Dementia: Mtindo wa maisha unaweza kuzuwia hatari za matatizo ya akili

Mazoezi ya mwili ni moja ya njia za kupunguza hatari ya kupata maradhi ya kiakili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mazoezi ya mwili ni moja ya njia za kupunguza hatari ya kupata maradhi ya kiakili

Karibu kila mmoja anaweza kupunguza ugonjwa wa matatizo yanayotokana na kuathirika kwa akili (dementia), hata kama ni ya kurithi katika familia ,kulingana na utafiti wa maisha ya kiafya.

Utafiti wa watu karibu 200,000 unaonyesha hatari ya kupata matatizo ya kiakili ikishuka kwa kwa kiwango cha robo tatu.

Watafiti kutoka Chuo kikuu cha Exeter wanasema matokeo ya ya utafiti wao yalikuwa ni ya kusisimua, kutia msukumo na yalionyesha kuwa watu hawawezi kuhangaishwa na hofu ya kupata maradhi ya kuathirika kwa akili (dementia).

Matokeo yalifichuliwa katika Kongamano la Kimataifa la Jumuiya ya magonjywa yanayodumaza akili yanayofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama -alzheimer's

Ni maisha gani yanayotambuliwa kuwa ni ya kuzingatia afya?

  • Watafiti waliwapa alama watu juu ya mtindo wa maisha kwa kuzingatia mazoezi ya mwili , lishe, pombe na uvutaji sigara
  • Huu ni mfano wa mtu aliyepata alama za nzuri:
  • Havuti sigara kwa sasa
  • Huendesha baiskeli kwa kasi ya kawaida kwa muda wa saa mbili na nusu kwa wiki.
  • Hula mlo kamili ambao unajumuisha aina tatu za matundana mboga kwa siku nani nadra lkula nyama za kusindikwa.
  • Hunywa glasi moja ya bia kwa siku.
  • Ni mvutaji wa sigara mara kwa mara
  • Hafanyi mazoezi ya mara kwa mara
  • Hula chakula chenye matunda chini ya mara tatu na mboga kwa wiki, na hujumuisha mara mbili au zaidi nyama za kusindikwa na nyekundu kwenye mlo wake kwa wiki.
  • Hunywa walau glasi tatu za bia kwa siku
Sue Taylor ambaye mama yake na bibi yake walipatwa na matradhi ya kiakili anasema mazoezi ni muhimu

Chanzo cha picha, SUE TAYLOR

Maelezo ya picha, Sue Taylor ambaye mama yake na bibi yake walipatwa na matradhi ya kiakili anasema mazoezi ni muhimu

Sue Taylor, mwenye umri wa miaka 62, kutoka eneo la Exeter, ameshuhudia athari za dementia katika familia- mama yake na bibi yakewalikuwa na maradhi hayo ya kiakili.

Anahudhuria darasa la mazoezi ya mwili kwenye bustani mara tatu kwa wiki - hata katika katika majira ya baridi - na hutembea kwa muda wa dakika 45-kabla ya kwenda kazini.

" Inahitaji juhudi kubwa, unapaswa kufikiria kuhusu mazoezi haya na kuhakikisha yanaingia akilini na maishani mwako ," anasema.

Lakini anasema faida zake ni muhimu, hususan kwa wajukuu wake.

"ninataka tu kutunza akili yangu katika hali nzuri kwa muda mrefu iwezekanavyo.

Sitaki wajukuu wamkose bibi kimwili na kiakili ," anasema.

Lakini je maisha bora ya kiafya yanaleta utofauti gani?

Utafiti ulifuatilia maisha ya watu 196,383 wenye umri kuanzia miaka 64 kwa muda wa miaka minane.

Ulitathmini vipimo vya vinasaba (DNA) vya watu kupima hatari za maumbile yao ya urithi za kupata hatari ya ugonjwa.

Utafiti huo ulionyesha kuwa kuna visa 18 vya maradhi ya dementia kati ya watu 1,000 ikiwa watazaliwa na jeni za ugonjwa na baadae kuishi mtindo wa maisha ya kutozingatia afya.

Lakini kiwango hivho kilishuka hadi kufikia visa 11 kati ya watu 1,000 wakati wa utafiti, ikiwa watu hao wenye hatari ya kupatwa na ugonjwa huo wangeishi mtindo wa maisha unaozingatia afya.

