Madaktari wanachunguza ugonjwa wa ajabu wa ubongo nchini Canada

Chanzo cha picha, Courtesy Steve Ellis
Madakjtari nchini Canada wamekuwa wakikutana na wagonjwa wanaoonesha dalili sawa na zile za ugonjwa wa ubongo unaojulikana kama Creutzfeldt-Jakob, ugonjwa ambao unaua kwa kushambulia ubongo. Lakini wakati walipojaribu kuuchunguza kwa ukaribu zaidi, kile walichobaini kiliwaacha vinywa wazi.
Takriban miaka miwili iliyopita, Roger Ellis alianguka akiwa nyumbani kutokana na mshituko katika siku ya maadhimisho yake ya miaka 40 ya ndoa.
Katika miaka ya sitini, Bw Ellis, ambaye alizaliwa na kukulia katika eneo la rasi ya New Brunswick Acadian, amekuwa mwenye afya hadi ilipofika mwezi Juni, na alikuwa akifurahia maisha yake ya kustaafu baada ya miongo ya kufanya kazi kama mekanika wa viwandani.
Mwanae wa kiume, Steve Ellis, anasema baada ya siku ile, afya ya baba yake ilidorora haraka.
"Alikuwa na mkanganyiko wa mawazo kuhusu mambo, kuona mambo ambayo hayapo, kupoteza uzito wa mwili, hasira na kurudia maneno ," anasema.
"Wakati mmoja hakuweza hata kutembea. Kwa hiVyo katika kipindi cha miezi mitatu tuliletwa hospitalini kuambiwa kuwa walikua wanaamini kuwa alikuwa anakufa-lakini hakuna mtu hata mmoja aliyejua ni kwanini."
Madaktari wa Roger Ellis kwanza walioshuku kuwa ulikuwa ni ugonjwa wa Creutzfeldt-Jakob [CJD].
CJD ni ugonjwa unaoua ni maradhi ya urithi yanayotokana kuvurugika kwa mfumo wa utendaji wa ubongo ambao huwafanya wagonjwa kuwa na dalili kama vile kupoteza kumbukumbu, mabadiliko ya tabia na kuwa na ugumu katika uratibu wa mawazo.
Mmoja unaofahamika zaidi ni aina ya CJD, ambayo inahusishwa na ulaji wa nyama za ng'ombe vichaa. CJD pia uko katika kundi moja na magonjwa mengine ya ubongo yanayovuruga utendaji wa ubongo kama Alzheimer, Parkinson na ALS, ambapo protini katika mfumo wa neva huwa zimefungwa vibaya na kukusanyika.
Lakini vipimo vya CJD vya Ellis vilirudi vikionesha hana ugonjwa huo, akafanyiwa vipimo vingine huku madaktari wakijaribu kuelewa hasa sababu ya ugonjwa wake.
Mwanae wa kiume anasema kundi la madaktari walifanya kila wawezavyo kuzuia dalili mbalimbali za baba yake lakini latizo lilibaki kutojulikana: nini kilikuwa nyuma ya kudorora kwa afya ya Bwana Ellis?.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwezi Machi mwaka huu, Bw Ellis akiwa kijana alikuwa na uwezekano wa kupata jibu la muda mfupi.
Radio-Canada,ambayo ni radio ya umma, ilipata nakala ya wizara ya afya ambayo ilikuwa imetumwa kwa maafisa wa matibabu ikiwaonya kuhusu kundi la wagonjwa waliokuwa wakionesha dalili zisizofahamika za ugonjwa wa ubongo.
"Kitu cha kwanza nilichoona ilikuwa ni: 'Huyu ni baba yangu,'" anakumbuka.
Roger Ellis sasa anaaminiwa kuwa mmoja wa wale waliokumbwa na ugonjwa huu na yuko chini ya uangalizi wa daktari Alier Marrero.
Daktari bingwa wa magonjwa ya ubongo Dkt Georges-L-Dumont katika kituo cha Chuo Kikuu cha Canada anasema madaktari mwanzoni walikutana na ugonjwa huo wa kushangaza mwaka 2015. Wakati huo alikuwa ni mgonjwa mmoja aliyekuwa na "ugonjwa wa kipekee ", anasema.
Lakini tangu wakati ule kumekuwa na wagonjwa zaidi wanaoumwa kama mgonjwa wa kwanza- wa kutosha kiasi kwamba madaktari wameweza kutambua ugonjwa huo kuwa kama hali tofauti au dalili "ambazo hazijawahi kuonekana kabla ".
Jimbo linasema kwa sasa kuna watu 48 wanaoumwa maradhi hayo, wanawake 24 na wanaume 24, wenye umri kati ya miaka 18 na 85. Wagonjwa hao wanatka katika rasi ya Acadian Peninsula na eneo la Moncton arla New Brunswick. Watu sita wanaaminiwa kuwa wamekwishakufa kutokana na ugonjwa huo.
Wagonjwa wengi walianza kuonesha dalili hivi karibuni, kuanzia mwaka 2018, ingawa mmoja anaaminiwa kuwa nao mwaka 2013.
Dr Marrero anasema dalili ni nyingi na zinaweza kuwa tofauti miongoni mwa wagonjwa.
Kwanza , kunaweza kuwa na mabadiliko ya tabia kama vile kuwa na wasiwasi, msongo wa mawazo, kukasirika, na kuwa na maumivu ya muda mrefu yasiyokuwa na sabab, maumivu ya misuli.
Mara kwa mara, wagonjwa hupata ugumu wa kulala- kukosa usingizi na kuwa na matatizo ya kumbukumbu. Kunaweza kuwa na hali ya kupoteza uwezo wa kuzungumza lugha haraka ambao unamgfanya mtu kushindwa kuwasiliana na kuzungumza vyema-na kuwa na matatizo kama kigugumizi au kurudiarudia maneno.
Dalili nyingine ni kupungua haraka kwa uzoto wa mwili, pamoja na matatizo ya kuona au tatizo la uratibu na mtiririko wa mawazo. Wagonjwa wengi huhitaji msaada wa kutembea kama fimbo au kiti ch walemavu.
badhi huwa na ndoto za kutisha, au ndoto zinazowafanya waamke na kutembea.
"Inasikitisha sana kwasababu, kwa mfano, mgonjwa anaweza kumwambia mke wake : 'Samahani mama huwezi kuingia kitandani, Mimi ni mume aliyeoa, hata kama mwanamke atamueleza jina lake, alisema: 'Wewe sio mke wangu halisi e,'" Dkt Marrero anasema.
Mtaalamu wa magonjwa ya ubongo wa Moncton anaongoza uchunguzi kuhusu hali hii, kwa usaidizi wa timu ya watafiti na shirika la afya ya umma la shirikisho.
Wagonjwa walifanyiwa vipimo vya prion na vipimo vya hali za Jeni za urithi, watafiti wanaangalia mkanganyiko wa kinga au aina za saratani, na uchunguzi wa vitu kama virusi, vimeta au kingamwili.
Wanaulizwa kuhusu hali ya mazingira, mtindo wao wa maisha, safari, matibabu na vyanzo vyao vya chakula na maji. Hupitia vipimo mbali mbali vya uti wa mgongo kwa ajili ya kubaini maambukizi na mvurugiko wa mfumo wake wa utendaji.
Hakuna tiba zaidi ya kusaidia kupunguza maumivu ya baadhi ya dalili. Kwa sasa, dhana ni kwamba ugonjwa huo mtu anaupata , sio wa urithi.
"Wazo letu la pamoja ni kwamba kuna aina ya sumu ambayo inapatikana katika mazingira ya mgonjwa huyu ambayo inasababisha mabadiliko,"anasema Dkt Marrero.

