Chanjo ya corona: Athari ya mabadiliko ya kipindi cha hedhi yachunguzwa

Wakati unapoelekea kupatiwa chanjo, huenda utaonywa kuhusu madhara , kama vile joto mwilini, kuumwa na kichwa, uchungu mkononi kwa siku moja au mbili .

Hatahivyo mabadiliko ya hedhi yako hayataorodheshwa katika orodha hiyo.

Wanawake mitandaoni kote duniani wameanza kuuliza iwapo hedhi za mapema , zenye uzito ama zile za maumivu huenda ni madhara yanayotokana na chanjo.

Dkt. Kate Clancey , alisambaza katika mtandao wa twitter uzoefu wake wa hedhi nzito isio ya kawaida baada ya kupatiwa chanjo ya Moderna na alipata madhara kama hayo.

Huku madaktari wenzake wa zamani kama vile Dkt Katherine Lee wakianzisha utafiti wa kutafuta maoni kutoka kwa watu, bado hatujui iwapo chanjo inasababisha mabadiliko hayo - Utafiti haujafanywa .

Kuna uwezekano kwamba wanawake wanaweza kuona mabadiliko baada ya kupatiwa chanjo hiyo hususan baada ya kusikia maono ya wanawake wengine.

Lakini Dkt Victoria Male , kutoka chuo cha Iamperial College London, alisema kwamba kuna uwezekano kwamba wanawake waliomaliza hedhi na wale wanaotumia homoni ambazo zinasitisha hedhi zao , wa meripoti kutokwa na hedhi.

Hivyobasi uhusiano kwamba huenda kuna madhara ya chanjo hiyo.

Idadi kubwa ya wanaume waliobadilisha jinsia na wanawake waliomaliza hedhi ambao huwa hawapati hedhi waliwasiliana na madaktari Clancy na Lee wakisema kwamba walitokwa na damu baada ya chanjo.

Na ijapokuwa uhusiano huo haujathibitishwa , kuna sababu chanjo hiyo huenda inasababisha mabadiliko katika hedhi.

Uhusiano wa kuaminika

Utandu wa tumbo ni sehemu ya mfumo wa kinga - kwa kweli kuna seli za kinga karibu kila sehemu ya mwili.

Seli za kinga zina jukumu katika kujenga, kudumisha na kuvunja utando wa uterasi - ambao unakuwa mzito kujiandaa kwa ujauzito, na kisha hutoka kwa njia ya hedhi iwapo yai halijatungishwa.

Baada ya chanjo, ishara nyingi za kemikali ambazo zina uwezo wa kuathiri seli za kinga huzunguka mwilini.

''Hii inaweza kusababisha utando wa tumbo kumwagika, na kusababisha kile ambacho huenda kikaonekana kama matoni ya damu'', Dk Male alielezea.

Hakuna uhusiano na kutoka kwa ujauzito

Hii haimaniishi kwamba hakuna uhusiano wowote na kutoka kwa ujauzito ijapokuwa wakati wa ujauzito mambo tofauti husaidia utandu wa tumbo ikiwemo kondo la nyuma - kiungo kinachounganisha usambazaji wa damu kati ya mtoto na mamake.

Hivi sasa kuna ushahidi mkubwa unaosema kwamba hakuna uhusiano kati ya chanjo hiyo na kutoka kwa ujauzito

Mbali na madhara katika utandu wa tumbo, wakati wa kutungwa mimba pia unaweza kuathiriwa na uvimbe , kwa mfano iwapo mtu ana joto dkt Alexandra Alvergne katika chuo kikuu cha Oxford anaelezea.

Hali hiyo huenda ikasababisha kuchelewa kwa hedhi.

Pia kuna Ushahidi kutoka kwa tafiti kwamba watu wenye ishara za uvimbe wanapata hedhi zinazoambatana na maumivu makali.

Watu wengine pia huripoti kupungua kwa seli zinazohusiana na mgando wa damu baada ya kupata chanjo , hatua ambayo inaweza kuathiri kutoka kwa damu nzito , alisema Dkt Lee.

Madhara yake ni ya muda

Mabadiliko ya hedhi sio suala la kuwa na wasiwasi kulingana na wataalamu wa masuala ya uzazi

Kuna ushahidi kutoka kwa chanjo za Flu na HPV kwamba zinaweza kuathiri kipindi cha hedhi kwa muda lakini hakuna madhara ya muda mrefu.

Na kuna ushahidi kwamba haziwezi kuathiri uzazi, Dkt Male anasema. Huku mabadiliko hayo yakiwa hayana kero, Dr. Male na wengine waliohojiwa wamesisitiza haja ya utafiti kufanywa kuhusu madhara ya chanjo katika hedhi ili watu wajue cha kutarajia.

''Kuna tatizo hapa kuhusu jinsi afya ya wanawake hupuuzwa'', alisema.

''Fikiria iwapo hujui kwamba joto mwilini linaweza kuwa athari za chanjo'', Dkt Jen Gunter ambaye ni mkunga aliandika katika tovuti yake The Vajenda.

Habari za uwongo kuhusu chanjo

Wakati huohuo dhana potofu kwamba chanjo huathiri hedhi imetumiwa na watu wanaosambaza habari mbaya kuhusu chanjo hiyo katika mitandao ya kijami.

Wale wasiopenda chanjo na makundi yenye nadharia potofu wamewasilisha ushahidi kuhusu watu waliopatwa na madhara baada ya kupata chanjo hiyo kama vile Dkt.Clancy .

Madai ya uongo kwamba kipindi cha hedhi cha wanawake kinaweza kuathiriwa kwa kuwa karibu na watu waliopatiwa chanjo zimevutia wengi katika mitandao ya kijami katika wiki za hivi karibuni.

Video moja kama hiyo , ilitazamwa na zaidi ya watu 300,000 tangu katikati ya mwezi Aprili , ikionesha daktari akiwaonya watumiaji kwamba hedhi za wanawake zinaathiriwa sana hata iwapo hawajapatiwa chanjo wao wenyewe. ".