Israel: Mabaki ya kipekee ya Biblia yapatikana pangoni

Officials look at fragments of scroll found in the Cave of Horror

Chanzo cha picha, Israel Antiquities Authority

Maelezo ya picha, Vipande vya ngozi vilikuwa na maandiko kutoka kitabu cha nane na cha mwisho cha kitabu cha Waebrania

Mabaki ya machapisho ya Biblia ya kale imepatikana katika kile maafisa wametaja kuwa "uvumbuzi wa kihistoria" katika mapango ya jangwani nchini Israel.

Makumi ya vipande vya karatasi ziliandikwa kwa Kigiriki, jina la Mungu likionekana kwa Kihibru.

Machapisho hayo yanayoaminiwa kuwa ya waasi wa kiyahudi waliokimbilia milimani baada ya kuibuka kwa upinzani dhidi ya utawa wa Kirumi katika karne ya pili.

Zilipatikana wakati wa oparesheni ya kuhifadhi eneo hilo la pangoni lisivamiwe.

Fragments of parchment found in the Cave of Horror

Chanzo cha picha, Israel Antiquities Authority

Maelezo ya picha, Maneno hayo yaliandikwa kwa Kigiriki, isipokua jina la Mungu, ambalo liliandikwa kwa Kihibru

Uvumbuzi huo ni wa kwanza kupatikana tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960 wakati mabaki kama hayo na mifupa 40 ilipatikana katika eneo hilo ambale limepewa jina pango la ajabu.

Mabaki yaliyopatikana yana machapisho kutoka ya Zakayo na Nahum, ambayo yanajumuisha sehemu ya maandiko yanayojulikana kama kitabu cha mitume 12 wadogo.

Mabaki ya ngozi yalikua yameandikwa kwa Kigiriki, lugha iliyotumiwa baada ya ushindi wa Yudea na Alexander the Great katika karne ya nne kabla ya ujio wa Kirstu. Jina la Mungu, hata hivyo linaonekana kuandikwa kwa Kihibru.

Mkurugenzi wa mamlaka ya mambo ya kale ya Israel (IAA), Israel Hasson amesema mabaki hayo na vitu vingine vilivyopatikana hapo ni ya "thamani kubwa ya mwanadamu".

Shehena ya shilingi za kale kutoka zama za uasi wa Kiyahudi, Mfupa wa mtoto uliodumu miaka 6,000-na kapu la kale lililotengezwa karibu miaka 10,500 iliyopita pia ilipatikana katika eneo hilo.

Coins found in the Cave of Horror

Chanzo cha picha, Israel Antiquities Authority

Maelezo ya picha, Sarafu iliyotumiwa na waasi wa Kiyahudi wakati wa uasi dhidi ya Roma ilipatikana
Mummified child's skeleton found in the Cave of Horror

Chanzo cha picha, Israel Antiquities Authority

Maelezo ya picha, Mfupa wa mtoto uliodimu, karibu miaka 6,000, pia ilipatikana
Ancient basket found in the Cave of Horror

Chanzo cha picha, Israel Antiquities Authority

Maelezo ya picha, Kapu kubwa linalosadikiwa kuwa la kale zaidi duniani pia lilikua miongoni mwa vitu vilivyopatikana katika pango hilo

Pango hilo lililopo chini ya mlima, haliwezi kufikiwa kirahisi isipokuwa timu ya wa wataalamu walio na ujuzi.