Chanzo cha picha, Getty Images
Daktari bingwa wa maradhi ya ubongo katika Chuo Kikuu cha British Columbia Dkt Neil Cashman ni moja wa madaktari wanaotaka kufichua chanzo cha maradhi haya ya ajabu.
Nadharia nyingine ni kwamba huenda wenye ugonjwa huo wameathiriwa na kile kinachoitwa "excitotoxin" aina ya asidi, ambayo ilihusishwa na tukio la chakula cha kilichowekwa sumu mwaka 1978 ambacho kilichafua misuli kwa sumukatika jimbo lililopo karibu la Prince Edward Island.
Kando na tatizo la maumivu ya sidi ya tumboni, karibu theluthi moja ya wale wanaoathiriwa walikuwa na tatizo , kama kupoteza kumbukumbu, kizunguzungu na mkanganyiko. Baadhi ya wagonjwa waliingia katika hali ya kupoteza fahamu, na wanne walikufa .
Dkt Cashman anasema pia wanaangalia sumu nyingine - beta-methylamino-L-alanine (BMAA) - ambayo inasemekana kuwa imesababishwa na hatari ya mazingira katika kusababisha magonjwa ya ubongo kama Alzheimer's na Parkinson's.
BMAA hutengenezwa na bacteria, wanaofahamika zaidi kama blue-green algae.

Chanzo cha picha, Courtesy Steve Ellis
Dkt Marrero anasema maradhi yaliyopatikana nje ya mikoa miwili - rasi ya Acadian , yanatoka katika jamii za wavuvi na fukwe za michanga, na Moncton, kituo cha jiji - ambako wagonwa wamebainika kwa sasa
"Je tunaona uwezekano wa barafu? Labda," anasema. "Ninatumai tunaweza kuparta chanzo chake ili tuweze kuzuia hili ."
Huku wale wanaoishi katika jamii zilizoathiriwa wana hofu inayoeleweka, Dkt Marrero anawataka watu ku "fanya kazi kwa tumaini sio kwa hofu. hofu inathoofisha."
Hali ya Roger Ellis imeimarika tangu tangu alipougua sana, mwanae wa kiume anasema.
Yuko katika makazi ya huduma ya kipekee na anahitaji msaada kwa ajili ya shughuli za kila siku, na anahangaika kuzungumza na kulala.
Unaweza pia kusoma:
Steve Ellis, ambae ana mtandao wa Facebook unaotoa usaidizi wa familia zenye matatizo haya, anasema anataka maafisa wa serikali kujitolea kuwa wakweli kuhusu ugonjwa huu.
Kubwa zaidi anataka kujua ni nini kilichomfanya baba yake augue.
"Ninafahamu kuwa wanashughulikia hilo, lakini ni vipi hii ilitokea ?" anasema.
"Kama famili, tunatambua sana ukweli kwamba huenda akafa kutokana na ugonjwa huu, na tunatumai kwamba iwapo itatokea kabla hajafa au baada ya hilo kuwe kuna majibu-na uwajibikaji kama ni kitu ambacho kingeweza kuzuiwa ."













