Wanaakiolojia wamepata mageneza 20 ya kale Misri

Majeneza ya kale ya Misri yapatikana Theban necropolis of Asasif, near Luxor

Chanzo cha picha, Egypt Antiquities Ministry

Maelezo ya picha, Maelezo zaidi kuhusu majeneza hayo yatatolewa siku ya Jumamosi

Wanaakiolojia wamepata zaidi ya majeneza ya 20 ya kale karibu namji wa Luxor nchini Misri, wizara ya mambo ya zamani inasema.

Majeneza hayo yaliyo na rangi ya kuvutia na ambayo bado michoro yake inaonekana, yalipatikana eneo la Asasif, katika ukingo wa magharibu wa mto Nile.

Zilikuwa kwa matabaka mawili huku ile ya juu ikipitana na ile ya chini .

Wizara hiyo imetaja ugunduzi huo kama "moja ya ugunduzi muhimu" katika miaka ya hivi karibuni.

Maelezo ziadi kuhusu majeneza hayo yatatolewa kwa vyombo vya habari siku ya Jumamosi.

Ancient Egyptian coffins uncovered at the Theban necropolis of Asasif, near Luxor

Chanzo cha picha, Egypt Antiquities Ministry

Ancient Egyptian coffins uncovered at the Theban necropolis of Asasif, near Luxor

Chanzo cha picha, Egypt Antiquities Ministry

Makaburi mengi katika eneo la Asasif, ambalo liko karibu na bonde la Kings, ni ya kale (664-332BC) Misri.

Wiki iliopita, wizzara ya vito za kale ilitangaza kuwa wanaakiolojia wamevumbua ''eneo la viwandani'' la kale katika bonde la magharibi mwa Luxor.

Eneo hilo lilijumuisha "nyumba za kuhifadhi na kuosha samani, nyingi wazo zilikuwepo tangu utawala wa kifalme wa karne ya 18", ilisema.

Map: Map of Egypt