Msichana aliyetelekezwa China kuwa mlimbwende maarufu duniani

Xueli

Chanzo cha picha, @Luxvisualstorytellers

Wakati Xueli alipokuwa mtoto, wazazi wake walimtelekeza katika bustani ya nyumba ya kulelea yatima.

Nchini China, kuwa albino ni laana.

Hali hiyo adimu ya kimaumbile imemfanya msichana huyo kuwa na ngozi na nywele tofauti.Na kumfanya kuwa makini sana na mwanga wa jua.

Lakini muonekano wake wa tofauti umemuwezesha kufanikiwa kuingia katika tasnia ya ulimbwende . Sasa ana miaka 16 na ameweza kuonekana kwenye jarida maarufu duniani la Vogue na katika kampeni nyingi za matangazo ya wabunifu wengi wa kubwa.

Kituo cha yatima walimpa jina la Xue Li. Xue ikimaanisha theluji na Li mrembo. Niliasiliwa nikiwa na miaka mitatu na kwenda kuishi na mama na dada zangu huko Netherlands.

Mama yangu alisema hakuna jina zuri zaidi kwangu kuliko nililokuwa nalo.

Nilidhani ni vyema kuendelea kutunza kumbukumbu ya eneo nililotoka.

Xueli

Chanzo cha picha, Biel Capllonch

Wakati nilipozaliwa nchini China, serikali ilikuwa imeweka sheria ya kila familia kuwa na mtoto mmoja.

Hivyo ilikuwa ni bahati mbaya sana kwa mtu kuwa na mtoto mwenye ualbino.

Kuna wengine kama mimi walitelekezwa , wengine walifungiwa na kama wakipelekwa shule, nywele zao zilipakwa rangi.

Lakini katika baadhi ya mataifa ya Afrika, albino wanauawa, viungo vyao vinakatwa.

Waganga wa kienyeji wanatumia mifupa yao kutengeneza dawa, huku watu wengi wakiamini kuwa ni tiba.

Lakini si kweli, hizo ni imani potofu tu.

Nilikuwa na bahati kuwa nilitelekezwa.

Xueli

Chanzo cha picha, Jet van Gaal

Wazazi wangu wa asili hawakuacha taarifa kuhusu mimi hivyo sijui hata siku yangu ya kuzaliwa ni lini.

Lakini mwaka mmoja uliopita nilifanyiwa X-ray katika mkono wangu na wakapata wazo la lini nilizaliwa na daktari alidhani kuwa ni karibu na miaka 15 iliyopita.

Nilianza kazi ya ulimbwende nikiwa na miaka 11 . Mama yangu aliwasiliana na mbunifu ambaye alikuwa na asili ya Hong Kong.

Aliamua kubuni mitindo ya nguo kwa ajili yangu ambayo iliniacha watu wengi kuwa mdomo wazi.

Xueli modelling for Kurt Geiger

Chanzo cha picha, Kurt Geiger

Aliita kampeni yake "perfect imperfections" na aliniuliza kama ninaweza kwenda kwenye maonesho Hong Kong. Nilifurahia sana.

Baada ya hapo nilialikwa katika kazi nyingi za picha na moja ilikuwa ya Brock Elbank huko London.

Aliweka picha zangu nyingi mtandaoni na wakala wa walimbwende Zebedee aliwasiliana name kuniomba kama ntaweza kujumuika katika mradi wa walemavu katika sekta ya fasheni.

Xueli Abbing

Chanzo cha picha, Marcel Schwab

Picha moja ilitoka kwenye jarida la Italia la Vogue mwaka 2019.

Wakati huo sikujua umuhimu wa jarida lile na ilinichukua muda kuelewa kwanini watu wamefurahi sana kuhusu mimi kuonekana katika jarida lile.

Katika ulimbwende, kuonekana tofauti ni baraka na sio laana na nmepata jukwaa la kuwaelimisha watu kuhusu ualbino.

Kampeni ya Kurt Geiger ni mfano mzuri unaoruhusu kuonesha utofauti wangu.

Ninaweza kujielezea namna nnavyoweza na ninajivunia na matokeo yake.

Walimbwende wenye ualbino mara nyingi huwa wanapewa taswira za kusadikika kama malaika au shetani, na jambo hilo linanisikitisha.

Haswa kwasababu ya imani potofu ambazo zimeweka hatarini maisha ya watoto wenye ualbino katika nchi kama Tanzania na Malawi.

Xueli

Chanzo cha picha, Rob Jansen

Anasema anapenda ulimbwende kwa kuwa unampa fursa ya kukutana na watu wapya, kujifunza kiingereza na kuona watu wakifurahi kuona picha zake.