Unawezaje kuzuia ubongo usizeeke haraka?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ubongo ni kiungo kama sehemu nyingine ile ya mwili na pia huzeeka kadiri mtu anavyokua.
Tunapotaka kusalia wachanga sio kwamba tunachukia makunyanzi ya usoni lakini ni kujilinda dhidi ya maradhi yanayotokana na uzee.
Utabiri umedhihirisha kwamba ifikapo mwaka 2050, asilimia 25 ya idadi ya wazungu watakuwa zaidi ya miaka 65 na watu mwenye umri wa miaka 80 itaongezeka mara tatu.
Lakini je kuna njia za kuwa kijana katika ubongo wako?
Ingawaje hatuwezi kurudisha wakati wa nyuma, tunaweza kufanya hivyo kwa kuzingatia mbinu bora za kiafya ili kupunguza athari zitokanazo na kuzeeka.
Uzee ni nini?
Uzee unaweza kufafanuliwa kama mabadiliko yanayotokana na umri na kupunguza kasi ya utendaji kimwili na akili.
Pia husababisha magonjwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Cheti chako za kuzaliwa kinadhihirisha wakati ulivyopita tangu kuzaliwa kwako.
Hata hivyo, kuna umri kutegemea na akili, kunakotegemea na hali ya mwili na unaweza kuwa mchanga kuliko umri halisi ikiwa utajitunza vizuri ama ukawa umezeeka zaidi kuliko hata umri wako wenyewe ikiwa utajiachilia.
Kukomaa kwa ubongo
Kadri umri unavyooongezeka, ubongo hupungua, neva inayopeleka habari akilini hupunguza utendaji na uzalishaji wa homoni na mishipa kwenye ubongo huanza kutofanyakazi vizuri.
Sababu nyengine ya ubongo kuzeeka ni kujikusanya kwa protini ambapo huzunguka pande za ndani na nje ya mishipa ya ubongo.
Hii husababisha magonjwa ya kiakili kama Alzheimer au ugonjwa wa kutetemeka wa Parkinson.
Ifahamike kuwa ugonjwa wa kiakili wa dementia umepitwa na wakati. Uzee hauna uhusiano na ugonjwa wa dementia au hali ya kusahau.

Iwapo kutakuwa na matatizo ya kusahau na kuelewa kwa kiwango fulani, hali hiyo inaweza kuhusishwa na ugonjwa maalum na sio hali ya kawaida ya ubongo kuzeeka.
Mambo ya kuzingatia kupunguza kasi ya kuzeeka
Lishe bora ni muhimu sana.
Lishe bora inayopendekezwa ni Mediterranea, ambayo huusishwa na ulaji wa kiwango kidogo cha nyama na kuku, maziwa, divai kidogo na utumiaji wa mafuta ya mzeituni, ulaji mkubwa wa mboga mboga, nafaka matunda na samaki.
Lishe hii ya Mediterranea imeonyesha kupunguza hatari ya kupatwa na matatizo ya kiakili kama vile ugonjwa wa Alzheimer.
Pia kupunguza viwango vya kalori kunaweza kupunguza kasi ya kuzeeka.
Aidha mbali na kulala saa nane kwa siku, uzingatia mzunguko mzuri wa wakati wa kulala na kuamka, ni muhimu kwa kazi zinazofanywa na ubongo, mfano, kutoa uchafu kutoka akilini ambao umejikusanyika siku nzima.
Wakati tunapolala nafasi katika mshipa ya akili huongezeka na kuimarisha ufanyakazi wa ubongo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hivyobasi, kuhakikisha unakuwa na ratiba ya kulala kunasaidia katika suala zima la kuzeeka.
Mazoezi ya mara kwa mara pia ni muhimu katika kupunguza athari za kuzeeka.
Utafiti unaonesha kwamba mazoezi ya viungo kuna jukumu muhimu katika ubonga kufanyakazi vizuri na pia kunapunguza kasi ya kupungua kwa ubongo na kuimarisha utenda kazi wake.
Hususan, kufanya mazoezi ya viungo kunaimarisha utendakazi wa ubongo sio tu kupunguza kuzeeka lakini pia unapunguza hatari ya kupata ugonjwa unaodhoofisha chembe za neva na ambao hauna tiba.
Kwa upande mwingine, imethibititshwa kwamba watu wenye kiwango cha juu cha elimu au ambao wanadumisha shughuli za kitaaluma - kama kusoma au kupata ujuzi fulani - uwezekano wa wao kupata ugonjwa wa dementia uko chini sana.
Mambo mengine ya udumishaji afya njema pia yanaweza kusaidia kupunguza athari za kuzeeka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Punguza kiwango cha pombe unachokunywa.
Jiepushe na uvutaji sigara na kadhalika.
Huku ikiwa kunywa kiwango kikubwa cha pombe kunaweza kuhatarisha utendaji wa akili, vinywaji vingine vya pombe vinaweza kuwa na manufaa katika udumishaji wa afya njema ya kiakili mfano ukinywa divai.
Uvutaji singara bila shaka ni tabia ambayo inastahili kuepukwa, kwasababu inahusishwa na kuongeza kasi ya kuzeeka kwa ubongo na matatizo ya kiakili na dementia.
Udumishaji wa kufanya mazoezi na utendaji wa ubongo unategemea kwa kiasi kikubwa, mishipa ya damu.
Shinikizo la juu la damu, mafuta kuziba mishipa ya damu na kiwango cha juu cha kolesteroli kunaongeza uwezekano wa akili kushindwa kufanyakazi vizuri, kuharusi na dementia.

Chanzo cha picha, Getty Images
kunaongeza uwezekano wa akili kushindwa kufanyakazi vizuri, kuharusi na dementi
Pia, ugonjwa wa kisukari na kunenepa kupita kiasi kunaathiri mmeng'enyo wa glukosi na kufanya chembe za mwili kutopokea insulini.
Yote hayo yanaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa mishipa ya ubongo na kuongeza kasi ya kuzeeka.
Aidha, uwazee wengi wanakuwa na ugonjwa wa sonona ambako husababisha ukosefu wa uwiano kwenye mishipa ya ubongo yaani molekuli zinazotumiwa na mishipa ya ubongo kuwasiliana.
Kwa muda mrefu, usumbufu huu unaweza kusababisha ubongo kutofanyakazi vizuri.
Kwa kifupi, msingi wa kuhakikisha unakuwa na afya njema na ubongo wako kuendelea kuwa mchanga ni sawa na kiungo kingine chochote cha mwili.
Yaani, unahitajika kupata lishe bora, lala usingizi saa za kutosha zinazohitajika, epuka kunywa pombe kupindukia, usivute sigara na pia upuka kuwa na msongo wa mawazo na fanya mazoezi kiasi.












