Gen Tsadkan Gebretensae: Jenerali hatari wa kijeshi anayeongoza maasi ya TPLF Ethiopia

Chanzo cha picha, Tsadkan family
Kwa mara ya pili katika maisha yake, jenerali wa zamani amejikuta katikati ya uasi dhidi ya serikali ya Ethiopia katika eneo la Tigray, anaandika mchambuzi Alex de Waal.
Kamanda wa vikosi vya waasi wa Tigraya, Jenerali Tsadkan Gebretensae, anachukuliwa na wachambuzi wa usalama wa kimataifa kama mmoja wa wataalamu bora wa kijeshi wa kizazi chake barani Afrika.
Jenerali huyo mwenye umri wa miaka 68- aliacha kusomea shahada yake ya bailojia katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa mwaka 1976 na kujiunga na kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF).
Awali kilikuwa kikosi kilichokuwa kikipigana vita vya kuvizia milimani dhidi yakatika utawala wa kiimla wa Mengistu Haile Mariam.
Utafiti wake, ujuzi wa taasisi yake na uwezo wa kuaminiwa na wapiganaji ulianza kuonekana mwishoni mwa mwaka 1980, alikuwa kamanda anayeheshimika sana katika operesheni za kivita.
Mwaka 1991, TPLF ilipigana na wanajeshi zaidi ya 100,000 wakiwemo wale waliojitenga.
Mwezi Mei mwaka huo, Jenerali Tsadkan - pamoja na wanajeshi wa Eritrea waliungana na TPLF - na kuongoza shambulizi ambalo lilifanikiwa kuuteka mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, na kuondoa madarakani utawala wa Mengistu

Chanzo cha picha, Getty Images
Wapiganaji wa TPLF waliingia na kuchukua kwa muda makao makuu , katika nyumba ya wageni karibu na hoteli ya Hilton.
Hapo Jenerali Tsadkan alilala katika kitanda chenye mashuka kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 15. Chini ya amri yake , wapiganaji hao wa porini waliingia mjini Mei 28, na kuanza kuwalipa mafao na mishahara ya watumishi siku tatu baadae.
Shambulio dhidi ya ngome ya al-Qaeda
Kwa miaka saba , Jenerali Tsadkan aliongoja mabadiliko ya kuimar isha jeshi la Ethiopia .Alipewa cheo cha Ujenerali na mkuu wa majeshi.
Wakati ambao Jenerali Tsadkan alikuwa kiongozi wa jeshi la taifa la Ethiopia kwa kipindi cha miaka 10,kamanda huyo wa zamani wa TPLF alisuka mipango yote ya kijeshi , aliongoza kulikosoa jeshi kuwa na upendeleo , kwa kuwa watu wa Tigray walikuwa 6% ya idadi yote.
Jenerali Tsadkan alirudi chuo na kusoma shahada ya uzamivu ya biashara katika Chuo Kikuu cha Open nchini Uingereza.
Profesa Graeme Salaman anamkumbuka mwanafunzi wake wa zamani: "Alikuwa hakai kuwa mwanajeshi mwenye ubaguzi,- alikuwa mkimya, anayependa kutafakari, msikivu , alikuwa na aibu, mwerevu lakini alikuwa shupavu."

Chanzo cha picha, Getty Images
Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalikuwa yamemalizika lakini bado ina ghasia.
Aliwaleta wapiganaji wa al-Qaeda kutoka Somalia mwaka 1996 na pia kutuma vikatumwa mpaka wa Sudan kumuunga mkono mpinzani wa rais Omar al-Bashir.
Kuachishwa kazi jesheni
Jenerali Tsadkan alimuonya kiongozi wa Eritrea Isaias Afewerki aliitishia Ethiopia na kupuuziwa na mwenzie wa TPLF , na baadae waziri mkuu Meles Zenawi.
Lakini wakati wa vita na Eritrea ambayo ilitokea mwaka 1998, Jenerali Tsadkan alikuwa kiongozi wa mipango ya jeshi la Ethiopia.
Ilikuwa ghasia kubwa ambayo iligharimu maisha ya watu 80,000 kutoka pande zote mbili.
Mwezi Juni, 2000, Ethiopia iliivamia Eritre na wanajeshi walisambazwa mpakani.
Jenerali Tsadkan alikuwa amejidhatiti kufanikiwa Zaidi ya mji mkuu wa Eritrean Asmara, lakini waziri mkuu Meles alitaka kusitisha vita hiyo na kusema malengo ya vita ya Ethiopia yalipatikana na Eritrea sasa ina heshima.

