NewNew: Fahamu programu inayokuwezesha kudhibiti maisha ya mtu mwingine

NewNew

Chanzo cha picha, NEWNEW

Utajihisi vipi ikiwa utalipa pesa kuweza kudhibiti maisha ya mtu mwingine kwa mambo mbalimbali binafsi yanayomhusu? Fahamu programu itakayokuwezesha kufanya hivyo.

Pale Mwandishi Brandon Wong aliposhindwa kuamua cha kuagiza wakati wa chakula cha jioni akiwa magahawani, aliomba wafuasi wake katika programu mpya inayofahamika kama NewNew kumchagulia.

Wale waliotaka kumuamulia cha kula walilipa dola 5 kupiga kura na uamuzi wa wengi ukamchagulia kula chakula cha Kikorea, na hicho ndicho alichonunua.

"Sikuweza kuamua kati ya chakula cha Kichina na Kikorea, kwahiyo programu hiyo ilinisaidia," amesema Bwana Wong, ambaye anaishi Edmonton, Canada. "Pia nimetumia programu mpya ya NewNew kuamua ni nguo gani nitakazo vaa siku hiyo na mambo mengine binafsi niliyotakiwa kujiamulia.

"Nilijiunga na program hii mnamo mwezi Machi na ninaweka ujumbe kwenye programu hiyo mara tatu au nne hivi kwa wiki. Na sasa hivi nimepigiwa jumla ya kura zaidi ya 1,700."

Mtandao wa NewNew huendeshwa na mfanyabiashara Courtne smith aliyechukua muda wa miaka miwili iliopita akitengeza wazo hilo

Chanzo cha picha, NEWNEW

Maelezo ya picha, Mtandao wa NewNew huendeshwa na mfanyabiashara Courtne smith aliyechukua muda wa miaka miwili iliopita akitengeza wazo hilo

NewNew ni program mpya na changa ya Courtne Smith mjasiriamali wa Los Angeles. Programu hiyo ambayo bado inaendelea kufuatiliwa na kuboreshwa inajieleza kama "soko la hisa la mwanadamu ambapo unanunua hisa katika maisha halisi ya watu, ili kudhibiti maamuzi yao na kufuatilia matokeo".

Kwa wengi programu hiyo huenda ikawa inatia wasiwasi, lakini ukweli ni kwamba iko sawa. Inalenga kile ambacho kinajulikana kama "wabunifu" - waandishi, wachoraji, wanamuziki, wabunifu wa fasheni, wanablogu na kadhalika.

Imeundwa kwa namna ya kumuunganisha tu na mashabiki na wafuasi wake tofauti kidogo ikilinganishwa na mitandao mingine na cha msingi zaidi, uhusiano wao ni wa kifedha.

Pale mtumiaji anapoanzisha akaunti yake ya NewNew na kuanza kupata wafuasi, ana hamasishwa kuwauliza kupitia video fupi fupi kumpigia kura katika masuala yanayomuhusu kikazi na kibinafsi.

Bwana Wong aliyeandika mchezo wa kuigiza katika tovuti fulani, pia anatumia programu ya NewNew kupigiwa kura na kuamua ni kina nani atakao lenga, majina ya wahusika na namna ya kuendeleza mchezo.

Brandon Wong huwaruhusu wafuasi wake katika mtandao wa Kijamii wa NewNew kupigia kura masuala yake ya maisha yake ya kila siku

Chanzo cha picha, BRANDON WONG

Maelezo ya picha, Brandon Wong huwaruhusu wafuasi wake katika mtandao wa Kijamii wa NewNew kupigia kura masuala yake ya maisha yake ya kila siku

Kila kura inapopigwa, mtumiaji anapata pesa, pamoja kiwango fulani cha pesa zingine kando kwa kuendesha maudhui yake.

Mtumiaji anauliza swali na kuweka majibu mawili wafuasi wake wachagua. Wafuasi wao wanapiga kura na wanaweza kulipa kufanya hivyo mara nyingi wanavyotaka. Pesa hazirejeshwi haijalishi uamuzi ambao mtumiaji ataamua kuchukua.