Huenda idadi ikaonekana kuwa ni ndogo, lakini hiyo ni kwasababu watu wenye umri wa miaka chini ya 70 huwa ni wanakuwa na uwezekano mdogo wa kupata maradhi ya dementia yanayoathiri akili.

Watafiti wanasema kuwa kupunguza viwango vya dementia kwa kiwango cha theluthi moja duniani kunaweza kuwa na athari nzuri miongoni mwa watu wenye umri wa uzee ambao kMgonjwa apasuliwa ubongo kimakosa hospitalini Kenya wa kawaida huathiriwa na ugonjwa.

"Kiwango hicho kinaweza kuwa ni maelfu ya watu ," Dr David Llewellyn, aliiambia BBC.

Pia aina hii ya utafiti haiwezi kuidhinisha moja kw amoja sababu za mtindo wa maisha unaosababisha hatari tofauti za dementia. Ni sehemu chache katika data zilizobainika.

Lakini matokeo, yaliyochapishwa katika jarida la shirika la kitabibu la Marekani (Journal of the American Medical Association) yamefanana na yale ya utafiti na ushauri wa Shirika la afya duniani.

Je unaweza kuepuka dementia kabisa?

La kusikitisha ni kwamba, unaweza kuishi maisha ya mtakatifu, lakini bado ukapata ugonjwa huu. Mtindo wa maisha hubadili tu tabia mbaya.

Hata hivyo , hakuna dawa za kubadili sababu ya ugonjwa huu.

Kupunguza uwezekano ya kuupata ndicho kila mtu anachoweza kukifanya.

Hii hutokea kwa kila mtu?

Matokeo huenda yasiwe sawa kwa kila mtu kwa watu wote miongoni mwa watu wenye umri wa miaka juu ya 40 na juu ya 50 ambapo ndipo mtu anaweza kuupata, wanasema watafiti.

Ni ujumbe gani muhimu?

"hata kama una wasi wasi juu ya dementia, labda una historia ya ugonjwa hu katika familia yako, utafiti huu unasema haijalishi kuwa pia utaupata , Dkt. David Llewellyn, ameiambia BBC.

" Bado una uwezekano wa kupunguza hatari ya dementia kama utaweza kuishi maisha ya kiafya.

"Hilo kusema kweli linnatia moyo."

Mtafiti mwenzake Dkt Elzbieta Kuzma amesema mara ya kwanza kwa mtu lkukuonyesha kuwa unaweza kukabiliana na hatari ya urithi wa dementia na matokeo yake "yanasisimua".

Kupotea kwa nyama ya ubongokutokana na dementia (Kushoto) ikilinganishwa na ubongo wneye afya (Kulia)

Chanzo cha picha, SPL

Maelezo ya picha, Kupotea kwa nyama ya ubongokutokana na dementia (Kushoto) ikilinganishwa na ubongo wneye afya (Kulia)

Wataalamu wanasema nini ?

Fiona Carragher, kutoka shirika la kukabiliana na magonjywa ya ubongo na akili -Alzheimer's Society,alisema: "kwa hali iliyopo sasa ya kwamba mtu mmoja kupata dementia kila baada ya dakika tatu nchini Uingereza , kufahamu jinsi ya kupunguza hatari za dementia ni jambo muhimu sana''.

"Kwa hiyo kula mboga, badala ya kunywa mchanganyiko wa vileo , kunywa mchanganyiko wa sharubati juisi ya matunda na chukua vifaa vyako vya mazoezi ukafanye mazoezi ya mwili!"

Dr Carol Routledge, kutoka kituo cha utafiti wa magonjywa ya akili nchini Uingereza- Alzheimer's Research UK, anasema matokeo ya utafiti ni "muhimu".

"huu ni ushahidi mwingine zaidi kwamba kuna mambo ambayo sote tunaweza kuyafanya kupunguza hatari ya kupata ugonjwa , huku asilimia 34% pekee ya watu wazima wakidhani kuwa hili linawezekana.

"japo hatuwezi kubadili Jeni tulizorithi, utafiti unaonyesha kuwa kubadili mtindo wetu wa maisha bado kunaweza kusaidia kuleta mabadiliko ya mambo mabaya kwa ajili ya manufaa yetu ."