzi mtandaoni wakiwa chumbani. Awali, hakugundua ameshinda kesi hadi wakili wake alipompigia simu.

"Hatukung'amua kilichokuwa kinaendelea kwa sababu ya istilahi ya [kisheria]," anasema. "Hatukuelewa chochote ijapokuwa tulikuwa tunafuatilia. Tumbo ilinijaa maji, Nilikuwa na hofu pia nilikuwa na imani.

"Nilibubujikwa na machozi ya furaha.Niligundua kwamba tulikuwa tumeokoa maelfu ya wanawake katika ndoa sawa na yangu, "anasema Agnes.

Agnes nasema ujasiri wake umetokana na changamoto nyingi alizokumbana nazo maishani.

"Ni hulka yangu, hivi ndivyo nilivyo, Nataka kujitegemea kwa kila njia," aliendelea kusema. "Bila shaka ni jambo ambalo sio la kawaida katika utamaduni wetu na kwa wanawake wa kizazi changu.

"Kushinda kesi hii ni jambo zuri sana kuwahi kufanyika maishani mwangu."

Agnes,mume wake Gideon na mabinti zao watatu

Chanzo cha picha, Agnes Sithole

Maelezo ya picha, Agnes na mume wake Gideon walioana kwa karibu miaka 50

Agnes amemsamehe Gideon, ambaye alifariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19 wakati kesi ikiendelea.

Siku mbili kabla kifo chake, alimuomba msamaha mke wake na mabinti zake kutokana na jinsi mambo yalivyoenda.

Agnes baaadaye aligundua kuwa hakuwekwa katika wosa wake tu bali pia nyumba yao iliachiwa mtu mwingine. Walakini, uamuzi wa korti uliondoa matakwa yake.

"Tumemsamehe na moyo wangu una amani. "Sijutii chochote na muhimu zaidi nimetimiza ndoa yangu [hadi mwisho],"anasema Agnes.

"Sikutaka chochote ambacho kilikuwa chake lakini alitaka kuchukua kila kitu, pamoja na kile nilichomiliki na kukifanya kazi na hiyo ndio sikuipenda."