Vimelea hatari vya malaria 'vilivyoruka' kutoka kwa sokwe hadi kwa binadamu

Gorilla

Chanzo cha picha, Getty Images

Msururu usio wa kawaida wa matukio uliibua aina hatari ya malaria kutoka kwa sokwe "kuhama" na kuanza kushambulia binadamu, kwa mujibu wa wanasayansi.

Maelfu ya watu hufariki kutokana na malaria kila mwaka kutokana na vimelea vya Plasmodium falciparum -aina ambayo ilifanyiwa uchunguzi na watafiti - akichangia visa vingi.

Sokwe ndio waliokuwa 'wakibeba' vimelea hiyo.

Lakini mabadiliko yaliyotokana na maumbile miaka elfu 50 iliyopita iligeuka kuwa tishio kwa wanadamu, wataalam wamegundua.

kuumwa na mbu

Matokeo ya utafiti uliochapishwa katika jarida la PLoS Biology, huenda ikavumbua njia mpya ya kukabiliana na malaria, watafiti wa Taasisi ya Wellcome Sanger wanatumai.

Malaria husababishwa na Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vijidudu kitaalamu viitwavyo Plasmodium

Husambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au wanyama baada ya kuumwa na mbu jike wanaokuwa wakitafuta damu kwa ajili ya chakula.

Mtu anapoumwa huugua homa kali.

Kuna aina tofauti ya vijidudu hivyo na moja kati ya vile vinavyoathiri binadamu peke yake ni Plasmodium falciparum.

Ilihama kutoka kwa sokwe mtu na wakati sawa na ule ambao binadamu walihama kutoka Afrika, miaka kati ya 40,000 hadi 60,000 iliopita, watafiti wanasema.

girl holding a sign saying 'malaria kills'

Chanzo cha picha, Getty Images

Vijidudu hivyo huathiri seli kwenye ini na chembechembe nyekundu za damu, na kusababisha dalili nyingine ikiwemo upungufu wa damu.

Hatimaye ugonjwa huathiri mwili mzima, ikiwemo ubongo na unaweza kuua.

Takriban watu 435,000- wengi wao watoto- hufa kutokana na malaria kila mwaka.

Uchunguzi wa jeni za kale za vijidudu tofauti vinavyosababisha malaria, uliangazia zaidio jeni moja iliofahamika kama rh5 - sehemu muhimu ya chembe chembe ya vinasaba DNA ambayo huwezesha malaria kushambulia celi nyekundu katika mwili wa binadamu.

Ni moja ya tafiti ambazo madaktari wanatumia kutengeneza chanjo mpya ya malaria.

Watafiti wanaamini maelfu ya miaka iliopita, aina mbili za vimelea vya malaria vilitokea kuambukiza sokwe na wakabadilishana vitu vya maumbile kati yao.

Mbu

Chanzo cha picha, Getty Images

Plasmodium falciparum ilichagua jeni aina ya rh5.

Mmoja wa watafiti hao Dr Gavin Wright anasema: "Hii ilikuwa tukio ambalo sio la kawaida ambayo ilichangia ongezeko la vifo kwa binadamu.

"Tumeshangazwa sana na matokeo hayo. Ilikuwa na matokeo chanya kwasababu inashabihiana na tafiti zingine zilizofanywa na na wenzetu . Ilibainisha maelezo kuhusu jinsi vijidudu hivyo vilivyooka kwa sokwe na kuingia kwa binadamu.

"Rh5 kwasasa ni chanjo muhimu katika kiwango cha damu cha mtu ambaye anaweza kupata malaria kwa hio tukipata maelezo zaidi kuhusu jeni hii, inaweza kutusaidia katika juhudi za kukabiliana na ugonjwa huu."

Alisema uwezekano wa vijidudu hivyo kuendlea kuzaana muda mfupi baadae ni "kidogo sana", japo hilo kihalisia inasemekana kuna uweze kano huo.

Karibu nusu ya watu duniani wanakabiliwa na tisho la kupatikana na malaria.

Vifo vingi vinavyotokana na malaria hasa kwa watoto katika eneo la Jangwa la Sahara barani Afrika husababishwa na Plasmodium falciparum.