Baada ya vita, TPLF ilisambaratika vibaya kutokana na malengo ya vita na maelekezo ya kisiasa ya chama.
Bwana Meles alimfukuza Jenerali Tsadkan katika kazi ya ukuu jeshi.
Hivyo ghafla kukosa kwake kwa ajira kumtambulisha kutopendwa kwake na viongozi wa TPLF,na kuangaliwa kwa karibu na wakala wake wa usalama, Jenerali Tsadkan alipata wakati mgumu kuzoea kuwa raia wa kawaida.
Aliandika ripoti ya namna wanajeshi wanaweza kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Aliajiriwa na idara ya Uingereza ya maendeleo ya kimataifa kushauri serikali mpya ya Sudan Kusini masuala ya sekta ya usalama- mradi ambao haukufanikiwa kuimarisha jeshi la nchi hiyo.
Jenerali Tsadkan alianza kufanya biashara katika maeneo ya nyumbani katika wilaya ya Raya, kusini mwa Tigray, na kuanza biashara ya mbogamboga.
Hisia za mapambano dhidi ya Tigray
Alikosolewa vikali na wanadi wake wa zamani wa TPLF alipounga mkono uteuzi wa Abiy Ahmed kuwa Waziri Mkuu wa Ethipia mwaka 2018 na kusema yuko tayari kufanya kazi naye.

Mwaka 2019 alijiunga na kundi ambalo halikuwa rasmi ili kujaribu kuwapatanisha bwana Abiy na viongozi wa TPLF lakini aliacha mwaka mmoja uliopita na kusema bwana Abiy hayupo makini.
Hisia za kutengwa kwa Tigray ziliongezeka katika mji mkuu wa Addis Abab, alirudi katika mji mkuu wa Tigray', Mekelle.
Wakati vita ilipotokea Tigray mwezi November mwaka jana, alijiunga na jeshi la waasi, na kuachana na tofauti zake na viongozi wa Tigray.
Vijana walijiunga kulaani mauaji ya kusikitisha yanayotokea dhidi ya watu wao.
Wapiganaji wengine wakiwemo wale ambao walijitenga na TPLF miaka iliyopita walijiunga.
Katika upande wa serikali ya Ethiopia ambayo ilitaka Jenerali Tsdakan na viongozi wengine wa Tigray kukamatwa. Iliwashutumu kwa kuwa waasi ambao walianzisha vita na walipanga kushambulia ngome ya jeshi la serikali lililopo Tigray.
Mafanikio ya kushangaza ya jeshini
Mapigano yaliandaliwa na jeshi la ulinzi la Tigray Defence Forces (TDF), wakishirikiana na wajumbe wa TPLF na wasio wajumbe wa-TPLF.
Jenerali Tsadkan alipewa jukumu la kusimamia masuala ya kijeshi.

Chanzo cha picha, AFP
Mwezi Januari, alisema : "Tulikuwa tunaangukia vumbi." Walikuwa wanakimbia , na kujificha katika milima ya kusini mwa Tigray, wapiganaji wengi wadogo walikuwa peku, wakiwa na silaha mikononi mwao.
Lakini walifanikiwa kupata ushindi na kuwashangaza wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea jinsi walivyoongoza mashambulizi.
Jenerali Tsadkan hakusema ni wapiganaji wangapi wa TDFambao waliuawa au walijeruhiwa.
Kwa miezi minne ya mafunzo , kupanga mapigano na mapigano wakati huohuo mpaka Mei, Jenerali Tsadkan na makamanda wengine walikadiria kuwa walifanikiwa kupata usawa kutoka kwa wapinzani wao.

zaidi kuhusu mzozo wa Tigray:

Wiki tatu zilizopita , mataifa yenye nguvu duniani G7 imewataka kusitisha mapigano Tigray. TPLF ilitoa maelezo kuwa , iko tayari kusitisha bila ya kusema chochote juu ya kusitisha mapigano.
Alafu Juni 17 , TDF ilichukua jitihada. Ila ilisema kuwa mapigano ya mfululizo yanaendelezwa na jeshi la Ethiopia katika maeneo kadhaa - nusu ya nguvu ya jeshi. Jeshi la Ethiopia lilikanusha madai yake na kudai kuwa hiyo taarifa ya uongo.
Waandishi wa habari bado hawajatembelea katika eneo hili au kuwahoji wafungwa wa vita kuthibitisha madai haya.
Lakini yanaonekana kuwa mafanikio mazuri kwa TDF kuwa wachache walitarajiwa na jeshi la Ethiopia kuangaika Zaidi.
Hofu ya kuzozana na Eritrea
Jeshi la TDF liliingia Mekelle, na serikali ya Ethiopia na jeshi lake limekimbia kwa kudai kuwa wamesitisha mapigano.
Wakiwa na silaha kubwa, TDF sasa inakabiliana na jeshi la Eritrea, ambalo lilijumuika katika vita mwezi Novemba katika upande wa jeshi la Ethiopia.
Ni vigumu Zaidi kukabiliana nao na ingawa jeshi lake bado lipo thabiti.
Taarifa zinasema iliitelekeza miji ambayo walikuwa wameichukua kaskazini mwa Tigray na kuweka ulinzi maeneo ya mpaka.
Rais wa Eritrea Isaias anakabiliana na maamuzi ya kuondoa majeshi yake mpaka wa kaskazini au kupigana,lakini TDF inaweza kumlazimisha ili aendelee kubaki madarakani na hivyo Vita nyingine inaweza kutokea.















