Virusi vya corona: Nesi wa Ujerumani 'aliyewachanja' maelfu ya watu kwa maji ya chumvi

Udanganyifu huo ulitokea katika kituo cha chanjo kama hiki katika jiji la Dresden.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Udanganyifu huo ulitokea katika kituo cha chanjo kama hiki katika jiji la Dresden.

Muuguzi mmoja anachunguzwa kwa kuwachanja maelfu ya watu nchini Ujerumani kwa kutumia maji ya chumvi badala ya chanjo ya corona.

Kisa hicho kilifanyika kati ya mwezi Machi na Aprilii mwaka huuu katika kituo cha kutoa chanjo mkoani Friesland, eneo la vijijini lililopo kasakazini mwa nchi hiyo.

Ijapokuwa kudungwa sindano ya maji ya chumvi sio hatari, anakadiriwa wakazi 8,600 wengi wao wazee waliohatarini kuambukizwa virusi vya corona walipokea chanjo feki.

Naibu mkuu wa polisi wa Wilhelmshaven-Friesland Peter Beer, amewaambia waandishi wa habari kwamba kulingana na ushahidi uliotolewa ''kuna uwezekano mkubwa tukio hilo hatari lilifanyika".

Mamlaka zinatoa wito kwa watu ambao huenda wameathiriwa kuchanjwa tena.

Hakuna maelezo ya kina yaliyotolewa kumhusu nesi huyo - ambaye hakutambulishwa- lakini inafahamika aliyefanyia kazi shirika la Msalaba mwekundu alikuwa akisimamia kuweka chanjo ya Pfizer, Moderna au AstraZeneca kwenye sindano.

Mwisho wa April jali ya kubadilisha dawa katika sindano hizo ilijulikana, lakini wakati huo iliaminika kuwa lilikuwa tukio la kipekee, kulingana na gazeti la Ujerumani Süddeutsche Zeitung.

Wakati huo nesi huyo alikiri kuwa ameweka maji ya chumvi kwenye sindano sita badala ya chanjo ya Pfizer. Moja ya sindano hizo ilianguka chi ni alipokuwa akijaribi kuchanya, akajaribu kuficha. gazeti la Ujerumani liliandika.

Nesi huyo alikuwa akisimamia kuweka chanjo kwenye sindano

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nesi huyo alikuwa akisimamia kuweka chanjo kwenye sindano

Mamlaka zilichukua hatua ya kuchunguza kiwango cha ulinzi cha zaidi ya watu 100 waliochanjwa siku hiyo kwa kutumia vipimo vya kinga ya mwili.

Polisi na waendesha mashtaka waliendelea na uchunguzi wa kina na walipata ushahidi wa maambukizi mapya wakati wa kumfanyia uukaguzi shahidi mmoja katikati ya mwezi Juni, kulingana na Naibu Mkurugenzi wa Polisi Beer.

Imebainishwa kuwa chanjo 10,000 huenda zilivurugwa.

"Nimeshangazwa sana na kisa hiki," alisema Kasela wa Friesland Sven Ambrosy, akiomba waliioathirika kuchanjwa upyaharaka iwezekanavyo.

"Lazima tuwaepushe watu na madhara, hata kama hatujui ni watu wangapi walioathiriwa," alisema.

Haijulikani nia ya muuguzi huyo ilikuwa nini kwa udanganyifu huo, lakini hapo awali alikuwa ameelezea mashaka yake dhidi ya chanjo kwenye mitandao ya kijamii, kulingana na watafiti.

Kesi ya muuguzi huyo imepelekwa kwa kitengo maalum kinachochunguza uhalifu unaochochewa kisiasa.

Makundi yanayopinga chanjo yamepata ufuasi mkubwa nchini Ujerumani

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Makundi yanayopinga chanjo yamepata ufuasi mkubwa Ujerumani

Makundi yanayopinga chanjo nchini Ujerumani yamepata nguvu na wafuasi wengi kutokana na ujumbe usiokuwa na msingi unaoangazia nadhari za kula njama katika mitandao ya kijamii na maandamano makubwa.

Moja ya makundi hayo ni lile la Querdenken, lililo na ufungamano nasiasa za mrengo wa kulia.Msimu uliopita wa joto liliandamana na kujaribu kuvamia bunge la nchi hiyo mjini Berlin.