Mbali na kupiga kura, wafuasi pia wanaweza kulipa pesa za ziada kuanzia dola 20 kumtaka mtumiaji wa programu ya NewNew kufanya jambo jingine wanalotaka wao, kama vile kumtaja mhusika wa kitabu fulani. Lakini pia mtumiaji anaweza kukataa yote hayo na ikiwa atafanya hivyo, mfuasi wake hataitishwa pesa.

Wakati programu zingine kama vile Wishbone zinataka watumiaji kupiga kura kwasababu ya jambo fulani, programu ya NewNew, inasema kile inachofanya ni kutoa fursa kwa wafuasi kulipa ndio wapige kura kuangazia mambo binafsi na ya kikazi, kitu ambacho ni kipya.

Lakini je programu ya NewNew iliyoanzishwa miezi miwili iliyopita na sasa hivi ikiwa ina wafuasi kidogo chini ya 100 itafanikiwa kuvutia wengi?

Muigizaji Will Smith ni mwekezaji wa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muigizaji Will Smith ni mwekezaji katika programu hiyo

"NewNew ina fanana kwa kiwango fulani na program ya TikTok au mfano wa kipindi halisi cha kwenye televisheni kama vile 'Big Brother' na zote hizo zimefanikiwa kupata umaarufu," amesema.

Mwanzilishi mwenza wa programu hiyo Ms Smith, raia wa Canada amesema kuwa ana mipango mikubwa katika programu ya NewNew huku wawekezaji wakiwa ni pamoja na Peter Thiel, bilionea, mwanzilishi mwenza wa programu ya Paypal.

Wakati wengi wanaweza kuuliza "umuhimu" wa programu hiyo, ni kwamba wafuasi ndio watakaopiga kura kuamua maisha ya mtu, Bi. Smith ameongeza kwamba itakuwa ina imarisha zaidi uhusiano wa pande zote mbili. "Inafanya mtu kuwa uhusiano imara na wa karibu zaidi na mtumiaji."

Smith alimfanyia kazi Rapa Drake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Smith alimfanyia kazi Rapa Drake

Mwanasaikolojia wa masuala ya kibiashara Stuart Duff, anasema programu ya NewNew pia inaleta usheshi wakati mtu anaitumia "kuunda uhusiano wa kipekee kati ya watumiaji na wafuasi". Lakini akaongeza kuwa katika matukio machache huenda kuna wale watakao kiuka sheria.

"Huenda isichukue muda mrefu kabla baadhi ya watumiaji kutumia kila mbinu kupata wafuasi wa kumpigia kura, na kusababisha matukio ambayo ni ya kudhalilisha," amesema.

Msemaji wa kampuni ya NewNew amesema kuwa kampuni hiyo "ina haki ya kumuondoa mtumiaji na kumpiga marufuku yeyote yule ikiwa maudhui yake yatakuwa kinyume na miongozo iliyowekwa".

André Patrick, 34 kutoka Toronto, ni mfuasi wa programu mpya ya NewNew.

Chanzo cha picha, ANDRÉ PATRICK

Maelezo ya picha, André Patrick, 34 kutoka Toronto, ni mfuasi wa programu mpya ya NewNew.

Aliongeza kuwa: "Usalama wa wote katika jukwaa hilo la mawasiliano ndio kipaumbele chetu. Kampuni inapitia maudhui yote yanayowekwa na kuondoa yale ambayo hayastahili."

"NewNew ni programu mpya nzuri inayokuwezesha kuwa karibu na mtu, na pia inaonesha upande wa pili ambao ni nadra sana kuonekana," amesema.

Sasa basi, Je programu ya NewNew itakuwa kitu kikubwa kitakachofuata katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii? Utakuwa tayari kumuamulia nyota unayempenda chakula chake cha jioni na mengine mengi binafsi yanayomhusu?