Virusi vya corona: 'Mtoto wa miujiza' azaliwa mama yake akiwa amepoteza fahamu kabisa

Mwanamke aliyekuwa amepoteza fahamu kabisa kwasababu ya ugonjwa wa virusi vya corona wakati akiwa mjamzito amezungumzia vile alivyoamka kesho yake baada ya kumzaa mtoto kama jana.

Wakati Marria Ahmad alipokwenda hospitali ya Grange mnamo mwezi Januari baada ya kupatikana na virusi vya corona, hakuwa amebeba chochote kama vile nguo kama inavyokuwa mwanamke anapokwenda kujifungua kwasababu hakujua kwamba atakuwa hospitali kwa kipindi kirefu na pia muda wake wa kujifungua haukuwa umefika.

Akiwa na ujauzito wa miezi 29, yeye pamoja na mume wake Usman hawakuwa hata wameamua jina la mtoto wao wa pili.

Lakini hali ya Marriam ikabadilika kwa haraka sana.

Marriam ambaye ni msaidizi wa mwanasheria, mwenye matatizo ya ugongwa wa pumu, alijipata akiwa katika hali ya kukatisha tamaa.

"Ghafla, chombo changu cha oksijeni nilichokuwa ninatumia kikawekwa kutoa huduma hiyo kwa kiwango cha juu - sikuweza kusikia vizuri," amesema.

"Nilikuwa nasikia kelele tu. Nikasikia mmoja anaosha uso wangu, huyo bila shaka ni yule aliyekuwa nami hospitali kipindi hicho. Sikuwa na nguvu kabisa."

'Aga wapendwa wako'

Hapo ndipo daktari wake alipoanza kusema kuwa afanyiwe upasuaji na mwanzo akawa ameonya kuwa kuna hatari Marriam akapoteza fahamu kipindi chote hicho.

Lakini pia aliambiwa kuwa mtoto wake anaweza akakosa nguvu ya kunusurika kifo.

Kadiri siku ilivyokuwa inaendelea kusonga mbele, timu ya madaktari ilifanya uamuzi wa kuwa Marriam anahitajika kuwekwa katika hali ya kupoteza fahamu kabisa. Daktari wake alikuwa amemshika mkono wakati anasema "huenda asifanikiwe kurejea tena kuwa hai".

"Kila kitu kilitokea haraka sana," amesema. "Ilikuwa ndani ya dakika tano tu, waliniambia utakuwa unapumua kwa kutumia kifaa cha kupumulia, unafanyiwa upasuaji, mtoto atatoka lakini wewe utaendelea kuwa katika hali ya kupoteza fahamu, unaweza ukashindwa kurejea kuwa hai tena. Kwahiyo, aga wapendwa wako kabisa'."

Mariam alipigia simu wazazi wake huko Swansea na daktari akampigia simu mume wake ambaye alikuwa nyumbani huko Newport akiwa na mtoto wao wa mwaka mmoja Yusuf.

"Hata sikuzungumza na mume wangu wala mtoto wangu - Sijawahi kumuacha kijana wangu, hata usiku mmoja," alisema.

"Nilizungumza na wazazi wangu kupitia njia ya video. Ilikuwa ni kama dakika mbili hivi - Mama yangu aliuliza 'unasema nini?'. Nilikuwa mpweke niliye jawa na hofu."

Mtoto wa Marriam alizaliwa Januari 18 saa 20:27 za eneo akapewa jina la 'Ahmad' na kwa siku za kwanza za maisha yake, alikuwa na uzito kwa kilo 1 na gramu 1.7.

Lakini cha kushangaza ni kwamba licha ya onyo lilitolewa na daktari kufikia mchana siku iliyofuata, Marriam alikuwa ameamka yaani fahamu zake zimerudi.

"Sikujua nini hasa kimetokea" alisema. "Nilipoamka. Niliona sina chochote tumboni na nikawa mwenye maumivu mengi sana."

Wiki iliyofuata hakuweza kumuona mtoto wake. Lakini madaktari walimpigia picha na video ya mtoto wake na kumuonesha mtoto baada ya kutoka chumba cha wagonjwa mahututi na sasa kipindi hicho akiwa amesharejeshwa wadi ya kawaida akiendelea kupata afueni.

Mtoto wake alimpa jina imara

Na baada ya karibu wiki moja, Marrriam na mume wake Usman wakawa wanajitayarisha kumuona mtoto wake waliyempa jina la Khadija.

"Katika imani ya dini ya Kiislam, Khadija ni jina imara, mwanamke aliyejitegemea," Marriam alisema.

"Kwa mtazamo wangu, Khadija wangu alikuwa imara kweli. Hakuwa na matatizo yoyote licha ya kuzaliwa akiwa na wiki 29. Walikuwa wakiniambia kwamba atakuwa na kila aina ya matatizo. Lakini alikuwa mzima kabisa. Ilikuwa ni miujiza."

Na hatimaye baada ya kumuona mtoto wangu, nilihisi vipi?

"Nilimuona akiwa mzuri kweli kweli," amesema. "Hata kama alikuwa amewekwa waya kila sehemu akiwa tu amelala, 'nilimuona nikahisi kweli huyu ni mtoto wangu."

Na baada ya wiki nane hospitalini, Khadija aliruhusiwa kwenda nyumbani uzito wake ukiwa umeongezeka hadi kilo tatu unusu, mwenye afya na anayekuwa vizuri.

Marriam anakubali kuwa maisha yake na mtoto wake hajawahi kupata muda wa kufikiria kilichotokea.

"Namshukuru sana Mungu kwamba mtoto wangu yuko hai na mimi pia niko hai.

"Hata kama lilikuwa tukio la kuogopesha, lenye kufadhaisha nimejipata nikiwa mwenye shukrani zaidi kwa kile nilicho barikiwa nacho. Kuwa na muda tu na familia yangu.